BODI YA WADHAMINI CUF KUMFUNGULIA KESI LIPUMBA NA MSAJILI

BODI YA WADHAMINI CUF KUMFUNGULIA KESI LIPUMBA NA MSAJILI

Like
176
0
Wednesday, 05 October 2016
Slider

Bodi ya wadhamini CUF imefungua maombi ya kufungua kesi katika Mahakama Kuu dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa,Jaji Francis Mutungi, Prof Ibrahim Lipumba na wanachama 12 waliosimamishwa uanachama wa chama hicho. Katika maombi hayo bodi hiyo inaomba kibali cha kufungua kesi dhidi ya Msajili, Lipumba na wenzake, ili mahakama itoe amri ya kumzuia Msajili asifanye kazi nje ya mipaka ya mamlaka yake kisheria. Jana wajumbe wanne wa bodi hiyo waliibuka na kuunga mkono msimamo wa msajili wa vyama vya siasa na kupanga kuwakutanisha Profesa Lipumba na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif ili kumaliza mgogoro.

Comments are closed.