Slider

TAPELI ATUMIA SAUITI FEKI YA MAKONDA KUWALIZA WACHINA
Slider

Raia wa China wametapeliwa fedha taslimu Sh22.8 milioni wakidai kuwa sauti waliyoisikia kwenye simu ya kiganjani iliyotumiwa na tapeli ilifanana na ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro alisema jana ofisini kwake kuwa Oktoba Mosi, mwaka huu mfanyakazi wa Kampuni ya Group Six ambaye ni raia wa China, Marco Li (24) alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni Makonda. Sirro alisema tapeli huyo alimtaka raia...

Like
262
0
Tuesday, 01 November 2016
RAIS MAGULI: KENYA NI MSHIRIKA WETU MKUBWA AFRIKA
Slider

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema kuwa Kenya ndio mshirika nambari moja wa Tanzania katika uwekezaji na biashara barani Afrika. Akizungumza katika ikulu ya rais jijini Nairobi mda mfupi baada ya kuwasili nchini Kenya,Rais Magufuli amesisitiza kuwa hakuna taifa jingine ambalo limewekeza nchini mwake kama Kenya. Amesema kuwa kulingana na rekodi za uwekezaji nchini Tanzania kuna takriban kampuni 529 nchini humo kutoka Kenya ambazo zinaingiza takriban dola bilioni 1.7 kila mwaka huku takriban Watanzania 57,260 wakiwa wameajiriwa. Rais...

Like
267
0
Monday, 31 October 2016
ITALIA: MAELFU YA WAKAAZI WALALA NJE KUFUATIA KIMBUNGA KIKALI
Slider

Maelfu ya watu katikati mwa Italia wamelala katika magari na mahema ikiwa ni kama makazi ya muda mfupi baada ya kimbunga kikali kupiga katika eneo hilo tokea kile cha mwezi Agosti. Wakaazi katika eneo lililoathirika zaidi la Norcia wamesema walikuwa na hofu sana kuendelea kukaa ndani mwa nyumba zao. Takriban watu 20 wamejeruhiwa na kimbunga hicho kilichotokea siku ya Jumapili, lakini inasemekana mtu mmoja amepoteza maisha. Mkuu wa eneo hilo Luca Ceriscioli amesema zaidi ya watu laki moja watahitaji...

Like
207
0
Monday, 31 October 2016
GARETH BALE AMWAGA WINO KUENDELEA KUKIPIGA REAL MADRID
Slider

Real Madrid imemsainisha mkataba mpya winga wake Gareth Bale na kumfanya aendelee kudumu klabuni hapo mpaka 2022. Bale mchezaji wa zamani wa Southampton alijiunga na klabu hiyo akitokea Tottenham Hotspur mwaka 2013. Tiyari ameisaidia Madrid kushinda vikombe vitano katika misimu mitatu ya nyuma ikiwemo ligi ya mabingwa Ulaya mara 2 huku akifunga magoli 62 katika michezo 135. Viungo wawili wa timu hiyo Luka Modric na Toni Kroos nao pia walisaini mikataba mipya mwezi huu. Mkataba wa Bale unatajwa kuwa wa...

Like
232
0
Monday, 31 October 2016
AHEL YAILIZA NSSF BIL. 270
Slider

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limekiri kuingia mkataba wa ujenzi wa mji wa kisasa wa Dege Eco Village, Kigamboni na kampuni ya Azimio Housing Estates (AHEL) ambayo haikuwa na mtaji hali iliyolazimu kusitisha mradi huo huku likihofia kupata hasara ya Sh270 bilioni. Machi mwaka huu, Mwananchi liliandika “NSSF yaliwa mchana kweupe” likifafanua ufisadi katika mradi huo na mingine ya Mwanza, Pwani, Mtwara na Arumeru, Arusha ambako ekari moja ya ardhi ilithaminishwa kwa Sh1.8 bilioni. Jana, Mkurugenzi Mkuu...

Like
300
0
Thursday, 27 October 2016
WATUMISHI 10 WATIMULIWA MVOMERO
Slider

Watumishi 10 wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, wamefukuzwa kazi kutokana na makosa mbalimbali yakiwamo ya ubadhirifu wa fedha na utoro kazini. Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Florent Kyombo alisema jana kwamba watumishi hao wamefukuzwa kutokana na kushindwa kusimamia ukusanyaji wa mapato, utoro na uzembe. Kyombo alisema watumishi hao wamefukuzwa kwa kuzingatia kanuni na utaratibu wa utumishi wa umma kwenye vyombo husika na kuidhinishwa na vikao vya...

Like
250
0
Thursday, 27 October 2016
MAN UTD YAINYOA MAN CITY
Slider

Manchester United walifika hatua ya robo fainali katika Kombe la EFL baada ya kuwalaza mabingwa watetezi Manchester City kwenye debi iliyochezewa uwanja wa Old Trafford. Juan Mata alifunga bao la pekee mechi hiyo baada ya kupata mpira kutoka kwa mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic. Paul Pogba alikuwa amegonga mlingoti kwa kombora kali awali na kusisimua mechi hiyo kipindi cha pili. Kipindi cha kwanza kilikuwa kikavu bila upande wowote kupata kombora la kulenga goli. Manchester United sasa watakutana na West Ham ambao waliwalaza...

Like
203
0
Thursday, 27 October 2016
KOREA KASKAZINI “HAIKO TAYARI” KUZIACHA SILAHA ZA NYUKLIA
Slider

Sera ya Marekani kuishawishi Korea kaskazini kuachana na mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia huenda ‘haina ufanisi’ , mkurugenzi wa shirika la kitaifa la ujasusi Marekani amesema. James Clapper amesema Marekani jambo ambalo Marekani inaweza kutumainia ni kuzuia uwezo wa taifa hilo, katika hotuba New York. Ni nadra kwa Marekanikukiri kuwa lengo lake kuu la kuwa na dunia isiyokuwana matumizi ya nyuklia huedna isifanikiwe. Hatahivyo, wizara ya mambo ya nje Marekani inasema sera yake hiyo haijabadilika. Korea kaskazini inadai...

Like
290
0
Wednesday, 26 October 2016
MAUZO YA KAMPUNI YA APPLE YASHUKA
Slider

Kampuni ya Apple imeripoti kushuka kwa mapato yake ya mwaka kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2001. Matokeo ya robo ya mwisho ya mwaka wa fedha nchini Marekani imethibitisha mwenendo wa robo mbili zilizopita kuwa mapato yalishuka kwa asilimia tisa. Mapato kutoka China ambako kuna soko kubwa yanaonyesha huenda yatashuka kwa asilimia kubwa. Faida nayo imeshuka kwa asilimia kumi na tisa kwa miezi mitatu ukilinganishwa na miezi hiyo hiyo kwa mwaka jana. Wachambuzi wanasema kuwa ni dalili ya kuwepo kwa...

Like
222
0
Wednesday, 26 October 2016
UTAFITI: BETRI ZINAZOTUMIWA KATIKA SIMU ZINA SUMU
Slider

Zaidi ya gesi 100 zinazoweza kusababisha kifo hutolewa na betri zinazopatikana miongoni mwa mabilioni ya vifaa vinavyotumiwa na raia wengi duniani kama vile simu aina ya smartphone na vipatakilishi kulingana na utafiti mpya. Utafiti huo ulibaini gesi 100 zenye sumu zinazotolewa na betri za Lithium, ikiwemo ile ya kaboni monoksaidi, ambayo inaweza kusababisha kujikuna katika ngozi, macho na pua mbali na kuathiri mazingira. Watafiti kutoka taasisi ya ulinzi ya NBC nchini Marekani pamoja na chuo kikuu cha Tsinghua nchini China...

Like
276
0
Tuesday, 25 October 2016
PAPA FRANCIS AINGILIA KATI MZOZO VENEZUELA
Slider

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amechukua hatua isiyotarajiwa na kuingilia kati kujaribu kutatua mzozo wa kisiasa nchini Venezuela. Taifa hilo pia linakabiliwa na matatizo ya kiuchumi. Wakati wa mkutano wa faraghani na Rais Nicolas Maduro uliofanyika Vatican, Papa Francis ameomba kuongoza mashauriano kati ya rais huyo na viongozi wa upinzani. Mjumbe wa Papa nchini Venezuela Emil Paul Tscherrig amesema pande zote mbili zimeahidi kufanya mashauriano rasmi Jumapili ijayo katika kisiwa cha Margarita, Venezuela. Lakini kupitia...

Like
196
0
Tuesday, 25 October 2016