Slider

KONGAMANO LA UWEKEZAJI KATI YA WATANZANIA NA WARUSI KUFANYIKA IJUMAA WIKI HII
Local News

KITUO cha Uwekezaji Tanzania –TIC, kwakushirikiana na Russian Export Club kimeandaa Kongamano la Uwekezaji kati ya Watanzania na Warusi litakalofanyika siku ya Ijumaa katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.   Mbali na TIC kongamano hilo limeandaliwa pia kwa ushirikiano na Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi na Ubalozi wa Urusi nchini Tanzania, kwa usimamizi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji nchini Tanzania, Wizara ya Biashara na Viwanda ya Urusi na...

Like
208
0
Wednesday, 27 April 2016
AL SHABAAB ALIYEJIUNGA NA IS ANASWA SOMALIA
Global News

KAMANDA wa kundi la al-Shabaab aliyejiunga na kundi linalojiita Islamic State nchini Somalia amekamatwa na maafisa wa usalama nchini humo.   Hassan Mohamed Siad ambaye pia hujulikana kama Hassan Fanah alikamatwa jana Jumapili baada ya maafisa wa ujasusi wa Somalia kufanya operesheni katika nyumba moja mtaa wa Kahda.   Vyombo ya habari nchini Somalia vinasema alikuwa anajificha katika mtaa huo kutoka wa wapiganaji wa al-Shabab. Serikali ya Somalia ilikuwa imeahidi zawadi ya $2,000 kwa mtu ambaye angetoa habari za kusaidia kukamatwa...

Like
197
0
Monday, 25 April 2016
ICC YAANZISHA UCHUNGUZI WA AWALI KUHUSU MAUAJI YA BURUNDI
Global News

MWENDESHA mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) amesema mahakama hiyo imeanzisha uchunguzi wa awali kuhusu mauaji ambayo yamekuwa yakitokea nchini Burundi.   Bi Fatou Bensouda amesema amekuwa akifuatilia kwa karibu matukio ya Burundi tangu Aprili 2015 na kwamba mara kwa mara amezitaka pande zote husika kutojihusisha na ghasia na mauaji.   Watu 430 wameuawa na wengine 3,400 kukamatwa tangu kuanza kwa machafuko Aprili mwaka...

Like
208
0
Monday, 25 April 2016
MTOTO WA MWAKA MMOJA APOTEZA MAISHA BAADA YA KUTUMBUKIA SHIMONI
Local News

MTOTO mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi na moja aliye tambulika kwa jina la  Waziri Kashinje amefariki dunia baada ya kutumbukia katika shimo la maji wakati akicheza na wenzake katika nyumba ya jirani yao eneo la igoma Jijini Mwanza.   Akizungumza na E Fm katika eneo la tukio mjumbe wa serikali ya mtaa huo Amosi Shirangi amesema tukio hilo limetokea wakati mtoto huyo alipokuwa akicheza na wenzake lililopo katika nyumba ya jirani.   Nao Wazazi wa mtoto huyo Kashinje...

Like
299
0
Monday, 25 April 2016
RAIS WA MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA 26 YA TANZANIA BARA
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli, leo amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania bara. Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa kati ya Makatibu tawala hao 10 ni wapya, wawili wamebadilishiwa vituo na 13 wamebakishwa katika vituo vyao vya sasa. Makatibu tawala wa Mikoa 10 ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza, wataapishwa siku ya Jumatano April 27, Ikulu saa tatu...

Like
268
0
Monday, 25 April 2016
WENGER AONYESHA HOFU EPL
Slider

Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema ameanza kuingiwa na wasiwasi kuhusu Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu. Anasema wasiwasi zaidi unatokana na hatari ya klabu hiyo kushindwa kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza katika miaka 19. The Gunners walipoteza nafasi ya kupanda hadi nambari tatu kwenye jedwali baada ya kutoka sare tasa na Sunderland ugenini Jumapili. “Tuna haja sana na hilo na tuna wasiwasi kuhusu hilo kwa sababu sasa yatakuwa ni mapambano,” alisema...

Like
216
0
Monday, 25 April 2016
MAREKANI KUPELEKA MAJESHI SYRIA
Global News

MAAFISA wakuu nchini Marekani wanasema kuwa Rais Barack Obama atatuma wanajeshi wa ziada wapatao 250 nchini Syria, ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na vikosi vya ndani vya nchi hiyo, katika kupambana na wapiganaji wa Islamic State. Kwa mujibu wa maafisa hao, lengo hasa ni kuwasajili waarabu wa dhehebu la Sunni kuungana na wapiganaji wa kikurdi waliopo kaskazini mashariki mwa Syria. Hata hivyo vikosi hivyo vya Marekani havitawajibika moja kwa moja katika mapambano...

Like
276
0
Monday, 25 April 2016
WAPINZANI WA TRUMP WAUNGANISHA NGUVU KUMZUIA
Local News

WAPINZANI wawili wakuu wa Donald Trump katika kinyang’anyiro cha kumteua mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani wametangaza mipango ya kuungana kukabiliana na mgombea huyo. Ted Cruz na John Kasich wanataka kushirikiana kupunguza uwezekano wa mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York kushinda mchujo katika majimbo zaidi. Cruz, ambaye ni seneta wa jimbo la Texas, amesema atapunguza kampeni zake katika majimbo ya Oregon na New Mexico, Kwa upande wake John Kasich, ambaye ni gavana wa Ohio, naye amesema atamwachia Cruz katika...

Like
244
0
Monday, 25 April 2016
WANANCHI KUNUFAIKA NA UVUVI KWENYE BWAWA LA MTERA
Local News

WANANCHI wanaoishi kando ya bwawa la mtera mkoani Iringa wataendelea kunufaika na shughuli za uvuvi kutokana na bwawa hilo kujaa maji. Wakizungumzia kujaa huko kwa maji baadhi ya Wavuvi wamesema hali ya uchumi wao imeanza kutengemaa tofauti na ilivyokuwa awali kwa kuwa Samaki wameanza kupatikana kwa wingi. Nao wafanyabiashara wa Samaki wamesema bei ya samaki inaendelea kushuka kutokana na Samaki kupatikana kwa...

Like
488
0
Monday, 25 April 2016
SUDAN KUSINI: MATAIFA YENYE NGUVU YATAKA MACHAR AREJEE JUBA
Global News

MATAIFA makuu duniani yamewapa muda viongozi wa pande zinazohasimiana nchini Sudan Kusini kuhakikisha wanakubaliana na kuhakikisha kiongozi wa zamani wa waasi Riek Machar anarejea Juba ifikapo kesho. Mataifa hayo yamesema kuwa wakishindwa kukubaliana, makubalianao ya amani yaliyolengwa kumaliza miaka miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe yatavunjika. Siku ya Jumamosi April 23 imewekwa na wawakilishi wa  halmashauri ya JMEC iliyoundwa na Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya, China, Uengereza, Norway na Marekani ambapo Sudan Kusini ni mwanachama wa...

Like
248
0
Friday, 22 April 2016
MAREKANI: IDADI YA WATU WANAOJIUA YAONGEZEKA
Global News

TAKWIMU rasmi za serikali zinaonesha idadi ya watu wanaojiua nchini Marekani imeongezeka kwa kiasi kikubwa. Takwimu hizo kutoka Kituo cha Taifa cha Takwimu za Afya zinaonyesha kuwa viwango vya watu kujiua vimeongezeka kwa karibu asilimia 25 katika kipindi cha miaka 15 iliyopita. Utafiti huo uliofanyika kwa jinsia zote umeonesha kwamba viwango vya wanawake kujiua ndivyo vilivyoongezeka zaidi, vikipanda kwa asilimia 36 vikiwahusisha zaidi wanawake wa umri wa makamo.                        ...

Like
284
0
Friday, 22 April 2016