Author: EFM

  • MFUMUKO WA BEI

    MFUMUKO WA BEI

     

    Dar es Salaam. Watumiaji magari, mashine na mitambo inayotumia petroli na dizeli watapata ahueni baada ya bei ya bidhaa hizo kupungua, huku bei ya mafuta ya taa ikipanda.
    Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), jana ilitangaza kushuka kwa bei ya petroli na dizeli kwa asilimia 2.7 na asilimia 3.8; na ongezeko la asilimia 0.09 kwa mafuta ya taa.
    Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Nzingagwa Mchany ilisema bei hizo mpya zitatumika Tanzania Bara kuanzia leo.
    Hata hivyo, kwa watumiaji wa mafuta yanayopitia katika Bandari ya Dar es Salaam ni neema, lakini wa Bandari ya Tanga bei imeongezeka.
    Mchany alisema mabadiliko hayo ya yanatokana na kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na marekebisho ya bei yaliyofanywa na Ewura kutokana na kubadilika kwa tozo za wakala na Serikali za mitaa katika bidhaa hizo.
    Ikilinganishwa na tangazo la bei ya mafuta la Aprili 4 kwa mafuta yanayopitia katika Bandari ya Dar es Salaam, bei ya petroli imepungua kwa Sh88 kwa lita (asilimia 3.8) na dizeli Sh61 kwa lita (asilimia 2.75); huku bei ya mafuta ya taa ikiongezeka kwa Sh2 kwa lita sawa na asilimia 0.09.
    Tofauti na wanunuzi wa rejareja, bei ya wale wa jumla upande wa petroli imepungua kwa Sh100.91 kwa lita (asilimia 4.58), dizeli Sh73.71 kwa lita (asilimia 3.52) na mafuta ya taa Sh10.49 kwa lita sawa na asilimia 0.51.

  • Donald Trump alijitungia barua kuhusu afya yake, daktari Harold Bornstein asema

    Donald Trump alijitungia barua kuhusu afya yake, daktari Harold Bornstein asema

    Aliyekuwa daktari wa Donald Trump amesema kwamba si yeye aliyeiandika barua iliyomweleza mgombea huyo wa chama cha Republican wakati huo kuwa aliyekuwa na “afya nzuri ajabu”, vyombo vya habari Marekani vinasema.
    “[Trump] alitunga na kuamrisha kuandika kwa barua yote,” Harold Bornstein aliambia runinga ya CNN Jumanne.
    Ikulu ya White House haijazungumzia tuhuma hizo za daktari huyo.
    Bw Bornstein pia amesema maafisa wa serikali walitekeleza “uvamizi” katika afisi zake Februari 2017 na kuondoa nyaraka zote zilizohusiana na taarifa za kimatibabu za Bw Trump.

    Katika mahojiano na CNN, Bw Bornstein amesema barua hiyo ya mwaka 2015 iliyodokeza kwamba Bw Trump angekuwa “mtu mwenye afya bora zaidi aliyewahi kuchaguliwa kuwa rais” haikuwa utathmini wake wa kitaalamu wa hali yake ya afya.
    “Nilitayarisha nilipokuwa nasonga,” anasema.
    Haijabainika ni kwa nini Bw Bornstein anatoa tuhuma hizo kwa sasa.

    Barua hiyo ilisema nini?

    Barua hiyo ilikuwa na miongoni mwa mengine tamko kuhusu nguvu za kimwili za Bw Trump na ukakamavu wake, ambavyo vilielezwa kuwa “vya kipekee”.
    Vipimo kuhusu shinikizo la damu yake na pia uchunguzi mwingine wa maabara vilielezwa kuwa “vya kushangaza kwa uzuri wake” na kwamba alikuwa amepoteza uzani wa kilo 7 katika kipindi cha mwaka mmoja.
    Barua hiyo iliongeza kwamba Bw Trump hakuwa na aina yoyote ya saratani na hajawahi kufanyia upasuaji wowote wa maungo.

     

  • MATUKIO KWA PICHA, SHIKA NDINGA 103.3 MBEYA 2018

    MATUKIO KWA PICHA, SHIKA NDINGA 103.3 MBEYA 2018

    Mshindi wa chombo cha moto (Pikipiki) Shika Ndinga Mbeya Bw.SAIDI DAIMON KATEMBWE Mkazi wa Masewe, Mbeya mjini
    Bi.AMIDA HARUNI SELEMANI, akiwa katika hatua za mwisho kabla hajajishindia Chombo cha moto (pikipiki) kwa upande wa wanawake mkoa wa Mbeya. Shika Ndinga 2018.

  • SHIKA NDINGA MBEYA 2018

    SHIKA NDINGA MBEYA 2018

    Hatua za awali za ukaguzi wa uwanja ambao utatumika kubadilisha maisha ya wamiliki wa namba kubwa 103.3 Mbeya na kuwaongezea thamani kwa mtaji wa sikio tu.
    #ShikaNdinga2018Mbeya #TunapinduaMezaKibabe

  • TETESI ZA SOKA

    TETESI ZA SOKA

     

    Arsenal inaamini inaweza kumshawishi aliyekuwa mkufunzi wa Barcelona Luis Enrique kuchukua mahala pake Arsene Wenger kama meneja wake.
    Mkuu wa uhusiano katika klabu hiyo hiyo Rail Sanllehi alifanya kazi na Enrique katika klabu ya Barcelona.. (Mirror)
    Mkufunzi wa zamani wa Chelsea Carlo Ancelotti, ambaye ni mkufunzi mwengine anayepigiwa upatu kumrithi Wenger amepewa kazi ya kuifunza timu ya taifa ya Italy.

  • Ronaldo kumuwakilisha Messi Ligi ya mabingwa

    Ronaldo kumuwakilisha Messi Ligi ya mabingwa

     

    Cristiano Ronaldo

    Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya inaendelea tena usiku wa leo ambapo mabingwa wa Bundesliga, Bayern Munich watakuwa wanaikaribisha Real Madrid.

    Real Madrid tayari wameshatua mjini Bayern ambapo nguvu zao kubwa wameziweka kwenye mashindano hayo hivi sasa.

    Madrid haina nafasi tena katika taji la La Liga kutokana na ubora wa mpinzani wake, FC. Barcelona ambaye ameshajiwekea mazingira mazuri ya kutwaa Kombe hilo huku akitupwa nje ya UEFA Champions League na AS Roma.

    Nyota Cristiano Ronaldo anapewa nafasi ya kuendelea kucheka na nyavu kwenye mashindano haya ambapo mpaka sasa anaongoza kwa kuwa na mabao mengi.

    Ronaldo atakuwa anamuwakilisha Messi kutokana na ushiriki wa Madrid ambayo inacheza La Liga pia nchini Spain leo.

  • Kwa nini Saratani nyingine ni ‘hatari’

    Kwa nini Saratani nyingine ni ‘hatari’

    Utafiti umevumbua kwa nini baadhi ya maradhi ya saratani ni hatari kuliko aina nyingine ya saratani ingawa zinaonekana kufanana
    Taasisi ya wanasayansi ya Francis Crick ilianzisha uchambuzi wa historia ya saratani kwa ajili ya kutabiri mustakabali wake

    Utafiti kwa wagonjwa wa saratani ya figo unaonyesha kuwa baadhi ya uvimbe ”ni hatari” huku nyingine zikiwa hazina madhara na wakati mwingine hazihitaji matibabu
    Taasisi ya utafiti la Cancer Research ya Uingereza imesema utafiti huu unasaidia wagonjwa kupata uangalizi mzuri wa kitabibu
    hatuwezi kutofautisha kati ya unaohitaji tiba na usiohitaji.
    Mtu mmoja mwenye saratani anaweza kufa haraka kuliko mtu mwingine mwenye saratani inayofanana ambaye anaweza kuishi kwa miongo kadhaa baada ya matibabu
    Kazi iliyochapwa kwenye jarida liitwalo Journal Cell, iliainisha saratani za figo kwa wagonjwa 100
    Wakati saratani ikikua zinakuwa zikibadilika zaidi na hatimae sehemu mbalimbali za uvimbe zinajiunda kwa namna mbalimbali
    Watafiti huchukua sampuli kutoka sehemu mbalimbali za uvimbe huohuo na kutazama kwa namna gani zina uhusiano wa karibu

    Wanasayansi wanaeleza kivipi saratani nyingine ni hatari zaidiHaki miliki ya pichaCRICK INSTITUTE
    Image caption
    Wanasayansi wanaeleza kivipi saratani nyingine ni hatari zaidi
    Utafiti umevumbua kwa nini baadhi ya maradhi ya saratani ni hatari kuliko aina nyingine ya saratani ingawa zinaonekana kufanana
    Taasisi ya wanasayansi ya Francis Crick ilianzisha uchambuzi wa historia ya saratani kwa ajili ya kutabiri mustakabali wake
    Utafiti kwa wagonjwa wa saratani ya figo unaonyesha kuwa baadhi ya uvimbe ”ni hatari” huku nyingine zikiwa hazina madhara na wakati mwingine hazihitaji matibabu
    Taasisi ya utafiti la Cancer Research ya Uingereza imesema utafiti huu unasaidia wagonjwa kupata uangalizi mzuri wa kitabibu
    hatuwezi kutofautisha kati ya unaohitaji tiba na usiohitaji.
    Mtu mmoja mwenye saratani anaweza kufa haraka kuliko mtu mwingine mwenye saratani inayofanana ambaye anaweza kuishi kwa miongo kadhaa baada ya matibabu
    Kazi iliyochapwa kwenye jarida liitwalo Journal Cell, iliainisha saratani za figo kwa wagonjwa 100
    Wakati saratani ikikua zinakuwa zikibadilika zaidi na hatimae sehemu mbalimbali za uvimbe zinajiunda kwa namna mbalimbali
    Watafiti huchukua sampuli kutoka sehemu mbalimbali za uvimbe huohuo na kutazama kwa namna gani zina uhusiano wa karibu
    Familia ya Malley ilijitolea kufanya uchunguziHaki miliki ya pichaMICHAEL MALLEY
    Image caption
    Familia ya Malley ilijitolea kufanya uchunguzi


    Michael Malley, 72,kutoka London, alishiriki kufanyiwa vipimo hilo kwenye hospitali ya Royal Marsden baada ya kugundulikwa kuwa na saratani ya figo.
    Alisema: ”kwa kweli tafiti kama hizi ni muhimu kwa ajili ya kupata uelewa ni jinsi gani saratani ya figo inavyokua kadiri muda unavyokwenda, na nina matumaini kuwa hii itasaidia wagonjwa kama mimi kupata tiba nzuri.
    bado kuna changamoto ya namna nzuri ya kutibu kila aina ya uvimbe, pia namna ya kufanya uchunguzi kwenye hospitali badala ya maabara za utafiti

  • SHIKA NDINGA 2018 TANGA

    SHIKA NDINGA 2018 TANGA

    Kutoka kaskazini mwa Tanzania kwenye mji wenye mahaba tele tumekuja kuongeza thamani ya maisha kwa wakazi wa 88.9 #ShikaNdinga2018Tanga#TunapinduaMezaKibabe

    #Hatupoi Tukiwa nyumbani 88.9 Tanga waja leo wabaki milele.

    Huu ndio muonekano wa leo kwenye uwanja wa Lamore mahali ambapo akili nyingi itatumika na nguvu kiasi kuweza kuwachuja washiriki watakaokwenda kushika ndinga jukwaani.
    #ShikaNdinga2018Tanga#TunapinduaMezaKibabe

    Tukiwa karibu nawe kwa namba 88.9 Tanga ndugu zetu wa @ttcl_corporation wanatupa uthubutu zaidi na habari njema ni kwamba *150*71# ndio namba yako ya kipesa kukuwezesha kununua umeme ili uendelee kusikiliza E-fm na kutazama @tvetanzania
    #RudiNyumbaniKumenoga

  • SHIKA NDINGA; 88.9 TANGA HODI HAPOOOH.

    SHIKA NDINGA; 88.9 TANGA HODI HAPOOOH.

    Timu ya wafanyakazi wa Efm na Tv E ilipo wasili katika uwanja wa Ramore Tanga kwaajili ya shindano la SHIKA NDINGA litakalofanyika kesho April 14 2018.
    Picha ya pamoja wafanyakazi wa Efm & Tv E na TTCL Mara baada ya kuwasili katika mkoa wa Tanga na kufanya ziara fupi kwenye ofisi za TTCL mkoani hapa.
  • Mpambe wa Rais Magufuli aombwa apangiwe kazi nyingine

    Mpambe wa Rais Magufuli aombwa apangiwe kazi nyingine

    Mkuu wa Majeshi ya Tanzania, Venance Mobeyo, amemuomba Rais Magufuli aridhie mpambe wa Rais wake, Kanali MN Nkelemi kupangiwa kazi nyingine baada ya kupandishwa cheo kutoka Kanali, kuwa Brigedia Jenerali.

     

    Hata hivyo amesema kuwa “Pamoja na upandishwaji vyeo huo nimeomba pia aridhie na amekubali kupandishwa cheo Luteni Kanali DPM Mulunga kuwa Kanali na kwa cheo hicho Mh. Rais ameridhia vilevile ateuliwe kuwa mpambe wa Rais kuanzia leo taratibu zingine za kuwavisha vyeo hivyo zitafanyika kesho Makao Makuu ya Jeshi ,” amesema Mobeyo.