GWIJI wa Soka la Kimataifa wa Liberia George Weah ametangaza rasmi kuwa atawania nafasi ya urais wa nchi hiyo kwa mara ya pili. Weah, ambaye aliwahi kuchezea klabu za PSG, AC Milan, Chelsea, na Monaco amebainisha kwamba amekuwa na malengo ya kuliletea Taifa hilo mabadiliko, tangu alipoanza kujihusisha na masuala ya kisiasa mara tu baada ya kurejea Liberia mwaka 2003. Rais wa Sasa Johnson Sirleaf anamaliza awamu yake ya pili na ya mwisho katika utawala wake mwaka 2017 ambapo kwa mujibu...
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imetakiwa kurekebisha mtaala wa kutoa mafunzo ya ukunga ili kuifanya taaluma hiyo iweze kuheshimika na kunusuru maisha ya watoto na akina mama wakati wa kujifungua. Wito huo umetolewa na Katibu mkuu wa Chama cha Wakunga Tanzania-TAMA-Dokta. Sebalda Leshabari alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari katika Semina maalumu iliyofanyika Jijini Dar es salaam ambapo amesema Wizara hiyo inatakiwa kuangalia namana ya kurekebisha mitaala ya utoaji wa mafunzo ya ukunga...
MJUMBE wa Umoja wa Mataifa nchini Syria Staffan de Mistura amezitaka Urusi na Marekani kuimarisha usitishaji tete wa mapigano nchini Syria kabla ya mazungumzo ya amani yenye lengo la kumaliza miaka 5 ya mzozo nchini humo. Kauli hiyo ya de Mistura inakuja muda mfupi baada ya kulifahamisha baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya mazungumzo ya amani, ambayo amesema yamepiga hatua licha ya vikwazo vya hivi ...
MAMIA ya watu wamekusanyika nje ya uwanja wa ndege wa Kinshasa kuupokea mwili wa mwanamuziki Papa Wemba uliowasili nchini humo kutoka Abidjan. Mwanamuziki huyo ambaye ametajwa kuwa mmoja ya waanzilishi wa muziki wa kizazi kipya cha Soukous anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne baada ya mwili huo kuwekwa katika uwanja wa mpira kwa raia kutoa heshima zao za mwisho. Maafisa wa serikali na wanadiplomasia watahudhuria ibada ya kumkumbuka mwanamuziki huyo katika uwanja wa ndege kabla ya mwili huo kupelekwa katika chumba cha...
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam Mh. Ally Hapi leo amewatembelea wananchi maeneo ya Bunju na Mbweni waliokuwa na kero mbalimbali. Katika eneo la Bunju Kilungule, baadhi ya wananchi nyumba zao zimezungukwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Akijibu maombi ya wananchi hao, Mheshimiwa, Hapi amewaagiza mainjinia wa manispaa kuhakikisha kuwa wanafanya utaratibu wa kupata pampu kubwa ya kuvuta maji hayo, huku akiwataka wananchi kuwa wale wote waliojenga katika eneo hatarishi ambalo ramani inaonesha kuwa ni eneo...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC, Bi Juliet Kairuki. Kwa mujibu wa Taarifa kwa vyombo vya Habari iliyotolewa leo na kusainiwa na Katibu Mkuu, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda, Uteuzi wa Bi Kairuki umetenguliwa kuanzia April 24 mwaka huu. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, hatua hiyo imechukuliwa na Mheshimiwa Rais baada ya kupata taarifa kwamba Mkurugenzi huyo amekuwa hachukui mshahara wa Serikali tangu alipoajiriwa mwezi April...
MGOMO wa wafanyakazi wa sekta ya umma umevuruga shughuli za kawaida nchini Ujerumani hii leo. Wanachama wa chama cha wafanyakazi wa sekta ya umma Verdi wamegoma kufanya kazi kutokana na madai ya nyongeza ya mshahara. Viwanja vya ndege vya Frankfurt, Dusseldorf na Munich vimeathirika na mgomo huo ikiwa ni pamoja na usafiri wa mjini katika miji mbali mbali, lakini uwanja wa ndege wa mjini Berlin unafanyakazi kama ...
SALAH ABDESLAM , anayetuhumiwa kuchukua nafasi ya juu katika mashambulizi ya mjini Paris ambayo yamesababisha watu 130 kuuwawa, anafikishwa mahakamani nchini Ufaransa leo, kwa mtazamo wa kuwekwa chini ya uchunguzi rasmi. Hatua hiyo inakuja baada ya Abdeslam kupelekwa nchini Ufaransa kutoka Ubelgiji mapema leo Jumatano. Mtuhumiwa huyo aliwasili nchini Ufaransa mapema leo...
IMEBAINISHWA kuwa kwa mwaka 2012/2015 kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom imechangia zaidi ya shilingi bilioni 3 katika pato la taifa ambayo ni sawa na asilimia 2 ya pato la Tanzania. Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam katika tathmini iliyofanywa na KPMG juu ya mchango mpana wa kiuchumi na kijamii ikiwamo ukuzaji wa uchumi,ajira,na kupunguza umaskini,tathmini iliyofanyika kuhusu mtaji na shughuli za uwekezaji kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2012/...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli, amewaapisha Maafisa Tawala wapya kumi aliowateua April 25, mwaka huu na kuwapangia vituo vyao vya kazi. Makatibu Tawala hao wapya, wameapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam na kuweka saini ya ahadi ya uadilifu kwa Viongozi wa Umma, Zoezi lililoendeshwa na kamishna wa maadili Sekretarieti ya maadili ya Viongozi wa Umma, Mheshimiwa Jaji Salome Kaganda mbele ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John...
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Alfred Lucas kuwa Afisa Habari na Mawasiliano mpya wa shirikisho kuanzaia leo Aprili 27, 2016. Alfred anachukua nafasi ya Baraka Kizuguto aliyehamishiwa katika Kurugenzi ya Mashindano kuwa Afisa Mashindano na Meneja wa Mifumo pepe ya Usajili (TMS). Alfred ana uzoefu kutoka vyombo mbalimbali alivyovitumikia kama mwandishi wa habari na mhariri.Kadhalika Alfred kitaaluma amesomea uandishi wa habari, uhusiano wa kimataifa na diplomasia pamoja na...