TANZANIA YAONGOZA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA KIFEDHA KUPITIA MITANDAO YA SIMU
Slider

TANZANIA imetajwa kuwa nchi ya kwanza duniani kufanikiwa katika utoaji wa huduma za kifedha kwa kutumia mitandao ya simu. Hayo yamebainishwa Jana Jijini Dar es salaam na Kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasiliano nchini–TCRA, Mhandisi James Kilaba katika mkutano wa kimataifa wa wadau wa mawasilino ulioandaliwa na shirika la kimataifa la mawasilino -ITU kwa kushirikiana na TCRA pamoja na benki kuu ya tanzania, ambao umeshirikisha washiriki 156 kutoka nchi mbalimbali duniani, lengo likiwa ni kuhakikisha huduma za fedha kupitia...

Like
257
0
Tuesday, 20 September 2016
MCHUNGAJI AKATISHA HOTUBA YA TRUMP
Slider

Mchungaji wa kanisa moja la watu weusi katika jimbo la Michigan, Marekani amemkatisha Donald Trump akihutubu alipoanza kumshutumu mpinzani wake Hillary Clinton. Mchungaji Faith Green Timmons alimkatisha BwTrump alipomshutumu mgombea huyo wa chama cha Democratic kuhusu mikataba ya kibiashara duniani. “Bw Trump, nilikualika hapa uje kutushukuru kwa juhudi ambazo tumefanya Flint, si kutoa hotuba ya kisiasa,” amesema pasta huyo wa kanisa la Bethel United Methodist. “Aha, hilo ni jambo njema,” amemjibu mgombea huyo wa chama...

Like
291
0
Thursday, 15 September 2016
MSN NI MVUA YA MAGOLI, YAISAMBARATISHA CELTIC 7-0
Slider

Celtic walipokezwa kichapo kibaya zaidi katika mashindano ya Ulaya Jumanne usiku baada ya kuchapwa mabao 7-0 na Barcelona uwanjani Camp Nou. Mshambuliaji Lionel Messi, raia wa Argentina, alifunga ‘hat-trick’ yake ya sita katika mechi hiyo ya kundi C. Alianza kwa kufunga bao la mapema. Mchezaji wa Celtic Moussa Dembele alishindwa kufunga penalti kabla ya Messi kufunga la pili. Kipindi cha pili, Neymar alifunga kupitia frikiki, Andres Iniesta akafunga la nne, Messi akaongeza la tano naye Suarez akakamilisha ushindi kwa mabao...

Like
291
0
Wednesday, 14 September 2016
HILLARY CLINTON KUENDELEA NA KAMPENI
Slider

Mgombea urais wa chama cha Democratic nchini Marekani Hillary Clinton atarejelea kampeni zake mnamo Alhamisi, msemaji wake amesema. Mwanasiasa huyo alikuwa amepumzika kwa siku kadha ili kupata nafuu baada ya kuugua kichomi. Bi Clinton alizidiwa na nusura azirai alipokuwa anahudhuria hafla ya kuadhimisha miaka 15 tangu kutekelezwa kwa shambulio la kigaidi la 9/11 ambapo watu karibu 3,000 waliuawa. Aligunduliwa kuwa anaugua kichomi, ugonjwa wa mapafu ambao pia hujulikana kama nimonia, siku ya Ijumaa. Kumezuka mjadala mkali kuhusu afya yake...

Like
193
0
Wednesday, 14 September 2016
MAHAKIMU 11 KIBARUA CHAOTA NYASI
Slider

Dar es Salaam. Wakati mahakimu 11 na watumishi 23 wa mahakama wakifukuzwa kutokana na kukiuka maadili ya utumishi, wengine 62 watajadiliwa na vyombo vya kimahakama kuangalia hatima yao. Akizungumza baada ya kupokea ripoti ya miezi minane ya utendaji wa mahakama Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman amesema mahakimu 32 walioshinda kesi za jinai katika mahakama mbalimbali nchini, watapelekwa kwenye Kamati ya Maadili ya Mahakama kwa ajili ya kufunguliwa mashauri ya kinidhamu. Amesema mahakimu wengine 30 walioshinda kesi za rushwa katika mahakama...

Like
199
0
Thursday, 08 September 2016
CHINA KUFUNGA DARAJA LA VIOO BAADA YA WIKI MBILI
Slider

Daraja la vioo lililojengwa juu nchini Uchina ililosifiwa kwa kuvunja rekodi lilipozinduliwa siku 13 tu zilizopita limefungwa. maafisa wanasema serikali inapanga kufanya ukarabati wa dharura wa eneo hilo na hivyo kufunga daraja hilo Ijumaa, ambapo tarehe ya kufunguliwa tena itatangazwa Lakini Kituo cha televisheni cha Marekani CNN kimesema kuwa msemaji amewaambia kuwa daaja hilo linaloelea juu “limekuwa likitembelewa na wageni wengi kupita uwezo wake “. Amesema kuwa hakuna ajali iliyowahi kutokea na daraja halikuwa na ufa wala...

Like
484
0
Monday, 05 September 2016
GABON: VURUGU ZATANDA BAADA YA ALI BONGO KUTANGAZWA MSHINDI
Slider

Fujo zimezuka katika mji mkuu wa Gabon, Libreville baada ya Rais Ali Bongo kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumamosi. Mgombea wa upinzani Jean Ping amesema watu wawili wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya vikosi vya usalama kuvamia makao makuu ya chama chake. Serikali imesema inawaandama “wahalifu wenye silaha” ambao awali walikuwa wameteketeza majengo ya bunge. Bw Ping amepinga matokeo ya urais ambayo yalionyesha Rais Bongo alishinda uchaguzi kwa kura chache. Hii inampa fursa ya kuongoza taifa hilo...

Like
358
0
Thursday, 01 September 2016
ARSENAL KUMTOA JACK WILSHERE KWA MKOPO
Slider

Arsenal iko tayari kumtoa kwa mkopo kiungo wa kati wa Uingereza Jack Wilshere ili kupata fursa ya kujumuika katika kikosi cha kwanza cha timu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24,ambaye mchezo wake uliathirika kutokana na jeraha la mguu aliichezea Arsenal mara tatu pekee msimu uliopita baada ya kupata jeraha hilo. Aliichezea Uingereza mara sita pekee msimu ulioipita ,ikiwemo mechi tatu katika mashindano ya Euro2016, lakini hakuchaguliwa katika kikosi cha kwanza cha mkufunzi Sam Allardyce wiki hii. Arsenal ililipa pauni...

Like
200
0
Tuesday, 30 August 2016
WHATSAPP KUSHEA DATA NA FACEBOOK
Slider

Kamishna wa mawasiliano nchini Uingereza anachunguza uamuzi wa programu ya WhatsApp wa kugawana data na kampuni ya facebook. Data hiyo ya watumiaji wa WhatsApp itatumiwa kuvutia matangazo yanayoonekana na watumiaji wa mtandao wa facebook. Itagawana nambari za simu na maelezo ya mara ya mwisho mteja kuingia katika akaunti yake ya WhatsApp na facebook. Kamishna huyo amesema kuwa kwa kuwa mabadiliko hayo yataathiri watu wengi ,anataka maelezo zaidi kuhusu kile kitakachogawanywa kati ya huduma hizo mbili. Kamishna Elizabeth Denham amesema kuwa...

Like
406
0
Monday, 29 August 2016
MATUNDA NA MBOGA HUPUNGUZA HATARI YA UGONJWA WA MOYO
Slider

Utafiti mpya uliofanywa nchini Italy unasema kuwa chakula kinachotumiwa katika eneo la Mediterranean kinapunguza hatari ya vifo vya mapema miongoni mwa watu walio na ugonjwa wa moyo. Utafiti huo umebaini kwamba watu wanaotumia matunda,mboga,samaki na njugu hupunguza hatari ya kufariki ikilinganishwa na wale wanaokula nyama nyekundu na siagi. Mmiliki wa ripoti hiyo amesema kuwa mpango huo wa chakula unaweza kuwasaidia sana wagonjwa wa moyo ikilinganishwa na dawa zinazopunguza kiwango cha mafuta mwilini. Tafiti za awali kuhusu umuhimu wa chakula...

Like
280
0
Monday, 29 August 2016
MAHAKAMA YA UFARANSA YAAHIRISHA MARUFUKU YA UVAAJI WA BURKINI
Slider

Mahakama ya juu ya utawala nchini Ufaransa imeahirisha marufuku iliyowekwa na miji ya mwambao juu ya uvaaji wa vazi la kuogelea linalofunika mwili mzima ama burkini linalovaliwa na wanawake wa kiislam. Mahakama hiyo imeahirisha marufuku hiyo katika moja wapo ya miji hiyo wa – Villeneuve-Loubet – lakini kuna uwezekano mkubwa kwamba karibu miji thelethi iliyoweka amri hiyo pamoja na maeneo mengine ya miji ya mwambao wakaondoa marufuku hiyo. Kesi hiyo iliwasilishwa na wanaharakati ambao walisema hatua ya kupiga marufuku burkini...

Like
220
0
Friday, 26 August 2016
« Previous PageNext Page »