Slider

ALIYEITEKA NDEGE YA MISRI AKAMATWA
Global News

RIPOTI zimesema kuwa mtekaji wa ndege ya EgyptAir amedai kuwa anahitaji kuongea na mkewe waliyetengana naye anayeishi Cyprus ambaye kwa sasa anadaiwa kuelekea katika uwanja huo wa ndege. Rais wa Cyprus NicosAnastasiades amewaambia waandishi wa habari kwamba tukio hilo la utekaji nyara halikuwa la kigaidi na kwamba wanahakikisha kuwa kila mtu anaachiliwa akiwa salama. Shirika la habari la Cyprus-CYBC limesema kuwa mtekaji huyo huenda alikuwa na malengo yake...

Like
183
0
Tuesday, 29 March 2016
MAKONDA AKABIDHIWA OFISI RASMI DARESALAAM
Local News

ALIYEKUWA mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick leo amemkabidhi rasmi ofisi mkuu wa mkoa mpya wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda ambapo amemuomba Mkuu huyo mpya wa mkoa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo afya na elimu. Akizungumza mbele ya maofisa na watendaji mbalimbali ambao wamejitokeza kwa ajili ya kushuhudia makabidhiano hayo Mheshimiwa Sadick amesema licha ya yeye kufanya kazi kwa mafanikio bado kuna changamoto ambazo anaamini kutokana na uzoefu alionao mkuu huyo wa mkoa...

Like
218
0
Tuesday, 29 March 2016
SUMATRA NA JESHI LA POLISI WAKAMATA AMABASI 105 NA 36 YAFIKISHWA MAHAKAMANI
Local News

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani wamefanya ukaguzi katika Jiji la Dar es salaam na kufanikiwa kukamata mabasi  105 na kati hayo 36 yamefikishwa mahakamani  baada ya kukiuka masharti ya leseni ya usafirishaji abiria.   Hayo yamebainishwa leo na Meneja Mawasiliano wa SUMATRA David Mziray wakati wa mkutano na vyombo vya habari uliolenga kutoa ufafanuzi kuhusu hatua zinazochukuliwa na Mamlaka hiyo katika kutatua kero zinazowakabili...

Like
221
0
Tuesday, 29 March 2016
MIKAKATI YA MOURINHO KUIBORESHA MAN UNTD
Global News

Meneja wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho anadaiwa kuanza kujipanga na Manchester United kama atachukua nafasi ya Louis van Gaal. Kwa mujibu wa jarida la Don Balonna Mourinho anataka kusajili nyota watatu. Kocha huyo ameshaanza mipango ya usajili kwa kuweka wachezaji kadhaa nyota katika orodha yake akiwemo mshambuliaji wa Napoli Gonzalo Higuain, kiungo wa Real Madrid James Rodriguez na mshambuliaji wa Juventus Alvaro Morata. Mourinho ameshawahi kufanya kazi na Higuain wakati akiwa Madrid na United wameonyesha kuwa tayari ingawa watalazimika...

Like
225
0
Tuesday, 29 March 2016
MAREKANI YAIFUNGUA IPHONE YA MLIPUAJI
Global News

WIZARA ya Sheria ya Marekani imesema imefanikiwa kuzisoma data zilizohifadhiwa kwenye Simu ya iPhone, mali ya mmoja wa walipuaji katika tukio la mauaji la San Bernardino na kutangaza kuacha mpango wake wa kisheria dhidi ya Kampuni ya Apple. Wakili wa Marekani Eileen Decker amesema kuna mtu aliisaidia idara hiyo kuifungua Simu hiyo ya iPhone bila kuathiri data zilizohifadhiwa. Simu hiyo ni mali ya Rizwan Farook ambaye pamoja na mke wake wanatuhumiwa kuwaua watu kumi na nne kusini mwa California Desemba...

Like
223
0
Tuesday, 29 March 2016
NDEGE YA MISRI ILIYOTEKWA NYARA YATUA CYPRUS
Global News

NDEGE ya Misri iliyotekwa nyara imefanikiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Larnaca nchini Cyprus. Taarifa za uchunguzi kutoka kwenye ndege hiyo zimeeleza kuwa ndege hiyo ya abiria iliyokuwa ikisafiri kutoka mjini Alexandria kuelekea Cairo ilitekwa nyara na watu waliojihami. Msemaji wa shirika la ndege la Misri amenukuliwa akisema kwamba Watekaji hao waliiamrisha ndege hiyo kutua Cyprus baada ya...

Like
231
0
Tuesday, 29 March 2016
MKURUGENZI HALMASHAURI YA WILAYA YA ITILIMA ASIMAMISHWA KAZI
Local News

MKURUGENZI wa Halmashauri ya wilaya ya Itilima mkoani Simiyu John Aloyce amesimamishwa kazi kwa tuhuma za kushindwa kuisimamia halmashauri hiyo na kusababisha kuwepo kwa migogoro kati ya madiwani na watendaji. Uamuzi huo umechukuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka katika kikao cha dharura cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo. Mbali na uamuzi huo Mtaka amefuta posho zote kwa wakuu wa Idara na vitengo katika halmashauri zote zilizopo mkoani hapo wanaoingia katika vikao vya madiwani...

Like
375
0
Tuesday, 29 March 2016
RAIS MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA CAG
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa dokta John pombe Magufuli, jana amepokea taarifa ya ukaguzi wa hesabu za serikali kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu Jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu Rais Magufuli amepokea taarifa hiyo yenye ripoti tano, ikiwa ni utaratibu wa kikatiba unaomtaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kukabidhi kwa Rais taarifa ya ukaguzi kabla ya mwisho wa mwezi Machi....

Like
224
0
Tuesday, 29 March 2016
MCHINA AKIRI KUIBA SIRI ZA MAREKANI
Global News

MWANAMUME mmoja kutoka Uchina amekiri kuhusika katika njama ya kuiba siri kuu kuhusu mifumo ya kijeshi ya Marekani. Su Bin anaaminika kuwa kwenye kundi la watu ambao wamekuwa wakiiba habari kuhusu ndege za kivita, ndege za kubeba mizigo na silaha. Bw Su, mwenye umri wa miaka 50, alikiri kufanya kazi na watu wawili kutoka Uchina kati ya Oktoba 2008 na Machi 2014 kudukua mifumo ya kompyuta ya Marekani, ikiwemo kampuni ya Boeing inayotumiwa na jeshi la Marekani kuunda ndege...

Like
279
0
Thursday, 24 March 2016
MSHUKIWA WA BRUSSELS ALIUNDA MABOMU YA PARIS
Global News

MAAFISA wa Ufaransa na Ubelgiji wanasema mmoja wa walipuaji wa kujitoa mhanga waliotekeleza mashambulio ya Brussels alikuwa mtaalamu wa kutengeneza mabomu. Wamesema mshukiwa huyo alihusika katika kuunda mabomu yaliyotumiwa kutekeleza mashambulio ya Paris Novemba mwaka jana na kusababisha vifo vya watu 130.   Wakizungumza, bila kutaka kunukuliwa, maafisa hao walisema chembe nasaba za DNA za mshukiwa huyo Najim Laachraoui zilipatikana katika mikanda ya kujilipua iliyotumiwa...

Like
238
0
Thursday, 24 March 2016
MIONGOZO RAHISI YA USIMAMIZI WA MISITU YAZINDULIWA
Local News

MRADI wa MAMA MISITU kwa kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali wamezindua miongozo rahisi ya usimamizi shirikishi wa misitu kwa jamii, vijiji na kwa pamoja. Akizungumza na waandishi wa Habari katika uzinduzi huo, Meneja Mradi wa MAMA MISITU Gwamaka Mwakyanjala amesema kuwa lengo la uzinduzi wa Miongozo hiyo ni kuwawezesha wananchi kufahamu zaidi ni nini wanapaswa kufanya katika utunzaji wa misitu ili wafaidike na malighafi zinazotokana na...

Like
228
0
Thursday, 24 March 2016