23% YA WATOTO NCHINI WANASUMBULIWA NA UGONJWA WA MATUNDU YA MOYO

23% YA WATOTO NCHINI WANASUMBULIWA NA UGONJWA WA MATUNDU YA MOYO

Like
313
0
Friday, 22 April 2016
Local News

IMEELEZWA kuwa asilimia 23 ya watoto nchini wanasumbuliwa na ugonjwa wa matundu ya moyo ambao umekuwa ni moja kati ya magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo vingi vya watoto.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini dar es salaam leo Daktari bingwa wa Magonjwa ya moyo kutoka kitengo cha moyo cha Jakaya Kikwete, Peter Richard amesema kuwa dalili zinazoashiria uwepo wa ugonjwa huo kwa mtoto ni pamoja na kushuka kwa kiwango cha ukuaji na homa kali za mapafu zinazojitokea mara kwa mara.

Dokta Richard ameongeza kuwa endapo mzazi ataona mtoto anatembea kidogo na kuchoka au kushindwa kucheza na wenzake ni vyema kumuwahisha hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi haraka.

Comments are closed.