Category: Slider

  • SASA SUGU HURU !

    SASA SUGU HURU !

    Mbeya. Viongozi wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti, Freeman Mbowe waliokwenda Gereza Kuu la Ruanda mkoani Mbeya kuwalaki Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga wamepigwa butwaa baada ya kuelezwa na askari magereza kwamba wameshatoka.
    Wakiwa nje ya gereza leo Mei 10, 2018, viongozi hao walifuatwa na askari na kuelezwa kwamba wawili hao wameshatoka.
    Magari mawili ya polisi yaliyokuwa yameimarisha ulinzi gerezani hapo nayo yaliondoka.
    Happiness Msonge, mkewe Sugu akizungumza na MCL Digital amesema walipigiwa simu na kuelezwa kwamba wameshatoka na wako njiani wakielekea nyumbani.
    Baadhi ya viongozi waliokuwepo ni mbunge wa Viti Maalumu, Sophia Mwakagenda, Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi na madiwani.
    Viongozi hao walianza kufika gerezani leo Mei 10, 2018 saa 12:45 asubuhi na kuingia ndani ya uzio wa gereza ambako askari waliwaondoa.
    Sugu na Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela Februari 26 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desemba 30 mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.
    Wawili hao wameshatumikia adhabu hiyo kwa siku 73 ikiwa ni zaidi ya robo ya kifungo chao

  • SIRRO CUP KUANZA KUTIMUA KIBITI

    SIRRO CUP KUANZA KUTIMUA KIBITI

    Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akimkabidhi mpira mmoja wa Viongozi wa timu zinazoshiriki mashindano ya Sirro Kibiti mwaka 2018 katika uwanja wa Samora Kibiti wakati wa uzinduzi wa michezo hiyo uliofanyika jana. Mashindano hayo yanashirikisha timu 16 kutoka Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji.
    Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Migomba kutoka Wilayani Rufiji wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Sirro Kibiti mwaka 2018 katika uwanja wa Samora Kibiti. Mashindano hayo yanashirikisha timu 16 kutoka Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji.
    Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwasalimu wakazi wa Kibiti wakati wa Sherehe za ufunguzi wa mashindano ya Sirro Kibiti mwaka 2018 katika uwanja wa Samora Kibiti. Mashindano yanayoshirikisha timu 16 kutoka Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji.

     

     

     

     

  • Zuckerberg akiri kosa lake na kuomba radhi

    Zuckerberg akiri kosa lake na kuomba radhi

    Mkurugenzi Mtendaji wa Facebook Mark Zuckerberg ametoa maelezo katika Bunge la Marekani- Congress kwa mara ya kwanza Jumanne, akijibu wasiwasi ulioelezwa na wabunge juu ya kushindwa kwa mtandao wa jamii maarufu kulinda taarifa zao.
    Taarifa hizo za siri za watumiaji wanaofikia milioni 87 ulimwenguni zilizotumiwa na kampuni yenye kujishughulisha na siasa- Cambridge Analytica iliyokuwa na mafungamano na Trump.

    Mahojiano hayo yanaendelea Jumatano wakati Zuckerberg atakapokutana katika raundi ya pili kujibu maswali mbele ya jopo la Wabunge wa Marekani.

    Mkurugenzi huyo Mark Zuckerberg amekiri kuwa :”Hilo lilikuwa kosa kubwa na ni kosa langu mimi mwenyewe na naomba radhi. Nilianzisha matandao wa Facebook, niliusimamia na nina wajibika kwa kitu chochote kinachotokea.”

    Wachambuzi wanasema ni kosa ambalo liliruhusu kampuni ya kisiasa ya Cambridge Analytica kupata taarifa kwa kupitia programu iliyotengenezwa na kampuni nyingine, ambayo ili ingilia taarifa binafsi za mamilioni ya wanaotumia Facebook duniani.

    Marc Rotenberg wa kituo cha kutunza taarifa za siri za kielektroniki amesema: “Ni suala nyeti kwa Facebook kwa njia nyingi. Kuhakikisha bei ya hisa zao zinanyanyuka, watu wana wasiwasi mkubwa juu ya mustakbali wa kampuni hiyo. Lakini nafikiri vipi Facebook itaweza kuendelea kufanya shughuli zake kama ilivyo kwani ni suala la wazi. Nafikiri mjini Washington na maeneo mengine, utashuhudia shinikizo la kuwepo mabadiliko ya kweli.

    Mabadiliko yaliyoanza katika mahojiano yasiyo ya kawaida kabisa yakiendeshwa na nusu ya Baraza la Seneti ya Marekani.

    Seneta Richard Durbin (Mdemokrati) alimuuliza Zuckerberg: “Je, uko radhi kutuambia jina la hoteli uliofikia jana usiku?” “Um, uh, hapana,” alijibu Zuckerberg.

    Seneta Durbin : “Kama ulituma ujumbe kwa mtu yoyote wiki hii, unaweza kutujulisha majina ya watu hao uliowasiliana nao?’

    “Seneta, hapana, pengine sitopendelea kufanya hivyo hadharani hapa,” alijibu mkurugenzi huyo wa Facebook.

    “Nafikiri pengine hilo ndio suala zima. Haki yako ya kutoingiliwa maisha yako binafsi.”

    Hata hivyo Zuckerberg ameahidi mabadiliko. Amesema iwapo tutagundua kuwa mtu yoyote alitumia taarifa za watu kinyume cha utaratibu, tuta wafungia kutumia Facebook na kumfahamisha kila aliyeathirika.”

    Baadhi ya maseneta wamesema kuwa kuongeza uwazi katika mitandao ya jamii lazima iwe ni hatua ya pili baada ya hapa.

    “Mmarekani wa hali ya kati hajui chochote pale mitandao inapowapeleka, umeona misamiati na masharti yaliyopo Facebook, mimi ni wakili, lakini sikuweza hata kufahamu maelezo ya ibara ya kwanza.”

    Pamoja na kuwa baadhi ya maseneta wanatambua Facebook inahitaji kuwa na mfumo wa kibiashara unaoingiza kipato kwa kutumia taarifa za watu binafsi kwa ajili ya kuwavutia watangazaji.

    “Hakuna kitu kilichokuwa bure katika maisha, kila kitu kinahusisha biashara, iwapo unafikiri unataka kitu bila ya kulipia.”

    Mahojiano ya Zuckerberg na Bunge la Marekani limeibua mazungumzo.

    “Je, utawafiki sheria ambayo itakutaka uwafahamishe watumiaji wa mitandao ya jamii kunapotokea uvunjifu wa sheria katika kipindi cha saa 72,” aliuliza Seneta Amy Klobuchar (Mdemokrati). Zuckerberg amejibu kuwa jambo hilo linafaa.

  • Marekani inapima hatua za kujibu shambulio ‘kemikali nchini Syria

    Marekani inapima hatua za kujibu shambulio ‘kemikali nchini Syria

    Marekani inasema kuwa “tayari ana maamuzi mengi” za kujibu shambulio linaloshukiwa kuwa la kikemikali nchini Syria, huku viongozi wa magharibi wakiendelea kupima hatua za kijeshi.
    Msemaji wa Ikulu ya White House Sarah Sanders amewaambia wandishi wa habari kuwa hakuna ushahidi wa mwisho uliokwisha chukuliwa juu ya mashambulio ya kijeshi.
    Lakini amesema Marekani inaziwajibisha Urusi na Syria kwa tukio hilo.

    Baraza la Kitaifa la Usalama la Marekani litakutana Alhamisi, huku waziri mkuu wa Uingereza PM Theresa May akiitisha mkutano wa baraza la mawaziri kujadili tukio hilo la Syria.
    Wanaharakati, wahudumu wa uokozi na madaktari wanasema makumi ya watu walikufa katika mji unaodhibitiwa na waasi wa Douma Jumamosi.

  • Gavana atuhumiwa kwa ubakaji DRC

    Gavana atuhumiwa kwa ubakaji DRC

    Naibu Gavana wa jimbo la Ikweta kusini magharibu nchini Jamuhuri ya demokrasia ya Kongo ,Tathy Bikamba ameshtakiwa kwa tuhuma za ubakaji wa binti wa miaka 20 ambaye inadaiwa kuwa alimfanyia unyama huo baada ya kumpa dawa za kulevya.

    Gavana huyo anatarajiwa kufikishwa kinshasa kujibu tuhuma hizo mahakamani , ingawa wakili wake ametupia mbali tuhuma hizo.
    Taarifa kutoka duru za karibu za uchunguzi wa kesi hiyo ya kubaka vinasema kwamba gavana huyo alimbaka binti huyo siku ya Jumamosi.
    Bwana Bikamba ambaye kwa sasa yuko gerezani anatarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo ili aweze kujibu mashtaka yake ya kumwekea dawa ya kulevywa na kumfanyia tendo la ngono binti bila idhaa yake.
    Wakili wa gavana huyo, Imbambo Engulu ametupilia mbali tuhuma hizo na kushutumu mahakama ya jimbo hilo kwa kumzuia gavana huyo bila kujali na cheo chake
    “Kushikwa kwake ni kama uonevu, tuliomba wamuzuie kwanza nyumba kwake badala ya kumuweka gerezani moja kwa moja, majaji hawakukubali ombi letu, Nawambia kweli kuwa gavana hakufanya kitendo hicho, ni uongo.”
    Waziri wa sheria ,Faida mwangiliwa ambaye pia ni miongoni mwa wanaharati wa haki za wanawake ameomba sheria kumhukumu vikali gavana huyo ikiwa tuhuma hizo zitathbitishwa na mahakama

    Kesi za ubakaji zimeripotiwa nyingi nchini jamuhuri ya kidemokrasi ya kongo, idadi kubwa ya kesi imefanywa na waasi na wanajeshi wa taifa husuan mashariki mwa DRC.
    Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya kongo tayari kuathibu vikali askari kadhaa na maafisa wa jeshi la Kongo wengi kwa kuwapa kifungo cha maisha .

  • WAKILI ALIYEMUAPISHA RAILA ODINGA AZUHIRIWA UWANJA WA NDEGE

    WAKILI ALIYEMUAPISHA RAILA ODINGA AZUHIRIWA UWANJA WA NDEGE

    Bw Miguna

    Wakili wa upinzani aliyeidhinisha kiapo cha Bw Raila Odinga alipokuwa anajiapisha kuwa ‘Rais wa Wananchi’ mwezi Januari bado amekwama katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta, Nairobi.

    Bw Miguna Miguna alijaribu kurejea Kenya Jumatatu lakini akazuiwa kuingia baada yake kudaiwa kutowasilisha pasipoti ya Canada ambayo ilitumiwa kumsafirisha kwa nguvu hadi Canada.

    Wakili huyo alisisitiza kwamba ni raia wa Kenya na hafai kuzuiwa kurejea.

    Taarifa zinasema Bw Miguna, ambaye pasipoti yake ya Kenya ilitwaliwa na polisi kabla ya kuondolewa kwake Kenya mwezi jana, alikuwa ametakiwa kuwasilisha ombi la kupata visa ya kukaa Kenya kwa miezi sita kwa kutumia pasipoti hiyo yake ya Canada.

    Alikataa jaribio hilo na badala yake kutoa kitambulisho chake cha taifa kuonesha kwamba yeye ni Mkenya na kutaka aruhusiwe kuingia.

    Bw Miguna, aliyekuwa amewasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mwendo wa saa nane adhuhuri, alikesha kwenye uwanja huo.

    Maafisa walijaribu kumsafirisha kutoka uwanja huo kwa kutumia ndege ya shirika la Emirates ambayo ilikuwa inaelekea Canada kupitia Dubai.

    Wakili wa upinzani James Orengo, seneta ambaye majuzi alichaguliwa kuwa kiongozi wa upinzani Bunge la Seneti, ameambia Reuters kwamba maafisa wa polisi waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia ndio waliojaribu kumlazimisha Bw Miguna kupanda ndege hiyo iliyokuwa inaondoka.

    Lakini wakili huyo alikataa kuingia ndani ya ndege hiyo na mtafaruku ukazuka.

    Video iliyopeperushwa moja kwa moja na runinga ya kibinafsi ya Citizen ilimuonesha Bw Miguna akiwa kwenye lango la ndege akiwaambia wahudumu: “Siendi popote, hamuwezi kuniondoa kutoka kwa nchi yangu kwa nguvu.”

    Bw Orengo ameambia Reuters kwamba maafisa hao wa polisi baadaye walimuondoa mwanasiasa huyo kutoka kwenye ndege hiyo na kumzuilia kwa muda katika afisi za uhamiaji katika uwanja huo wa JKIA.

    Baadaye asubuhi, walimhamishia kituo cha polisi cha uwanja huo na kuendelea kumzuilia.

    Bw Odinga alikuwa amefika uwanjani humo Jumatatu usiku kujaribu kutatua mzozo huo.

    Kwa mujibu wa Bw Orengo, Bw Odinga alikuwa ametoa wito kwa serikali kumrejeshea Miguna pasipoti yake ya Kenya.

    Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Uhamiaji mapema Jumanne ilisema Bw Miguna alianza “kuzua fujo na kulalamika” uwanja wa ndege na kwamba alikuwa anataka kuruhusiwa kuingia Kenya bila kuidhinishwa na maafisa wa uhamiaji.

    Wizara hiyo imesema inafanikisha utaratibu wa kumuwezesha Bw Miguna kuwasilisha tena ombi la kuwa raia wa Kenya.

    Taarifa ya wizara hiyo ilisema fomu za kuwasilisha maombi hayo zimetumwa uwanja wa Ndege.

    Mkurugenzi wa Idara ya Uhamiaji Joseph Munywoki kwenye taarifa alisema: “Badala ya kuonesha hati za kusafiria alizotumia kwenda Canada, Miguna alianza kuzua fujo na kulalamika akisema kwamba yeye ni Mkenya na anafaa kuruhusiwa kuingia Kenya bila kupitia kwa meza ya idara ya uhamiaji kama inavyotakiwa kwa abiria wote wanaowasili bila kujali uraia wao.”

    “Hatujamzuia kuingia Kenya, tunamtaka tu afuate utaratibu kama watu wengine wote,” msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani

    Mwenda Njoka aliambia Reuters kwa njia ya simu

     

  • MICHAEL PETTER MSHINDI WA SHIKA NDINGA 2017

    MICHAEL PETTER MSHINDI WA SHIKA NDINGA 2017

    Michael Petter

    Michael Petter ambae ni mshiriki na mshindi wa #ShikaNdinga2017 akitoa mrejesho wa maisha yake ya biashara baada ya ushindi.

  • LADHANI LEO, 26 March

    LADHANI LEO, 26 March

    Professor Jay ndani ya Nyumba

    Professor Jay: Naamini basata ni wazazi na walezi wa muziki

    Professor Jay: Niliposikia nyimbo zinafungiwa nilishtuka, nafikili basata wanatakiwa kukaa na vijana kuweza kuwaelekeza

    Professor Jay: Kwa dunia ilivyo sasa sidhani hizi contents za kawaida sana sioni kama shida

    Professor Jay: Kweli tunaitji kujitune kufuata utamaduni wetu lakini tuliangalie hili

    Professor Jay: Unapoongelea serikali ni chombo kikubwa sana, na hata baraza la sanaa ni kama mzazi.

    Professor Jay: Kulidharau baraza la Sanaa si vizuri, kinachotakiwa ni kukaa na baraza na kuongea nayo

    Professor Jay:Yaha ni kweli vijana  wanakosea, na sisi ni kama kolodoza, tumechonga barabara haawa madogo wanapita kwenye njia imenyooshwa

    Professor Jay: Pagamisa ni neno la kizuru maana yake pukutisha, au usikate tamaa

    Professor Jay: Lengo la huu wimo ni kuwapa funzo vijana, wasikate tamaa, wapambane mpaka kieleweke

    Professor Jay: Unajua mimi  sasa ni mwanasiasa so siku hizi nikishasema wadau watasema mimi nasema kwa ajili ya upande wa chama

    Professor Jay: wimbo huu target yangu ni kuwini market ya umri wote, wale kitambo, na wasasa

    Professor Jay:  Video ya Pagamisa imeshatoka inapatika kwenye chanel yangu ya Youtube

     

     

  • POLISI YAKAGUA MAGARI YA WAFANYAKAZI EFM

    POLISI YAKAGUA MAGARI YA WAFANYAKAZI EFM

    Kikosi cha Usalama barabarani kikiongozwa na Kamanda J.T.Gwau kilifika ofisi za Efm redio Pamoja na tve kwa ajili ya kutoa elimu juu ya Usalama barabarani pamoja na Ukaguzi wa Magari ya Wafanyakazi wake. Ikiwa ni pamoja na Ubandikaji wa stika za siku ya Nenda kwa Usalama barabarani.

    Zoezi hilo lilikwenda vizuri bila matatatizo yoyote, wafanyakazi wa EFM Redio pamoja na TV E wamelishukuru Jeshi la Polisi kwa kuwapatia elimu hiyo, na kuhadi wataitumia vizuri pindi wawepo barabarni ili kupunguza ajali.

  • MAKONDA KUWAITA WALIOACHWA NA WAUME ZAO OFISI KWAKE

    MAKONDA KUWAITA WALIOACHWA NA WAUME ZAO OFISI KWAKE

    MKUU wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewataka wanawake wote waliotelekezwa na waume zao na hawapatiwi fedha za matunzo ya mtoto wafike ofisini Jumatatu ya Aprili 9 kwa lengo la kupatiwa msaada wa kisheria.

    Taarifa ya Makonda kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana amesema jopo la wataalamu wa sheria, maofisa ustawi wa jamii na askari Polisi kutoka dawati la jinsia wamejipanga ipasavyo kuwahudumia na kuhakikisha mzazi mwenza anatoa fedha kwa ajili ya matunzo ya mtoto.

    “Huduma hii inatolewa bure chini ya uongozi thabiti wa Serikali ya Awamu ya Tano.Ewe mwanamke huu si wakati wa kulia wala kuteseka kwani Serikali yako itasimama na wewe hadi upate haki yako,” amesema Makonda.