Slider

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI ATEMBELEA WANANCHI BUNJU
Local News

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam Mh. Ally Hapi leo amewatembelea wananchi maeneo ya Bunju na Mbweni waliokuwa na kero mbalimbali. Katika eneo la Bunju Kilungule, baadhi ya wananchi nyumba zao zimezungukwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.  Akijibu maombi ya wananchi hao, Mheshimiwa, Hapi amewaagiza mainjinia wa manispaa kuhakikisha kuwa wanafanya utaratibu wa kupata pampu kubwa ya kuvuta maji hayo, huku akiwataka wananchi kuwa wale wote waliojenga  katika eneo hatarishi ambalo ramani inaonesha kuwa ni eneo...

Like
292
0
Thursday, 28 April 2016
RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MTENDAJI WA TIC
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC, Bi Juliet Kairuki. Kwa mujibu wa Taarifa kwa vyombo vya Habari iliyotolewa leo na kusainiwa na Katibu Mkuu, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda, Uteuzi wa Bi Kairuki umetenguliwa kuanzia April 24 mwaka huu. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, hatua hiyo imechukuliwa na Mheshimiwa Rais baada ya kupata taarifa kwamba Mkurugenzi huyo amekuwa hachukui mshahara wa Serikali tangu alipoajiriwa mwezi April...

Like
242
0
Thursday, 28 April 2016
MGOMO WA WAFANYAKAZI WAKWAMISHA SHUGHULI ZA KAWAIDA UJERUMANI
Global News

MGOMO wa  wafanyakazi  wa  sekta  ya  umma umevuruga shughuli  za  kawaida nchini  Ujerumani  hii leo. Wanachama  wa  chama  cha  wafanyakazi  wa  sekta  ya umma Verdi wamegoma  kufanya kazi  kutokana na madai  ya nyongeza ya mshahara.   Viwanja  vya  ndege  vya Frankfurt, Dusseldorf  na  Munich vimeathirika  na  mgomo  huo  ikiwa  ni  pamoja na  usafiri wa mjini katika miji  mbali  mbali,  lakini  uwanja  wa  ndege wa mjini  Berlin unafanyakazi  kama ...

Like
209
0
Wednesday, 27 April 2016
UBELGIJI YAMPELEKA UFARANSA MSHUKIWA WA PARIS
Global News

SALAH ABDESLAM , anayetuhumiwa  kuchukua  nafasi  ya juu  katika mashambulizi  ya  mjini  Paris ambayo yamesababisha  watu  130  kuuwawa, anafikishwa mahakamani  nchini  Ufaransa  leo, kwa mtazamo  wa kuwekwa  chini  ya  uchunguzi  rasmi.   Hatua  hiyo inakuja  baada  ya  Abdeslam  kupelekwa nchini  Ufaransa  kutoka  Ubelgiji  mapema  leo Jumatano. Mtuhumiwa  huyo  aliwasili  nchini  Ufaransa  mapema  leo...

Like
181
0
Wednesday, 27 April 2016
VODACOM YACHANGIA ASILIMIA 2% YA PATO LA TAIFA 2012/2015
Local News

IMEBAINISHWA kuwa kwa mwaka 2012/2015 kampuni ya  simu za mkononi ya Vodacom imechangia zaidi ya  shilingi bilioni 3  katika  pato la taifa ambayo ni sawa na asilimia 2 ya pato la Tanzania. Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam katika   tathmini iliyofanywa na  KPMG juu ya mchango mpana wa kiuchumi na kijamii ikiwamo ukuzaji wa uchumi,ajira,na kupunguza umaskini,tathmini iliyofanyika kuhusu mtaji na shughuli za uwekezaji kwa kipindi cha mwaka wa fedha  wa  2012/...

Like
243
0
Wednesday, 27 April 2016
RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MAAFISA TAWALA WAPYA 10 LEO
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli,  amewaapisha Maafisa Tawala wapya kumi aliowateua April 25, mwaka huu na kuwapangia vituo vyao vya kazi. Makatibu Tawala hao wapya, wameapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam na kuweka saini ya ahadi ya uadilifu kwa Viongozi wa Umma, Zoezi lililoendeshwa na kamishna wa maadili Sekretarieti ya maadili ya Viongozi wa Umma, Mheshimiwa Jaji Salome Kaganda mbele ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John...

Like
241
0
Wednesday, 27 April 2016
ALFRED LUCAS ATEULIWA KUWA AFISA HABARI MPYA TFF
Slider

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Alfred Lucas kuwa Afisa Habari na Mawasiliano mpya wa shirikisho kuanzaia leo Aprili 27, 2016. Alfred anachukua nafasi ya Baraka Kizuguto aliyehamishiwa katika Kurugenzi ya Mashindano kuwa Afisa Mashindano na Meneja wa Mifumo pepe ya Usajili (TMS). Alfred ana uzoefu kutoka vyombo mbalimbali alivyovitumikia kama mwandishi wa habari na mhariri.Kadhalika Alfred kitaaluma amesomea uandishi wa habari, uhusiano wa kimataifa na diplomasia pamoja na...

Like
275
0
Wednesday, 27 April 2016
TAIFA STARS KUIVAA HARAMBEE STARS
Slider

Timu ya Taifa ya Tanzania inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na timu ya Taifa Kenya Mei 29, jijini Nairobi. Mchezo huo utachezwa jijini Nairobi Mei, 29 mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kwa timu zote mbili kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika mwezi Juni, 2016 ambapo Taifa Stars itacheza dhidi ya Misri Juni 04, mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. TFF kwa kushirkiana na FKF zimekubaliana kuwepo kwa...

Like
224
0
Wednesday, 27 April 2016
TRUMP APETA MAJIMBO MATANO MUHIMU MAREKANI
Global News

NCHINI Marekani, tajiri Donald Trump amesema kuwa anajihisi sasa kama mgombea mteule wa urais wa chama cha Republican. Amesema hayo alipokuwa akiwahutubia wafuasi wake baada ya vyombo vya habari kutangaza kuwa amepata ushindi katika majimbo yote matano kaskazini mashariki mwa Marekani. Katika shughuli za upigaji kura wa mchujo kwenye majimbo hayo, mtafuta nafasi katika chama cha Democratic Bi Hillary Clinton alimpiku muwaniaji mwenzake Bernie Sanders, ambaye alishinda katika jimbo moja tu la Rhode...

Like
272
0
Wednesday, 27 April 2016
WATU KUFANYA KAZI SIKU MBILI KWA WIKI VENEZUELA
Global News

SERIKALI ya Venezuela imebuni mikakati ambayo itapelekea wafanyakazi wapatao milioni mbili wa serikali, kufanya kazi kwa siku mbili pekee kwa wiki katika kipindi cha majuma mawili. Hatua hii inalenga kusaidia kukabiliana na uhaba wa umeme ambao unayumbayumba nchini humo. Wafanyakazi hao wa umma na wale wanaofanya kazi katika sekta zinazomilikiwa na serikali watafika kazini siku za Jumatatu na Jumanne pekee hadi matatizo hayo ya nguvu za umeme...

Like
229
0
Wednesday, 27 April 2016
MARA: WANANCHI WATAKIWA KUSHIRIKI KUCHANGIA MAENDELEO
Local News

WANANCHI katika halmashauri zote  mkoani mara wametakiwa kushiriki katika kuchAngia maendeleo na kuachana na dhana zinazoendelezwa na baadhi ya  viongozi katika serikali wanaotoa kauli zakuwapinga wananchi kuchangia maendeleo ya elimu na kulitumia vibaya neno Elimu bure. Yamesemwa hayo na mwenyekiti wa halmashauri ya BUTIAMA Magina Magesa alipokuwa akizungumza katika uhamasishaji wa kuchangia maendeleo ya elimu hususani ujenzi wa maaabara na madawati katika wilaya hiyo ....

Like
237
0
Wednesday, 27 April 2016