Global News

Uingereza: May aungwa mkono na mawaziri kuhusu Brexit
Global News

Waziri Mkuu Theresa May ameungwa mkono na baraza lake la mawaziri kuhusiana na rasimu ya makubaliano kati ya serikali yake na Umoja wa Ulaya, juu ya masharti ya Uingereza kujiondoa ndani ya umoja huo ifikapo Machi 2019. Ilichukua mazungumzo ya zaidi ya masaa matano, ambayo Bi May ameyaelezea kuwa ”marefu, yaliyogusa undani wa mambo, na yenye mjadala wa wazi.” Katika taarifa fupi aliyoisoma kwa vyombo vya habari baada ya kukubaliana na mawaziri wake, Bi May alisema ana imani thabiti kwamba rasimu ya...

Like
495
0
Thursday, 15 November 2018
Waziri wa ulinzi wa Israel Lieberman ajiuzulu
Global News

Waziri wa ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman amejiuzulu kwa ghafla akilalamika dhidi ya makubaliano ya kuweka chini silaha yaliyofikiwa pamoja na wanamgambo wa Hamas. Uamuzi wa kujiuzulu Avigdor Liebermann unaidhoofisha sana serikali ya mseto ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu na huenda ukapelekea uchaguzi kuitishwa kabla ya wakati. Liebermann anasema makubaliano ya kuweka chini silaha yaliyofikiwa pamoja na viongozi wa Gaza ni sawa na kusalim amri mbele ya ugaidi baada ya siku mbili za mapaigano makali. Liebermann alipendelea hatua kali zaidi...

Like
489
0
Thursday, 15 November 2018
Unaweza kutambua vipi mtoto wako anaugua kisukari?
Global News

Ulimwengu unapoadhimisha siku ya ugonjwa wa kisukari, utafiti uliyofanywa na shirikisho la kimataifa la ugonjwa wa kisukari (IDF) umebaini kuwa wanne kati ya wazazi watano hawana uwezo kung’amua dalili za mapema za ugonjwa huo kwa watoto wao. Awali ugonjwa wa kisukari ulihusishwa na watu wanene na wazee lakini miaka ya hivi karibuni watoto wachanga pia wamejikuta wakikabiliwa na maradhi hayo. Ili kufahamu kwanini watoto pia wanakabiliwa na ugonjwa huu BBC imezungumza na Farhia Mohammed kutoka mtaa wa Eastleigh jijini Nairobi,...

Like
844
0
Wednesday, 14 November 2018
Palestina na Israel zatatiza UN
Global News

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kukubaliana na mwenendo wa ghasia zilizotokea hivi karibuni kati ya Israel na Palestina katika Ukanda wa Gaza. Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa Riyad Mansour ameilaumu Marekani kwa kuwa kipingamizi. Mapigano makali kuwahi kutokea katika kipindi cha muda wa miaka minne, yaliibuka siku ya Jumapili iliyopita baada wa wapiganaji wa Hamas kuingilia kati operesheni za siri zilizokuwa zikifanywa na Israel katika ukanda wa Gaza. Chama cha Wapalestina cha Hamas kimesema kinachunguza...

Like
559
0
Wednesday, 14 November 2018
Uchaguzi DRC: Felix Tshisekedi asema hamuungi mkono mgombea wa upinzani
Global News

Felix Tshisekedi kiongozi wa chama kikubwa zaidi cha kisiasa nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, ameondoa uungwaji mkono wake wa kuwa na mgombea mmoja wa upinzani kwa uchaguzi ambao utafanyaika Disemba 23. Kiongozi huyo wa chama cha Union for Democracy and Social Progress alitoa tangazo hilo siku moja bada ya makuabaliano hayo kutangazwa. “Ninasema kuwa makubaliano yaliyoafikiwa Geneva hayajakubaliwa mashinani na yalikataliwa nao. Kutokana na hilo, ninaondoa uungwaji mkono wangu kutoka kwa makubaliano hayo, tuliyoyasaini jana,”...

Like
407
0
Tuesday, 13 November 2018
Mgawanyiko wazuka ndani ya upinzani nchini DRC
Global News

Vigogo wa vyama vikuu, kikiwemo kile cha UDPS, wametupilia mbali chaguo la viongozi wao hapo jana mjini Geneva, Uswisi, huku wafuasi wa vyama hivyo wakielezea huzuni yao kuhusu uteuzi wa Martin Fayulu. Upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umegawanyika baada ya kuteuliwa kwa Martin Fayulu kuwa mgombea pekee wa urais kwenye uchaguzi ujao wa Desemba 23. Vigogo wa vyama vikuu, kikiwemo kile cha UDPS, wametupilia mbali chaguo la viongozi wao hapo jana mjini Geneva, Uswisi, huku wafuasi wa vyama...

Like
458
0
Tuesday, 13 November 2018
Gabon;Rais Bongo aelezwa kuwa mgonjwa
Global News

Rais wa Gabon Ali Bongo ameelezwa kuwa ni mgonjwa, lakini hata hivyo kwa sasa anaelezwa kupata nafuu. Habari zilizosambaa kuhusiana na Rais huyo mwenye umri wa miaka 59, zinasema kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi. Alikuwa akitibiwa Afrika kusini, huku taarifa za awali zilizotolewa mwezi uliopita zikisema kuwa alikuwa akisumbuliwa na uchovu. Hakujakuwa na taarifa zozote rasmi kuhusiana na afya ya rais tangu matangazo ya mwanzo yalipotolewa kuhusiana na afya yake kwamba amechoka na anahitaji mapumziko. Msemaji wake Ike Ngouoni...

1
936
0
Monday, 12 November 2018
Maadhimisho ya miaka 100 tangu kumalizika WW1 yafanyika Ufaransa
Global News

Rais wa Ufaransa anatarijiwa kuwa mwenyeji wa marais Donald Trump, Vladimir Putin na viongozi wengine wa dunia mjini Paris kwa ajili ya kuadhimisha miaka 100 tangu kumalizika Vita Vikuu vya Kwanza. Rais Emmanuel Macron amedhoofika kisiasa baada ya kufanya ziara kaskazini mashariki mwa Ufaransa ambako alilazimika mara kwa mara kutega sikio lake ili kusikiliza malalamiko ya watu juu ya sera zake ambazo haziungwi mkono na wananachi wa kawaida aliotarajia kuhusiana nao vizuri. Ziara ya siku sita alizofanya kwenye majimbo, miji...

Like
873
0
Friday, 09 November 2018
Sita wakamatwa kupanga kumshambulia Macron
Global News

Maafisa wa usalama nchini Ufaransa wamesema wamewakamata watu sita wanaoshukiwa kupanga njama za kumshambulia rais wa nchi hiyo Emmanuel Macron Afisa mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema maafisa wa ujasusi wanawashikilia washukiwa hao sita katika maeneo matatu tofauti, mmoja akiwa maeneo ya milima ya Alps, Mwengine Brittany na washukiwa wengine wanne wakizuiliwa karibu na mpaka wa Ubelgiji na Ufaransa mjini Moselle. Mpango huo wa kumlenga rais wa Ufaransa ulionekana kutokuwa dhahiri na usiokamilika, lakini ulikuwa ni wa vurugu...

Like
448
0
Thursday, 08 November 2018
Trump amfukuza kazi Mwanasheria mkuu
Global News

Rais wa Marekani Donald Trump amemfukuza kazi Mwanasheria mkuu wa nchi hiyo Jeff Session. Akitoa taarifa kupitia mtandao wa Twitter, Rais Trump amesema nafasi yake hiyo itashikwa kwa muda na mwanasheria Matthew Whittaker. Katika ukurasa wake wa Twitter Rais wa Marekani amemshukuru mwanasheria huyo mkuu Jeff Sessions kwa kazi yake hiyo na kumtakia kila la kheri. Kwa upande wake, Jeff Sessions katika barua yake ya kujiuzulu, aliweka bayana kuwa uamuzi wa kuondoka katika nafasi hiyo haukuwa wake. Katika barua isiyokuwa...

Like
446
0
Thursday, 08 November 2018
Mapambano yapamba moto Hodeida
Global News

Wanajeshi wa serikali na waasi wamepambana tena leo karibu na mji wa bandari wa Yemen, Hodeida, ambao ni muhimu katika upitishaji wa msaada wa kiutu. Siku tano za mapambano kati ya waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran na jeshi, likisaidiwa na muungano wa kikanda wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia, zimesababisha vifo vya Zaidi ya watu 150 katika mkoa wa Bahari ya Sham wa Hodeida. Msemaji wa wa muungano unaoogozwa na Saudia amesema hawana mipango ya kufanya mashambulizi kamili...

Like
536
0
Wednesday, 07 November 2018