RAIS MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA CAG
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa dokta John pombe Magufuli, jana amepokea taarifa ya ukaguzi wa hesabu za serikali kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu Jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu Rais Magufuli amepokea taarifa hiyo yenye ripoti tano, ikiwa ni utaratibu wa kikatiba unaomtaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kukabidhi kwa Rais taarifa ya ukaguzi kabla ya mwisho wa mwezi Machi....

Like
224
0
Tuesday, 29 March 2016
MCHINA AKIRI KUIBA SIRI ZA MAREKANI
Global News

MWANAMUME mmoja kutoka Uchina amekiri kuhusika katika njama ya kuiba siri kuu kuhusu mifumo ya kijeshi ya Marekani. Su Bin anaaminika kuwa kwenye kundi la watu ambao wamekuwa wakiiba habari kuhusu ndege za kivita, ndege za kubeba mizigo na silaha. Bw Su, mwenye umri wa miaka 50, alikiri kufanya kazi na watu wawili kutoka Uchina kati ya Oktoba 2008 na Machi 2014 kudukua mifumo ya kompyuta ya Marekani, ikiwemo kampuni ya Boeing inayotumiwa na jeshi la Marekani kuunda ndege...

Like
279
0
Thursday, 24 March 2016
MSHUKIWA WA BRUSSELS ALIUNDA MABOMU YA PARIS
Global News

MAAFISA wa Ufaransa na Ubelgiji wanasema mmoja wa walipuaji wa kujitoa mhanga waliotekeleza mashambulio ya Brussels alikuwa mtaalamu wa kutengeneza mabomu. Wamesema mshukiwa huyo alihusika katika kuunda mabomu yaliyotumiwa kutekeleza mashambulio ya Paris Novemba mwaka jana na kusababisha vifo vya watu 130.   Wakizungumza, bila kutaka kunukuliwa, maafisa hao walisema chembe nasaba za DNA za mshukiwa huyo Najim Laachraoui zilipatikana katika mikanda ya kujilipua iliyotumiwa...

Like
238
0
Thursday, 24 March 2016
MIONGOZO RAHISI YA USIMAMIZI WA MISITU YAZINDULIWA
Local News

MRADI wa MAMA MISITU kwa kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali wamezindua miongozo rahisi ya usimamizi shirikishi wa misitu kwa jamii, vijiji na kwa pamoja. Akizungumza na waandishi wa Habari katika uzinduzi huo, Meneja Mradi wa MAMA MISITU Gwamaka Mwakyanjala amesema kuwa lengo la uzinduzi wa Miongozo hiyo ni kuwawezesha wananchi kufahamu zaidi ni nini wanapaswa kufanya katika utunzaji wa misitu ili wafaidike na malighafi zinazotokana na...

Like
228
0
Thursday, 24 March 2016
SHEIN AAPISHWA ZANZIBAR LEO
Local News

RAIS Mteule wa Zanzibar, Dokta Ali Mohammed Shein anaapishwa leo kwenye Uwanja wa Aman mjini Zanzibar. Kuapishwa kwa Dk Shein kunamfanya apate nafasi nyingine ya kuongoza Zanzibar kwa muda wa miaka mitano ijayo, baada ya mgombea huyo wa CCM kushinda urais wa Jumapili kwa kujinyakulia asilimia 91 ya kura zilizopigwa. Serikali pia imetangaza kuwa leo pia ni siku ya mapumziko visiwani humo ili kuwapa nafasi wananchi wahudhurie sherehe za kuapishwa kwa kiongozi wao. Wageni ambao wanatarajia kuhudhuria kwenye sherehe hizo...

Like
254
0
Thursday, 24 March 2016
TED CRUZ AMBWAGA DONALD TRUMP KWENYE JIMBO LA UTAH
Global News

LICHA ya kuongoza kwa mbali kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tiketi ya kuteuliwa kuwa mgombea urais wa Marekani kwa chama cha Republican, bilionea Donald Trump ameangushwa na hasimu wake Ted Cruz kwenye kura za mchujo za jimbo la Utah.   Wakati zaidi ya nusu ya kura zikiwa zimeshahesabiwa, Seneta Cruz anaongoza kwa takribani asilimia 70, huku Gavana John Kasich wa Ohio na Trump wakiwa nyuma yake.   Wiki iliyopita, Gavana Kasich alimshinda pia Trump kwenye uchaguzi wa...

Like
232
0
Wednesday, 23 March 2016
KONGO: DENIS SASSOU AATANGAZWA KUWA MSHINDI WA UCHAGUZI
Global News

KIONGOZI wa muda mrefu nchini Kongo, Denis Sassou Nguesso, ametangazwa na Tume ya Uchaguzi nchini humo kushinda tena urais, na hivyo kumpa nafasi ya kuendeleza utawala wake wa zaidi ya miongo mitatu sasa.   Huku matokeo ya mji mkuu wa kiuchumi na ngome ya upinzani, Pointe-Noire, yakiwa hayajajumuishwa, mkuu wa tume ya uchaguzi, Henri Bouka, amesema Nguesso tayari ana asilimia 67 ya kura.   Mwanajeshi huyo wa zamani wa kikosi cha miamvuli kwenye jeshi la Ufaransa na mwenye umri wa...

Like
198
0
Wednesday, 23 March 2016
WANANCHI NA MADEREVA WA DALADALA WAMEIOMBA SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU KATIKA VITUO VYA MAWASILIANO NA MAKUMBUSHO
Local News

WANANCHI na madereva katika vituo vya daladala vya Makumbusho na Mawasiliano, wameiomba serikali kutengeneza barabara ziingiazo katika vituo hivyo kwani ni mbovu na zinasababisha uharibifu wa magari. Wakizungumza na efm baadhi ya madereva hao wamesema kuwa barabara hizo ni finyu na mbovu hususani zinazoingia katika kituo cha makumbusho ambazo pamoja na Serikali kumwaga vifusi lakini kwa mvua iliyonyesha leo imekuwa ni kero ya tope kwa waenda kwa...

Like
273
0
Wednesday, 23 March 2016
JAMII IMETAKIWA KUEPUKA UHARIBIFU WA MAZINGIRA
Local News

KATIKA kupambana na athari za mabadiliko ya Tabia nchi ikiwemo ongezeko kubwa la Joto Duniani, Mamlaka ya hali ya hewa kwa kushirikiana na Wakala wa misitu Nchini, wameitaka jamii kuepuka uharibifu wa mazingira na kuongeza kasi ya upandaji miti .   Hayo yamebainishwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa Nchini Dokta Agness Kijazi alipozungumza na Waandishi wa habari katika maadhimisho ya Siku ya hali ya hewa Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 23mwezi wa tatu Duniani...

Like
217
0
Wednesday, 23 March 2016
FBI HUENDA WAKAFUNGUA SIMU YA MUUAJI
Global News

IDARA ya Haki ya Marekani imesema huenda shirika la upelelezi la FBI limegundua njia ya kufungua simu ya mkononi ya muuaji Syed Rizwan Farook aliyewapiga risasi watu eneo la San Bernardino. Idara hiyo imeiomba mahakama kuahirisha kusikilizwa kwa kesi kati ya shirika hilo dhidi ya kampuni ya utengenezaji wa simu, Apple.ya iPhone Idara hiyo imekuwa ikiishawishi mahakama ilazimishe Apple kufungua simu ya Farook, ambaye yeye na mkewe wanatuhumiwa kufanya shambulizi la bunduki na kuwaua zaidi ya watu 14 katika jimbo...

Like
205
0
Tuesday, 22 March 2016
PROFESA MUHONGO: MILANGO YA UWEKEZAJI IKO WAZI KWA MATAIFA YOTE KUWEKEZA TANZANIA
Local News

WAZIRI wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa milango ya uwekezaji iko wazi kwa Mataifa yote duniani yenye nia thabiti ya kufanya hivyo nchini Tanzania.   Profesa Muhongo ameyasema hayo jijini Dar Es Salaam wakati wa kikao chake na Balozi wa Afrika Kusini nchini,Thami Mseleku ambaye alifika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini kufahamu zaidi nafasi za uwekezaji kwa ajili ya manufaa ya Kampuni za uwekezaji za Afrika Kusini.   Katika kikao hicho, Profesa Muhongo amemueleza Balozi...

Like
261
0
Tuesday, 22 March 2016
« Previous PageNext Page »