NIGERIA KUUZA NDEGE ZA RAIS KUPUNGUZA UBADHIRIFU
Slider

Nigeria imetangaza kwamba itauza ndege mbili zinazotumiwa na rais wa nchi hiyo kama njia ya kupunguza matumizi mabaya ya pesa za umma. Msemaji wa Rais Muhammadu Buhari, Garba Shehu, amesema ndege hizo mbili kati ya 10 zinazotumiwa na rais wa nchi hiyo zitauzwa kama sehemu ya kupunguza ‘ubadhirifu’ wa serikalini. Serikali imeweka tangazo magazetini kwamba inauza ndege hizo, moja aina ya Falcon 7X na nyingine Hawker 4000. Bw Shehu amesema Rais Buhari ndiye aliyeidhinisha matangazo hayo. Ameongeza kwamba baadhi ya...

Like
143
0
Wednesday, 05 October 2016
DUTERTE ASEMA OBAMA ANAWEZA ‘KWEND JEHANAMU’
Slider

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amerejelea tena shutuma zake dhidi ya Rais Obama na viongozi wengine wa nchi za Magharibi wanaopinga mpango wake wa kupambana na walanguzi wa dawa za kulevya. Kiongozi huyo amesema Bw Obama anaweza “kwenda jehanamu”. Umoja wa Ulaya, ambao pia umemkosoa Bw Duterte, unaweza “kuchagua kwenda eneo la kutakasia dhambi ndogo, kwa sababu jehanamu kumejaa”, amesema. Watu karibu 3,000 wameuawa tangu kiongozi huyo alipoingia madarakani mwezi Juni. Watu wanaoshukiwa kulangua mihadarati au kuwa...

Like
220
0
Wednesday, 05 October 2016
WACHINA WAZINDUA VYOO VILIVYOJENGWA KWA VIOO
Slider

China imezidisha matumizi yake ya vioo kuunda vivutio vya kitalii kwa kujenga choo cha vioo ambacho mtu anaweza akaona nje na hata ndani. Vyoo hivyo, vimejengwa karibu na Ziwa Shiyan, katika mkoa wa Hunan kusini mwa nchi hiyo. Vioo hivyo vinawezesha wanaovitumia vyoo hivyo kutazama mandhari ya kuvutia ya msitu au wengine wanaotumia vyoo jirani. Kuta za vyoo hivyo, hata zile zinazotenganisha vyoo vya wanawake na wanaume, ni za vioo kabisa ingawa vioo hivyo vimetiwa ukungu kiasi. Vyombo vya habari...

Like
240
0
Monday, 03 October 2016
UCHAGUZI DRC WAAHIRISHWA KWA MIAKA MIWILI
Slider

aarifa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zinasema kuwa tume huru ya Uchaguzi nchini humo, imetangaza kuwa uchaguzi mkuu sasa utaandaliwa Novemba mwaka wa 2018 na wala sio mwaka huu kama ilivyotarajiwa. Viongozi kadha wa upinzani walioshiriki katika mazungumzo ya amani ya kitaifa wameafikiana na uamuzi huo, lakini kuna wale wanaoupinga wakisema ni njama ya Rais Joseph kabila kusalia...

Like
209
0
Monday, 03 October 2016
UTAFITI: WATOTO WASIOWEZA KUUGUA UKIMWI
Slider

Uchunguzi uliofanywa na wanasayansi wa chuo cha Oxford umeonysha kuwa asilimia 10 ya watoto walioambukizwa virusi vya HIV hawapati ugonjwa wa Ukimwi licha ya kutopata matibabu. Utafiti uliofanyiwa watoto 170 walio na virusi vya HIV nchini Sudan Kusini ulionyesha kuwa kinga yao ya mwili ililingana na ya nyani waliokuwa na virusi hivyo. Wataalamu wanasema kuwa ugunduzi huo ni ishara ya kwanza ya watu wanoishi na virusi vya HIV, ambao utasababisha kupatikana na tiba kwa wagonjwa wote walio na virusi hivyo....

Like
190
0
Thursday, 29 September 2016
ZIMBABWE KUTOA SARAFU YA DOLA
Slider

Mahakama ya juu zaidi nchini Zimbabwe imetupilia mbali kesi iliyowasilishwa na upinzani ya kupinga kutolewa sarafu mpya ya noti sawa na sarafu ya dola ya marekani, wakati nchi hiyo inapokabiliwa na hali mbaya ya uchumi tangu iache kutumia sarafu yake mwaka 2009. Mahakama ya katiba ilitoa uamuzi kuwa kesi iliyowasilishwa na kiongozi wa chama cha Zimbabwe People First ,Joice Mujuru ukiitaja kuwa uvumi. “Mnadai kuwa noti hizo zitatolewa kinyume cha sheria lakini serikali imesema kuwa itafanya hivyo kuambatana na sheria,...

Like
241
0
Thursday, 29 September 2016
HOMA YA PAMBANO LA SIMBA NA YANGA YAPAMBA MOTO
Slider

“Natayarisha Supu ya Mawe”, kauli ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hans Pope kuelekea mchezo utakawakutanisha watani wa jadi Simba na Yanga. Timu zote mbili zipo kambini kwa sasa kujiandaa na mchezo huo unasubiri kwa hamu kubwa na wapenzi wa soka huku ukitajwa kuwa na mvuto wa kipekee, Simba imeweka kambi Morogoro, huku Yanga wakiweka kambi...

Like
340
0
Wednesday, 28 September 2016
YANGA YAKATA RUFAA KUPINGA STAND UNITED KUMTUMIA MCHEZAJI FRANK IGOBELA
Slider

Yanga yapeleka barua TFF ikiwa na lengo la kukata rufaa kupinga klabu ya Stand United kumtumia mchezaji Frank Igobela kwenye mchezo wa ligi kuu uliomalizika kwa Yanga kupokea kichapo cha 1-0 kutoka Stand United, katika barua hiyo Yanga imeeleza kuwa Frank Igobela ni mchezaji halali wa Polisi ya...

Like
364
0
Wednesday, 28 September 2016
MAPYA KUHUSU KUVUNJIKA KWA NDOA YA BRAD PITT NA ANGELINA JOLIE
Slider

Mwigizaji maarufu kutoka Marekani Brad Pitt amesikitishwa na mkewe Angelina Jolie kudai talaka na kusema watoto wasihusishwe na suala hilo. Pitt amesema amegadhabishwa na suala hilo lakini amesema kitu muhimu kwa hivi sasa ni maslahi ya watoto wake, kwa mujibu wa gazeti la Marekani la People. Jolie mwenye umri wa miaka 41 aliwasilisha ombi la kutaka talaka kutoka kwa Pitt mwenye umri wa miaka 52, kutokana na “sababu zisizoepukika” siku ya Jumatatu Wakili wa Jolie, Robert Offer, alisema Jolie alichukua...

Like
304
0
Thursday, 22 September 2016
RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA UDHAMINI YA MFUKO WA PENSHENI WA LAPF:
Slider

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli, leo tarehe 21 Septemba, 2016 ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF Profesa Hasa Mlawa. Taarifa iliyotolewa na Ikulu leo inasema pamoja kutengua uteuzi wa Profesa Mlawa, Rais Magufuli amevunja Bodi ya Udhamini ya Mfuko huo. Uteuzi wa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Udhamini ya LAPF utafanywa...

Like
193
0
Wednesday, 21 September 2016
TRUMP AKEREKA MSHUKIWA WA NEW YORK KUTIBIWA NA KUPEWA WAKILI
Slider

Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amelalamikia hali kwamba mshukiwa anayedaiwa kutekeleza shambulio New York Ahmad Khan Rahami alitibiwa baada ya kujeruhiwa wakati wa ufyatulianaji risasi na maafisa wa polisi Jumatatu. Aidha, amekerwa na hali kwamba mshukiwa huyo bado atapewa wakili na serikali. Mshukiwa huyo mzaliwa wa Afghanistan mwenye umri wa miaka 28 amefunguliwa mashtaka matano ya kujaribu kutekeleza mauaji. Bw Trump akihutubu Fort Myers, Florida amesema hiyo si “hali nzuri” na inaashiria...

Like
194
0
Tuesday, 20 September 2016
« Previous PageNext Page »