SERIKALI YAOMBWA KUFANYA UKAGUZI WA MAENEO YALIYOTENGWA KWA AJILI YA SHUGHULI ZA KIJAMII
Local News

SERIKALI imeombwa kufuatilia na kukagua maeneo yaliyotolewa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo shule, hospitali na zahanati ili kuwaletea maendeleo wananchi. Rai hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Diwani wa kata ya Buguruni Adam Fugame alipokuwa akizungumza na wanahabari kwa lengo la kumuomba mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik kuukabidhi uongozi wa kata kiwanja alichowahi kukikabidhi mwaka 2011 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ambacho kimekodishwa kwa kampuni ya Yasser General...

Like
185
0
Wednesday, 17 February 2016
MWANZA: WANANCHI WATAHADHARISHWA JUU YA WEZI WANAOTUMIA BODABODA
Local News

MWENYEKITI wa chama cha waendesha pikipiki Mkoa wa Mwanza, Makoye Kayanda, amewatahadharisha wakazi wa jiji hilo kuwa makini wawapo barabarani ili kuepukana na vitendo vya ukwapuaji  mikoba na mabegi vinavyofanywa na baadhi ya wahalifu kwakutumia pikipiki maarufu Boda boda. Kayanda ametoa tahadhari hiyo jijini Mwanza baada ya kupokea malalamiko ya kukithiri kwa vitendo hivyo vinavyofanywa na baadhi ya watu wanaojifanya waendesha pikipiki  jambo linalochafua taswira ya waendesha pikipiki wa...

Like
257
0
Wednesday, 17 February 2016
UTURUKI YAENDELEZA MASHAMBULIZI DHIDI YA WAKURDI SYRIA
Global News

UTURUKI imeendelea kuyashambulia maeneo ya Wakurdi nchini Syria kwa siku ya pili, licha ya kuongezeka shinikizo la kimataifa kuitaka nchi hiyo isitishe mashambulizi yake kwenye eneo la mpakani. Uturuki inataka wapiganaji wa Kikurdi waondoke kwenye eneo hilo la mpaka. Akizungumza kwa njia ya simu na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, Waziri Mkuu wa Uturuki, Ahmet Davutoglu amesema vikosi vya usalama vya nchi yake havitowaruhusu Wakurdi wafanye vitendo vya uchokozi. Syria imeyalaani mashambulizi ya Uturuki, huku ikiutolea wito Umoja wa Mataifa...

Like
185
0
Monday, 15 February 2016
WANADIPLOMASIA KUANDAA RIPOTI YA USALAMA ISRAEL NA PALESTINA
Global News

WANADIPLOMASIA wa mataifa manne wapatanishi katika amani ya Mashariki ya Kati wamesema wataandaa ripoti kuhusu hali ya sasa ya usalama kati ya Israel na Palestina huku wakiangazia zaidi kuanza tena kwa mazungumzo ya amani. Baada ya kukutana mjini Munich, Marekani, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na Urusi, zimesema ripoti hiyo itajumuisha mapendekezo ambayo yanaweza kusaidia kuyajulisha mazungumzo ya kimataifa kuhusu njia bora ya kupatikana kwa suluhisho la mataifa hayo...

Like
158
0
Monday, 15 February 2016
TEMEKE: WANANCHI WATAKIWA KUFICHUA WAUZAJI WA DAWA ZA KULEVYA
Local News

JESHI la Polisi mkoa wa Kipolisi Temeke limewaomba wakazi wa maeneo hayo kutoa taarifa juu ya watu wanaohusika na uuzaji wa dawa za kulevya kwakuwa kimekuwa ni chanzo cha vijana kushindwa kujishughulisha. Akizungumza na EFM Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Temeke  Andrew Satta amesema kuwa kutokana na oparesheni inayoendelea ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya, jeshi hilo limegundua wauzaji wakubwa wa dawa hizo kukimbia na kwenda kujificha katika maeneo ya nje ya mkoa huo wa...

Like
257
0
Monday, 15 February 2016
WAKURUGENZI WANNE MSD WASIMAMISHWA KAZI KWA TUHUMA ZA UBADHIRIFU WA FEDHA
Local News

WAZIRI wa afya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu amewasimamisha kazi wakurugenzi wanne kutoka Bohari ya Dawa ya Taifa-MSD- kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha takribani shilingi Bilioni 1.5.   Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam leo katika kitengo cha Afya ya mama na mtoto baada ya kupokea vifaa kutoka Bohari kuu ya Taifa ya dawa, waziri Ummy amesema amefanya maamuzi hayo kufuatia kupokea taarifa ya uchunguzi ofisini kwake juu ya ubadhilifu wa...

Like
218
0
Monday, 15 February 2016
TAMASHA LA MCHIZI WANGU LAFANA JIJINI DAR ES SALAAM
Entertanment

93.7 Efm Radio,kuadhimisha tamasha kubwa la Mchizi wangu lililofanyika siku ya wapendanao tarehe 14/02/2016, likiongozwa na mziki wa mchiriku na singeli. Tamasha hilo lilisheheni Wasani kibao wakitumbuiza huku wakiongozwa na msaga sumu na skide mtoto wa mama shante. Umati wa watu ukisheheni katika tamasha la mchizi wangu concert   Raisi wa singeli Suleiman Jabir a.k.a Msaga Sumu akitumbuiza mashabaki waliofika kwenye tamasha la Mchizi Wangu. Amsha amsha kutoka kwa baadhi ya mashabiki wakionyesha nyuso za furaha wakati wakipata burudani....

Like
504
0
Monday, 15 February 2016
MUSEVENI: NINA IMANI NITASHINDA UCHAGUZI
Global News

RAIS wa Uganda Yoweri Museveni amesema ana imani atashinda urais kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika siku ya Alhamisi wiki hii. Hata hivyo, amesema yuko tayari kukabidhi madaraka kwa mtu mwingine iwapo chama chake kitashindwa. Akijibu maswali ya waandishi wa Habari  wakati wa kikao kilichofanyika Ikulu jana Jumapili, Bwana Museveni amesema kwa sasa haoni chama chochote ambacho kinaweza kuondoa chama cha National Resistance Movement (NRM)...

Like
348
0
Monday, 15 February 2016
KURA ZAHESABIWA AFRIKA YA KATI
Global News

MAAFISA wa uchaguzi wanaendelea kuhesabu kura baada ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kuandaa jana awamu ya pili iliyocheleweshwa ya uchaguzi wa rais na wabunge, ikiwa na matumaini ya kupatikana amani baada ya kutokea machafuko makubwa ya kidini kuwahi kushuhudiwa nchini humo tangu uhuru mwaka wa 1960. Upigaji kura ulifanywa chini ya ulinzi mkali huku maelfu ya wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wakiwekwa kote nchini humo, lakini uchaguzi huo ulikamilika kwa amani. Matokeo ya mwanzo yanatarajiwa kutangazwa...

Like
151
0
Monday, 15 February 2016
PROF. MBARAWA: SERIKALI BADO INA MASHAKA NA WATENDAJI ATCL
Local News

WAZIRI wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Profesa  Makame Mbarawa amesema Serikali bado ina mashaka na watendaji wa shirika la ndege la taifa ATCL na ili kuondoa dukuduku hilo inaendelea na uchunguzi wa kuwabaini watendaji wote waliohusika kulihujumu shirika hilo. Profesa Mbalawa ameyasema hayo jijini Mwanza kwenye mkutano wa sita wa sekta ya uchukuzi  katika ukanda wa Afrika ya kati kwa lengo la kutathmini maendeleo katika sekta hiyo pamoja na changamoto zake  uliowakutanisha mawaziri wa sekta hiyo kutoka nchi tano za...

Like
189
0
Monday, 15 February 2016
NJOMBE: UONGOZI WA HOSPOTALI YA HALMASHAURI UMEPEWA SIKU 90 KUREKEBISHA MAPUNGUFU YA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA
Local News

UONGOZI wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Njombe umepewa muda wa siku 90 kurekebisha mapungufu ya utoaji wa huduma za afya, vinginevyo  hospitali hiyo itafungwa.   Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati akizungumza na viongozi, Mganga Mkuu wa Mkoa, Samwel Mgema na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Imelda Mwenda na watumishi wa hospitali hiyo. Dkt. Kigwangalla alitoa agizo kufuatia ziara yake ya ukaguzi wa hospitali, vituo vya afya...

Like
310
0
Monday, 15 February 2016
« Previous PageNext Page »