Category: Slider

  • Hakuna kiwango cha pombe kilicho salama kwa afya yako

    Hakuna kiwango cha pombe kilicho salama kwa afya yako

    Ni habari mbaya kwa wale wanaofurahia kile wanachofikiri ni kikombe kimoja cha divai kwa siku.

    Utafiti mpya wa kimataifa ulimwenguni uliochapishwa katika jarida la Lancet umethibitisha utafiti uliopita ambao umeonyesha kwamba hakuna kiwango salama cha matumizi ya pombe.

    Watafiti wanakubali kwamba unywaji wa kiwango cha kadri unaweza kukulinda dhidi ya ugonjwa ya moyo lakini waligundua kwamba hatari ya saratani na magonjwa huzidi faida yoyote ya pombe mwilini.

    Mwandishi wa utafiti alisema matokeo yake yalikuwa muhimu kwa sasa kwa sababu ya mambo mengi yalioangaziwa.

    Utafiti wa magonjwa ulimwenguni uliangazia kiwango cha matumizi ya pombe na madhara yake ya afya katika nchi 195, ikiwemo Uingereza kati ya 1990 na 2016.

    Uchambuzi wa data miongoni mwa watu wenye kati ya umri wa miaka 15 hadi 95, watafiti walitofautisha kati ya watu wasiotumia pombe kabisa na wale ambao hutumia kikombe kimoja cha pombe kwa siku.

    Waligundua kwamba kati ya watu 100,000 wasiokunywa pombe, 914 watakuwa na tatizo la afya linalohusiana na pombe ama kupata madhara.

    Lakini watu wanne zaidi wataathiriwa iwapo watakunywa kikombe kimoja cha pombe kwa siku.

    Kwa watu ambao waliokunywa vikombe viwili vya pombe kwa siku, watu 63 zaidi walipata madhara katika kipindi cha ndani ya mwaka mmoja na kwa wale waliokunywa vikombe vitano vya pombe kila siku kulikuwa na watu 338 zaidi waliopata madhara ya kiafya.

    Mmoja wa waandishi wa utafiti huo, Profesa Sonia Saxena, mtafiti katika chuo cha Imperial mjini, alisema: “Unywaji wa kikombe kimoja kwa siku unaongeza hatari ndogo lakini ikilinganishwa na idadi kuu ya raia wa London inawakilisha idadi kubwa na kwamba wengi wao hawatumii kikombe kimoja kwa siku.

    Mwandishi anayeongoza utafiti huo Dk Max Griswold, katika Taasisi ya Matibabu na Tathmini ya Afya (IHME), Chuo Kikuu cha Washington, alisema: “Uchunguzi uliopita umeonyesha kinga ya pombe kwa hali fulani, lakini tumegundua kwamba hatari za pamoja za kiafya za pombe huongezeka kwa kiasi kwa kutumia kiwango chochote cha pombe.

    “Ushirika wa juu kati ya matumizi ya pombe na hatari ya saratani, majeruhi, na magonjwa ya kuambukiza hupunguza madhara ya kinga ya ugonjwa wa moyo katika utafiti wetu.

    “Ingawa hatari za afya zinazohusiana na pombe huanza kuwa ndogo kwa kunywa kikombe kimoja kwa siku, na huongezeka kwa haraka kadri ya watu wanapoendelea kunywa zaidi.”

    Mnamo mwaka wa 2016, serikali ilipunguza viwango vya pombe ilivyopendekeza kwa wanaume na wanawake kutozidi 14 kwa wiki – sawa na chupa sita za pombe ya wastani au glasi saba zamvinyo

    Wakati huohuo, Profesa Dame Sally Davies, afisa mkuu wa matibabu nchini Uingereza, alisema kuwa kiasi chochote cha pombe kinaweza kuongeza hatari ya saratani.

    Prof Saxena alisema utafiti huo ulikuwa ni utafiti muhimu zaidi uliofanywa juu ya somo hilo.

    Alielezea: “Utafiti huu umepiga hatua zaidi kuliko mwengine kwa kuzingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na mauzo ya pombe, taarifa za kujitegemea juu ya kiasi cha kunywa pombe, kujizuia, data ya utalii, viwango vya biashara haramu na pombe zinazotengezwa nyumbani.”

    Utafiti huo unaonyesha kwamba wanawake wa Uingereza hunywa vinywaji wastani vya chupa tatu za pombe kwa siku na wameorodheshwa katika nafasi ya nane katika ulimwengu wa watu wanaobugia viwango vya juu vya pombe.

    Wanaume wa Uingereza kwa kulinganisha, wako katika nafasi ya 62 kati ya nchi 195 zilizofanyiwa utafiti, ingawa pia hunywa wastani wa chupa tatu za pombe kwa siku.

    Hii ni kwa sababu viwango vya unywaji pombe vilikuwa vya juu zaidi kwa ujumla kati ya wanaume, na wanaume wa Kiromania hunywa vinywaji zaidi ya nane kila siku.

    Kinywaji kilielezewa kuwa na gramu 10 za pombe, ambayo inafanana na glasi ndogo ya divai, chupa ya bia, au whisky.

    Kote duniani, mtu mmoja kati ya watu watatu wanakunywa pombe na inahusishwa na vifo vyote kwa wale wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 49

    Prof Saxena alisema: “Wengi wetu nchini Uingereza hunywa zaidi ya mipaka salama, na kama utafiti huu unaonyesha hakuna viwango salama.

    Mapendekezo yanahitaji kuwafikia watu wengi zaidi na serikali inapaswa kufikiria upya sera yake.

    Iwapo unataka kunywa, jifunze mwenyewe kuhusu hatari, na kuchagua hatari unayoijua”

    cc;- bbcswahili

  • Wagombea wa upinzani walalamikia dosari uchaguzi DRC

    Wagombea wa upinzani walalamikia dosari uchaguzi DRC

    Wagombea wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamelalamikia dosari nyingi wanazosema zilitokea wakati wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumapili.

    Milolongo mirefu ya wapiga kura ilishuhudiwa katika vituo vingi na mitambo ikafeli kwenye baadhi ya vituo.

    Aidha, upigaji kura uliathiriwa katika baadhi ya maeneo baada ya mvua kubwa kunyesha, huku baadhi ya wapiga kura wakilalamikia majina yao kutokuwepo kwenye sajili katika baadhi ya vituo.

    Mmoja wa wagombea wa urais wanaotaka kumrithi Rais Joseph Kabila anayeondoka baada ya kuongoza kwa miaka 17, Felix Tshisekedi, amesema anahofia kwamba huenda hitilafu hizo zilipangwa ndipo kutoa sababu za uchaguzi kufutwa na kumuwezesha Bw Kabila kusalia madarakani.

    Wengi wa wapiga kura walitatizika kutokana na hali kwamba mashine zilitumiwa kwa mara ya kwanza kupigia kura.

    Wanaharakati walitumia vifaa vya uchaguzi kutoka kwa uchaguzi wa awali kuandaa uchaguzi wa uigizaji

     

    Aidha, baadhi ya mashine zilifeli.

    Bw John Tendwa, ambaye ni jaji mstaafu nchini Tanzania na aliwahi kuhudumu kama Msajili mstaafu wa Vyama vya Siasa nchini humo amesema iliwachukua baadhi ya wapiga kura hadi dakika saba kupiga kura kituoni.

    Shughuli ya kuhesabu kura zilizopigwa inaendelea baada ya vituo kufungwa Jumapili jioni na matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa katika kipindi cha wiki moja.

    Uchaguzi wa sasa ulifaa kufanyika miaka miwili iliyopita lakini uliahirishwa mara kadha kutokana na kutokamilika kwa maandalizi.

    Kabla ya uchaguzi, kulitokea utata baada ya uchaguzi kuahirishwa katika maeneo yaliyoathiriwa na Ebola yakiwemo miji ya Beni na Butembo mashariki mwa nchi hiyo, na pia katika jiji la Yumbi magharibi mwa nchi hiyo.

    Hatua hiyo iliathiri takriban wapiga kura 1.26 milioni kati ya jumla ya wapiga kura 40 milioni. Uchaguzi katika maeneo hayo uliahirishwa hadi Machi.

    Uamuzi huo ulizua utata ikizingatiwa kwamba rais mpya anafaa kuapishwa kufikia katikati mwa Januari.

    Baadhi ya wanaharakati waliandaa uchaguzi wa mwisho uliopewa jina ‘uchaguzi wa raia’ katika mji wa Goma, mojawapo wa miji iliyoathiriwa, anasema mwandishi wa BBC Gaius Kowene.

    Rais Kabila alipiga kura mapema asubuhi mjini Kinshasa katika shule ambayo mgombea anayemuunga mkono, waziri wa zamani wa mambo ya ndani Emmanuel Ramazani Shadary alikuwa pia anapiga kura.

    Baada ya kupiga kura, aliambia wanahabari: “Ni wazi kwamba uchaguzi huu ni huru na wa haki, na bila shaka utakuwa huru na wa haki.”

    Alisema wasiwasi wake pekee ulikuwa kwamba mvua ingeathiri idadi ya watu ambao wangejitokeza kupiga kura.

    Baraza kuu la maaskofu wa kanisa Katoliki (CENCO) lilisema mashine za kupigia kura zilikumbwa na hitilafu katika takriban vituo 544 kati ya 12,300 katika maeneo ambayo walifuatilia upigaji kura.

    Baadhi ya wapiga kura walilalamika kwamba majina yao hayakupatikana kwenye sajili ya wapiga kura.

  • Jeshi la Zimbabwe lalaumiwa kwa ‘kutumia nguvu kupita kiasi’

    Jeshi la Zimbabwe lalaumiwa kwa ‘kutumia nguvu kupita kiasi’

    Jeshi la Zimbabwe lilitumia “nguvu nyingi” dhidi ya waandamanaji wa upinzani baada ya uchaguzi wa kiti cha Urais.

    Hayo yamesemwa na tume maalum iliyoundwa kuchunguza kiini cha ghasia zilizotokea nchini humo.

    Watu 6 waliuwawa, baada ya vikosi vya jeshi kutumwa ili kukabiliana na waandamanaji hao waliozua ghasia katika maeneo kadhaa ya mji mkuu Harare mnamo Agosti 1.

    Tume huru ya uchunguzi huo, inasema jeshi lilitenda mabaya makubwa bila huruma, wakati ilipoamua kuwamiminia risasi waandamanaji waliokuwa wakitoroka.

    Lakini baadhi ya viongozi wa upinzani wanalaumiwa kwa kuchochea ghasia.

    Wanajeshi na polisi walikabiliana na waandamanaji ambao walimiminika barabarani, baada ya kuibuka madai kwamba chama tawala cha Zanu-PF, kiliiba kura Julai 30.

    “Matokeo ya uchunguzi yanabaini kuwa mauwaji ya watu hao 6, yalitokana na hatua ya jeshi na polisi,” sehemu ya ripoti hiyo inasema.

    “Matumizi ya risasi yaliyoelekezewa watu, hasa walipokuwa wakitoroka, yanaonyesha bayana kuwa hayakuidhinishwa hasa kutokana na ukubwa wake,” inaongeza ripoti hiyo.

    Tume hiyo iliyo na wanachama 7 na ambayo iliundwa na Rais Emmerson Mnangagwa, kufuatia ushindi wake finyu wa Urais, ilibaini kuwa kutumwa kwa jeshi kutuliza uhasama huo mjini Harare ulifanywa kwa kufuata sheria.

    Mwenyekiti wa tume hiyo ni rais wa zamani wa Afrika Kusini Kgalema Motlanthe na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi wa Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange ni miongoni mwa wajumbe wake.

    Ripoti hiyo pia imekishutumu chama cha upinzani cha MDC Alliance, kwa kuchochea ghasia, hasa kutokana na hotuba ya baadhi ya viongozi wake.

    “Ikiwa maandamano hayo hayangekabiliwa, hali hiyo ingeongezeka na kuwa vigumu kuthibitiwa na hatimaye kuwa mbaya zaidi” inasema.

    Tume hiyo sasa imependekeza kuwa serikali iwalipe ridhaa familia zote za wahasiriwa na kwa watu kadhaa ambao pia walijeruhiwa wakati wa maandamano hayo.

    Siku ya Jumanne, Bwana Mnanagagwa, alisema kwamba, “watachunguza matokeo ya tume hiyo na kisha kufanya maamuzi”.

    “Nimeridhika kuwa tume hiyo ya uchunguzi ilifanya kazi yake kikamilifu,” aliongeza kusema.

    Lakini chama kikuu cha upinzani mara moja kilipuuzilia mbali ripoti hiyo na kusema serikali inajaribu “kukanusha” hatua ambayo jeshi la taifa hilo ilichukua.

    “Maoni yetu ni kwamba… kuelezea na kufananisha uwongo kati ya waandamaji waliokuwa hawajajihami na silaha na polisi waliotumia bunduki na risasi ni jambo la kutamausha.” msemaji mmoja wa MDC amesema.

    Mwezi uliopita, kinara mkuu wa MDC Nelson Chamisa aliksnusha kuhusika na maandamano yaliyotokea Agosti 1, huku akiwaita waandamaji ”wapumbavu”.

    “Lilikuwa jambo la kijinga, hata kwa watu walioandamana…lilikuwa jambo la kipumbavu, kwa sababu, walijiingiza na kujiweka wazi kushambuliwa,”aliwaambia waandishi habari.

    Katika siku hiyo hiyo ya maandamano, Bw Chamisa, alikataa kukubali kushindwa, huku akisema ameshinda kwa wingi wa kura.

    Bwana Mnangagwa alipata ushindi finyu wa asilimia 50.7%, ili kuzuia uchaguzi huo kurudiwa, alizoa chini ya kura 30,000 kuliko kiwango kinachohitajika ili kupata ushindi wa moja kwa moja.

  • Jangili asukumwa ndani na kuamriwa kuangalia filamu ya wanyama

    Jangili asukumwa ndani na kuamriwa kuangalia filamu ya wanyama

    Jangili mmoja nchini Marekani ameamriwa kuangalia filamu ya wanyama ya Bambi kila mwezi baada ya kukutwa na hatia ya kuua “mamia” ya mbawala.

    Muwindaji huyo kutoka Missouri David Berry Jr anatakiwa kuangalia filamu hiyo walau mara moja kwa mwezi wakati akitumikia kifungo chake cha mwaka mmoja gerezani.

    Alitiwa nguvuni mwezi Agosti pamoja na ndugu zake wawili kwa kuwaua mbawala, kisha kuwachinja na kuondoka na vichwa huku akiacha miili ya wanyama hao ioze, waendesha mashtaka wamesema.

    Kesi hiyo ni moja ya kesi kubwa zaidi za ujangili kuwahi kuripotiwa kwenye historia ya jimbo la Missouri.

    Pamoja adhabu ya kwenda jela kwa kuwinda mbawala kinyume cha sheria, Jaji Robert George alimuamuru Berry Jr “kuangalia filamu iliyoandaliwa na kampuni ya Walt Disney iitwayo Bambi, ambapo alitakiwa kuangalia kwa mara ya kwanza kabla ama Disemba 23 na baada ya hapo kuangalia walau mara moja kila mwezi,” katika kipindi chote atachokaa jela.

    Filamu hiyo ya katuni ya mwaka 1942 inaangazia maisha ya familia moja ya mbawara ambao walilazimika kuishi bila mama aliyeuawa na majangili.

    Uchunguzi wa miezi uliofanyika kwenye majimbo kadhaa ulipelekea kunaswa kwa Berry Jr, baba yake David Berry Sr na kaka yake Kyle Berry, limeripoti gazeti la the Springfield News-Leader.

    Japo idadi kamili ya mbawala waliouawa haijulikani, mhifadhi wa Kaunti ya Lawrence Andy Barnes amesema yaweza kufikia “mamia”.

    Berry Jr alipewa adhabu ya kwenda jela baada ya kukubali mashtaka yalikuwa yanamkabili.

    Amepewa adhabu pia ya kwenda jela siku 120 kwa kukiuka masharti ya dhamana yake ya matumizi ya silaha za moto. Vibali vya jangili huyo na baba yake vya kuwinda vimefutwa moja kwa moja na Kamisheni ya Uhifadhi ya Missouri.

     

  • Marekani yamzuia mama raia wa Yemen kumuona mtoto wake aliye karibu kufa

    Marekani yamzuia mama raia wa Yemen kumuona mtoto wake aliye karibu kufa

    Mama wa mtoto aliye raia wa Yemeni amezuiwa kumuona kijana wake aliye karibu kuaga dunia kutokana na sheria ya kuwazuia wageni kutoka nchini mwake, familia imeeleza.

    Mtoto Abdullah Hassan alizaliwa na maradhi ya ubongo ambapo madaktari walisema hataweza kuishi.

    Ndugu wanasema mama yake anataka kumuona kwa mara ya mwisho kabla ya kuondoa mashine ya kumsaidia kupumua.

    Baba yake anasema mama wa Abdullah hawezi kwenda nchini Marekani kutokana na marufuku iliyowekwa na utawala wa Trump.

    Abdullah na Baba yake ni raia wa Marekani, familia imeeleza.

    ”Anachotamani ni kushika mkono wa mtoto wake kwa mara ya mwisho”, Baba wa mtoto Ali Hassan aliliambia gazeti la San Francisco Chronicle.

    Amesema mtoto atapoteza maisha kama atapelewa Misri, ambako mama yake anaishi kwa sasa.

    Mke wa Hassan, Shaima Swileh, anatafuta ruhusa kutoka wizara ya mambo ya ndani ya Marekani ili aweze kuingia nchini humo haraka

    Marufuku kuingia Marekani

    Muda mfupi baada ya kuingia madarakani, Rais wa Marekani, Donald Trump aliweka marufuku ya kuingia Marekani akizigusa nchi kadhaa hasa za kiislamu.

    Marufuku hiyo imewekwa kwa raia wa nchi ya Iran, Korea Kaskazini,Venezuela,Libya,Somalia,Syria na Yemen.

    Hatua hiyo yaelezwa kuwa ni ‘ukatili’

    Saad Sweilem, kutoka Baraza la kiislamu la nchini Marekani, amesema kumzuia mama wa mtoto Abdullah ni ”ukatili wa hali ya juu”

    Baba wa Abdullah alizaliwa California, lakini amekuwa ana ndugu zake na familia iliko asili yao nchini Yemen.

    Hassan alikutana na mkewe nchini Yemen, na wawili hao walipata watoto saba nchini humo.

    Abdullah alikutwa na maradhi ya ubongo kwa kitaalamu hypomyelination ambayo yameathiri uwezo wake wa kupumua.

    Alipokua na umri wa miezi minane,familia iliondoka Yemen kuelekea Cairo, kukwepa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

    Takriban miezi mitatu illiyopita, Bwana Hassan alimpeleka mtoto nchini Marekani kwa ajili ya kupata matibabu, akiwa na matarajio kuwa mke wake ataungana nao baadae.

    Lakini baada ya madaktari mjini Oakland, California, kumjulisha kuwa hali ya mtoto ni mbaya sana, familia ilianza kushughulikia vibali vya kumuwezesha mama wa mtoto kufika Marekani.

    Wamesema walipokea barua ya kukataliwa ombi lao kutoka wizara ya mambo ya ndani, wakirejea marufuku iliyowekwa na Trump.

    Afisa kutoka idara hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina alikataa kujadili kuhusu suala hilo.

  • Mahakama yamshushia rungu Rais wa zamani

    Mahakama yamshushia rungu Rais wa zamani

    Mahakama Kuu nchini Afrika Kusini imeamuru Rais wa zamani wa nchi hiyo, Jacob Zuma kulipia gharama zote za kesi zilizofunguliwa dhidi yake alipokuwa madarakani.

    Mahakama hiyo ya Kaskazini mwa Guateng imeeleza kuwa Zuma atapaswa kulipia gharama zote za uendeshaji kesi zake tangu mwaka 2005 bila kuihusisha Serikali.

    “Serikali haihusiki na gharama zozote za kesi dhidi ya Bw. Jacob Zuma, katika mashtaka ya jinai yaliyofunguliwa dhidi yake kwa namna yoyote,” imeeleza sehemu ya uamuzi wa Mahakama Kuu.

    “Mwendesha Mashtaka wa Serikali anaelekezwa kufanya majumuisho ya gharama zote zilizoingiwa katika kesi dhidi ya Bw. Zuma ambazo zilikuwa na mashtaka binafsi, ili aweze kukabidhiwa gharama zake kwa ajili ya malipo,” imeongeza.

    Chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance (DA), mwezi Machi mwaka huu kilianza mchakato wa kisheria wa kutaka Zuma alipe kiasi cha $1.3 bilioni ambazo ni pesa za walipa kodi zilizotumika katika kugharamia kesi binafsi dhidi yake alipokuwa madarakani.

    Kiongozi wa chama hicho, Mmusi Maimane alisema kuwa kama kuna makubaliano yoyote kati ya Rais Cyril Ramaphosa kuhusu Serikali kulipia gharama hizo ni lazima yawekwe hadharani.

     

  • Ongezeko la joto sasa ni tishio kwa binaadamu

    Ongezeko la joto sasa ni tishio kwa binaadamu

    Umoja wa mataifa umeonya kuwa ongezeko la joto sasa ni tishio kwa binadamu kuliko ilivyokua huko miaka ya nyuma.

    Akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa huko Poland, kiongozi wa Umoja wa mataifa kuhusu hali ya hewa, amesema kuwa mwaka huu ni miongoni mwa miaka minne yenye joto zaidi duniani.

    Wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali duniani wanatarajia kuleta mabadiliko kwa kuanza kufanyia kazi mkataba wa hali ya hewa wa ParisUmoja wa mataifa umeonya kuwa ongezeko la joto sasa ni tishio kwa binadamu kuliko ilivyokua huko miaka ya nyuma. 

    Akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa huko Poland, kiongozi wa Umoja wa mataifa kuhusu hali ya hewa, amesema kuwa mwaka huu ni miongoni mwa miaka minne yenye joto zaidi duniani.

    Wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali duniani wanatarajia kuleta mabadiliko kwa kuanza kufanyia kazi mkataba wa hali ya hewa wa Paris.

    Mkutano umeanza rasmi mapema Jumatatu, ni mkutano mkubwa wa hali ya hewa na tabia nchi kufanyika tangu ule wa Paris wa mwaka 2015.

    Wakati huo huo Benki ya dunia, imetoa dola bilioni 200 zilizoelekezwa kwa nchi zinazochukua hatua za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi kwa miaka mitano ijayo.

    mabadiliko ya hali ya hewa

    Rais wa umoja wa mataifa katika masuala ya hali ya hewa, Maria Esposa amesema kuwa jitihada za haraka zinahitajika.

    ”Tulipoanza na mkutano wa masuala ya hali ya hewa mwaka 1995, ni kama tulikua tukipanga maisha ya baadae, na tulikua tukizuia kuharibika kwa hali ya hewa, lakini sasa tunaishi ndani yake, sasa tunatakiwa tujikomboe haraka , na jamii inatakiwa ikubaliane na mabadiliko haya.

    Esponsa, amesema pia wajumbe wamekutana ili kujadili namna ya kujikomboa na mabadiliko hayo ya tabia nchi, na kuhakikisha makubaliano ya Paris yanafanyiwa kazi.

    Viongozi wanne wa umoja wa mataifa waliomaliza muda wao, na wazungumzaji wakuu kuhusu hali ya mabadiliko ya tabia nchi, walitoa tamko la kutaka jitihada za haraka kuchukuliwa ili kuzuia mabadiliko haya ya kasi.

    Wamesema kuwa hatua ndani ya miaka miwili zinaweza kupunguza janga hili.

    Wakati huohuo nchi kadhaa zimekua zikitoa tamko juu ya kuhakikisha wanapambana na mabadiliko ya tabia nchi, lakini hatua wanazochukua haziridhishi.

    Kutokana na suala hili kuwa la dharura, baadhi wa wadau walikutana mapema jana kujadili kabla kikao hakijaanza rasmi.

    Viongozi wa nchi 29 wanatarajiwa kuhudhuria , kwa upande wa China na Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kuonyesha kuwa kuna uwezekano wa ushirikiano wa pamoja hata katika kipindi hiki cha uongozi wa Donald Trump nchini Marekani.

  • Urusi yateka meli za kivita za Ukraine

    Urusi yateka meli za kivita za Ukraine

    Urusi imezishambulia na kuziteka meli tatu za kivita za Ukraine zilizokuwa baharini katika rasi ya Crimea katika kisa ambacho kimezidisha uhasama baina ya mataifa hayo mawili.

    Jeshi la wanamaji la Ukraine linaituhumu Urusi kwa kushambulia na kuharibu moja ya meli zake za kivita

    Meli mbili ndogo za kivita, pamoja na meli moja ya kusindikiza meli ndizo zilizotekwa na wanajeshi wa Urusi.

    Wahudumu kadha wa meli za Ukraine wamejeruhiwa.

    Kila taifa linamlaumu mwenzake kwa kusababisha kisa hicho.

    Leo Jumatatu, wabunge wa Ukraine wanatarajiwa kupiga kura kuidhinisha kuanza kutekelezwa kwa sheria za kijeshi.

    Mzozo wa sasa ulianza pale Urusi ilipoituhumu Ukraine kwa kuingiza meli katika maeneo yake ya bahari kinyume cha sheria.

    Urusi kisha iliweka meli kubwa ya kusafirisha mizigo na kuziba daraja la kuingia kwenye mlango wa bahari wa Kerch, njia pekee ya kuingia kwenye Bahari ya Azov na ambayo hutumiwa na mataifa yote mawili.

    Wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la Usalama na Ulinzi la Ukraine, Rais Petro Poroshenko alieleza vitendo vya Urusi kuwa “uchokozi usio na sababu na za kiwendawazimu.”

    Urusi imeomba kuandaliwe mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, mkutano ambao balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley amesema umepangiwa kufanyika saa tano asubuhi saa za New York (16:00 GMT) leo Jumatatu.

    Uhasama umekuwa ukiongezeka katika Bahari Nyeusi na Bahari ya Azov katika rasi ya Crimea, eneo lililotekwa na Urusi mwaka 2014 kutoka kwa Ukraine.

    Mzozo wa sasa umetokeaje?

    Asubuhi, meli za kivita za Berdyansk na Nikopol, pamoja na meli ya kuzisindikiza Yana Kapa, zilijaribu kusafiri mji wa bandarini kwenye Bahari Nyeusi wa Odessa kuelekea Mariupol katika Bahari ya Azov.

    Ukraine inasema Urusi ilijaribu kuzizuia meli hizo zisiendelee na safari yake, ambapo meli moja iliigonga meli ya Yana Kapa.

    Meli hizo ziliendelea na safari kuelekea mlango wa bahari wa Kerch, lakini zikapata njia imezibwa na meli moja kubwa.

    Urusi wakati huo ilikuwa imetuma ndege mbili za kivita na helikopta mbili ambazo zilikuwa zikipaa angani katika eneo hilo na kufuatilia mwenendo wa meli hizo.

    Urusi inaituhumu Ukraine kwa kuingia kinyume cha sheria katika maeneo yake ya bahari na usafiri eneo hilo umesitishwa kwa muda usiojulikana kwa sababu za kiusalama.

    Jeshi la wanamaji la Ukrane lilisema meli hizo zilikuwa zimeshambuliwa na kuharibiwa zilipokuwa zinajaribu kuondoka eneo hilo.

    Imesema wahudumu wake sita wamejeruhiwa.

    Jeshi la wanamaji la Urusi lilizizuia meli hizo za Ukraine baada ya kuzituhumu kwa kuingia kinyume cha sheria kwenye maeneo ya bahari ya Urusi

    Idara ya Usalama ya Urusi ifahamikayo kama FSM, ambayo inatekeleza mengi ya majukumu yaliyotekelezwa na KGB, ilithibitisha baadaye kwamba moja ya boti zake za kushika doria baharini ilitumia nguvu kuchukua udhibiti wa meli tatu za Ukraine.

    Lakini walisema ni mabaharia watatu pekee waliojeruhiwa.

    Ukraine imesema ilikuwa imeifahamisha Urusi kuhusu mpango wake wa kupitishia meli hizo zake eneo hilo kuelekea Mariupol.

  • Meng Hongwei: China yathibitisha inamzuia mkuu wa Interpol aliyepotea

    Meng Hongwei: China yathibitisha inamzuia mkuu wa Interpol aliyepotea

    China imethibitisha inamzuia mkuu wa Interpol aliyepotea Meng Hongwei.

    Beijing imesema alikuwa anachunguzwa na tume ya kupambana na rushwa nchini humo kwa ukiukaji wa sheria.

    Meng, ambaye pia ni naibu waziri wa wizara ya usalama wa umma China, aliarifiwa kupoeta baada ya kusafiri kutoka mji wa Lyon Ufaransa , kuliko na makao makuu ya Interpol kwenda China mnamo Septemba 25.

    Interpol imesema imepokea barua ya kujiuzulu kwake mara moja kutoka kwa ofisi ya rais.

    Familia yake Meng haijawasiliana naye tangu andoke katika makao hayo makuu ya Interpol nchini Ufaransa

    Gazeti la South China Morning Post lilikunuu taarifa zilizosema kuwa Bw Meng, 64, alipelekwa kwenda kuhojiwa nchini China.

    Haijulikani ni kwani nini alikuwa anachunguzwa na mamlaka za nidhamu au alikuwa anazuiliwa wapi.

  • LIVE UPDATES: MZIKI MENENE 2018 MOROGORO

    LIVE UPDATES: MZIKI MENENE 2018 MOROGORO

    Beka Flavour akilishambulia jukwaa la muziki mnene kinyumbani nyumbani

    SNURA ANELETA MAJANGA KWENYE JUKWAA LA MUZIKI MNENE 2018 MOROGORO

  • mtikisiko na vishindo vyaikumba 95.5 morogoro

    mtikisiko na vishindo vyaikumba 95.5 morogoro

    Mtikisiko na vishindo vya wana mazoezi wa  95.5 morogoro vyasikika mapema asubuhi ya leo

    MATUKIO KWA PICHA