ALIYEKUWA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA BOUTROS-GHALI AFARIKI DUNIA

ALIYEKUWA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA BOUTROS-GHALI AFARIKI DUNIA

Like
255
0
Wednesday, 17 February 2016
Global News

UMOJA wa Mataifa umetangaza kuwa aliyekuwa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Boutros Boutros-Ghali amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 93.

Mmisri huyo, aliyekuwa katibu mkuu wa kwanza kutoka Afrika pamoja na Ulimwengu wa Kiarabu, alifariki dunia jana mjini Cairo, kutokana na maradhi yasiyojulikana.

Wakati akisifiwa kwa operesheni ya kwanza kubwa ya msaada wa dharura kuwahi kufanywa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuwaisaidia waathiriwa wa baa la njaa nchini Somalia, uongozi wake ulikosolewa kutokana na Umoja wa Mataifa kushindwa kuchukua hatua wakati wa mauaji ya halaiki nchini Rwanda mwaka wa 1994 .

Comments are closed.