Category: Sports

  • BAHATI NASIBU YAIPELEKA GUINEA ROBO FAINALI

    BAHATI NASIBU YAIPELEKA GUINEA ROBO FAINALI

    Kamati ya utendaji ya Shirikisho la Kandanbda Africa CAF imetangaza kwamba Guinea ndio imeshinda katika bahati nasibu ya kusonga mbele dhidi ya Mali.

    Uwamuzi ulichukuliwa Alhamisi saa kumi saa za Africa Magharibi mjini Malabo, na hivyo sasa Guinea itapambana na Ghana na Algeria itapambana na Ivory Coast.

    AAAAA

     

  • CHELSEA MBIONI KUMYAKUA JUAN CUADRADO

    CHELSEA MBIONI KUMYAKUA JUAN CUADRADO

    Klabu ya Chelsea ipo kwenye hatua za mwisho kumsainisha mshambuliaji Juan Cuadrado mwenye umri wa miaka 26

    Juan Cuadrado ambae ni raia wa Colombia amekubaliana na dili hilo na viongozi wa ligi na klabu hivyo yupo katika hatua za mwisho za uhamiaji utakogharimu paundi milioni 26.8 kutoka kwenye klabu ya Fiorentina ya huko Italia.

     

    Ujio wa Cuadrado’s katika klabu ya Chelsea unamaana yakuwa mshambuliaji mwenye umri wa miaka 24 kutokea Ujerumani Andre Schurrle kwa sasa kuna uhakika wa yeye kuondoka Stamford Bridge kabla ya jumatatu ambayo ni tarehe ya mwisho ya uhamisho

  • FIFA: BLATTER AREJESHA FOMU KUWANIA URAIS

    FIFA: BLATTER AREJESHA FOMU KUWANIA URAIS

    Rais wa shirikisho la mpira wa miguu duniani Sepp Blatter leo amerudisha fomu za kuwania kugombea urais wa shirikisho hilo kwa awamu ya tano

    Kupitia akaunti yake ya Twitter Blatter aliandika

    “Today (Thursday) is a key date in the electoral calendar. I’ve made my submission, now the electoral committee follow a process,”

    akimaanisha kuwa leo ni siku muhimu katika kalenda ya uchaguzi na amefanya maamuzi hayoya kurudisha fomu hivyo anaichia kazi kamati ya Uchaguzi ifanye kazi yake

    alisema Blatter mwenye umri wa miaka 78, ikiwa leo ni siku ya mwisho kwa wagombea kurejesha fomu zao

    Blatter ambae amekuwa akishikilia nafasi hiyo toka mwaka 1998, tayari ameonyesha nia yake kuomba kugombea kwa kipindi kingine cha uongozi wa shirikisho hilo la soka duniani na kupata sapoti kubwa kutoka Afrika, Asia n.k

    Miongoni mwa wapinzani wake yupo mchezaji wa zamani wa Ureno na Real Madrid mshambuliaji Luis Figo, Michael Van Praag, Ali bin Al Hussein, Jerome Champagne na alikuwa mchezaji wa wa Ufaransa David Ginola.

  • AFCON: KOCHA WA IVORY COAST AMESEMA MASHINDANO YANAANZA SASA

    AFCON: KOCHA WA IVORY COAST AMESEMA MASHINDANO YANAANZA SASA

    Kocha wa Ivory Coast Herve Renard amesema mashindano ya kombe la mataifa Afrika yameanza sasa kwa timu yake baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Cameroon siku ya jumatano ambapo ushindi huo uliwapeleka katika hatua ya robo fainali.

    Kocha alisema

    “kwa timu kama hii kombe la mataifa ya afrika linaanza katika robo fainali kwasababu kutolewa kabla ya kuifikia hatua hiyo ni kushindwa ” alisema kocha huyo Mfaransa ambae timu yake ameweza kupenya kwenye hatua hiyo ngumu na kuziacha timu kama Cameroon na Senegal ambazo zimeshindwa kutamba

    aliongeza kwa kusema kama hautakutana na timu kama Cameroon au Ivory Coast ama Senegal basi lazima utaonyeshewa vidole

    Kocha huyo amesema Mchezo kati yao na Algeria utakuwa mgumu saana kwa mara nyingine tena hivyo hapo ndipo michuano inapoanza

  • BAFANABAFANA WAIPISHA GHANA ROBO FAINALI AFCON

    BAFANABAFANA WAIPISHA GHANA ROBO FAINALI AFCON

    Andre Ayew Amefanikiwa kuipeleka Ghana robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika  afcon baada ya kuwapa kichapo cha 2-1 afrika ya kusini na kuibuka washindi wa kundi c.

    Black Stars wa Ghana, wamewahi fikia  nusu fainali mara nne mfululizo katika michuano ya afcon, Walihfiwa kutolewa katika dakika ya 17 ambapo Mandla Masango kuipatia Afrika Kusini goli la kwanza.

    Matumaini ya ghana yalirejea Wakati mlinzi John Boye aliposawazisha katika dakika 73 na baadae dakika saba kabla kumalizika kwa mchezo ayew akafanikisha goli la pili kutokana na mpira wa kona uliopigwa na abdul rahman baba

    Wakati huo huo, Algeria waliibuka na ushindi wa magoli mawili  dhid iya wapinzani wao Senegal

  • ZAMBIA NA CAPE VERDE WAIAGA MICHUANO YA AFCON

    ZAMBIA NA CAPE VERDE WAIAGA MICHUANO YA AFCON

    Cape Verde na Zambia wameondolewa katika michuano ya Kombe la Mataifa afrika AFCON yanayofanyika Guinea ya Ikweta Afrika baada ya sare 0-0 katika mechi kugongwa na dhoruba kitropiki.

     

    Tunisia ilifanikiwa kushinda katika kundi B na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilikamata nafasi ya pili baada ya kutoka sare ya goli 1-1 katika mji wa bandari Bata wakati huo huo.

     

    Cape Verde amemaliza hatua ya mtoano kwa tofauti ya pointi na magoli na DR Congo, ambapo wamepoteza kwasababu walifunga bao moja tu katika mechi tatu wakati wa Kongo walifunga katika mechi mbili.

    Mvua kubwa, radi, umeme na upepo mkali vilifanya mpira mzuri ushindikane na wakati Zambia ilipata nafasi dakika za majeruhi wakati kwenye dakika nane za mwisho, Mukuka Mulenga alikosa goli zote kwa kupiga shuti nje ya mlango

    Ni mara ya pili mfululizo kwa Zambia Chipolopolo (Bullets Copper) ktoka katika hatua ya mtoano na kushindwa kutetea ubingwa wao wa mwaka 2012

  • AFCON: KUFA AMA KUPONA ZAMBIA KUINGIA DIMBANI LEO

    AFCON: KUFA AMA KUPONA ZAMBIA KUINGIA DIMBANI LEO

    Mabingwa watetezi Afcon Zambia wanatakiwa kuendeleza ubabe leo dhidi ya Cape Verde ili kuendeleza matumaini yao ya kufika robo fainali ya michuano hiyo inayofanyika Equatorial Guinea

    Zambia wana wakati mgumu katika kundi B ambapo wanaomba Tunisia wanaoongoza kundi hilo watoke suluhu au wafungwe na DRC

    Kwa sasa Tunisia wana pointi nne wakifuatiwa na Cape Verde na Drc huku Zambia ikiwa katika nafasi ya pili

  • MAAJABU YA EQUATORIAL GUINEA MICHUANO YA AFCON

    MAAJABU YA EQUATORIAL GUINEA MICHUANO YA AFCON

    Kocha wa Equatorial Guinea Esteban Becker ameeleza mafanikio na malengo ya taifa hilo mwenyeji wa michuano hiyo katika kufikia robo fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika na kufananishwa na hadithi za Cinderela baada ya kuichapa Gabon

    2-0 siku ya Jumapili.

    “Ni hadithi ya Cinderela ambapo temu kapuku ilipoichapa timu tajiri kwa faida. Shukran kwa kujitolea sadaka. Kujidhati kwao, uzalendo na mapenzi yao” alisema kocha huyo raia wa Argentina

    ni story itakayokumbukwa kwa Becker mwenyewe kwani alichaguliwa kuwa kocha wa kikosi hicho mwanzoni mwa mwezi huu

  • DIDIER DROGBA: BADO NAHITAJI KUITUMIKIA CHELSEA

    DIDIER DROGBA: BADO NAHITAJI KUITUMIKIA CHELSEA

    Didier Drogba amesema kuwa bado anahitaji kuitumikia klab ya Chelsea mara baada ya msimu huu wa ligi ya England

    Mshambuliaji huyo wa Ivory Coast alitangaza nia yake hiyo wakati anapokea tuzo ya mwaka inayoandaliwa na shirikisho la waandishi wa habari za mpira wa miguu kwa mwaka 2015 huko London.

    Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 36 ameelezea mapenzi yake kwenye klabu hiyo na kuongeza ya kuwa bado anahitaji kuwa sehemu ya klabu hiyo siku zijazo na ikibidi kucheza na wachezaji wapya na kuifanyia mengi makubwa.

  • TETESI ZA MAGAZETI YA NG’AMBO

    TETESI ZA MAGAZETI YA NG’AMBO

    TETESI ZA MAGAZETI:

    Klabu ya Manchester United imeweka mezani kitita cha paundi milioni 61 ili kumsajili kiungo wa klabu ya Juventus PAUL POGBA huku Chelsea nayo ikionekana kumuhitaji mchezaji huyo.

    (Daily Express)

    Klabu ya Valencia na Liverpool zimeingia katika kinyanganyiro  cha kuisaka saini ya kiungo wa Manchester City JAMES MILNER.

    (Sky Sports)

    Klabu ya Arsenal na Manchester United zipo katika kinyanganyiro cha kuisaka saini ya beki wa kati wa klabu ya Villarreal GABRIEL PAULISTA kwa paundi milioni 16.

    (Daily Mail)

    Klabu ya Chelsea ipo katika mazungumzo na klabu ya Fiorentina ili kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo JUAN CUADRADO kwa kitita cha paundi milioni 20.

    (Guardian) 

    Klabu ya Wigan Athletics imewekamezani paundi milioni 4 ili kumsajili mshambuliaji wa klabu ya West Brom  CALLUM McMANAMAN.

    (Goal.com)

    Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea ANDRE SCHURRLE yupo tayari kuihama timu hiyo na kutimkia katika klabu ya nyumbani Wolfsburg.

    (Independent)

     

  • ODEGAARD ATUA BERNABEU

    ODEGAARD ATUA BERNABEU

     

    Real Madrid imefikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji kutoka klabu ya Stromsgodset ya Norway Martin Odegaard mwenye umri wa miaka 16.

    Real Madrid hawakuweka wazi makubaliano yao na mshambuliaji huyo lakini vyombo vya habari vya Hispania vimeripoti kuwa wamelipia si chini ya euro milioni tatu kumpata mchezaji huyo

    Anatarajiwa kuungana na klabu ya Real Madrid timu B ambayo inaongozwa na mwalimu Zinedine Zidane