CHELSEA NA TOTTENHAM WAMEPIGWA FAINI

CHELSEA NA TOTTENHAM WAMEPIGWA FAINI

Like
316
0
Thursday, 05 May 2016
Slider

Chelsea na Tottenham wamepigwa faini kwa pamoja na shirikisho la soka nchini Uingereza FA kwa kukabiliwa na makosa matatu ya kushindwa kuwazuia wachezaji pamoja na maofisa wake wakati na baada ya mchezo wa jumatatu.

Kiungo wa Spurs Mousa Dembele amekumbana na adhabu pia ya kusababisha vurugu katika mchezo huo ulioisha kwa suluhu ya 2-2.FA inasema kuwa kitendo cha Dembele kumuingizia vidole machoni mchezaji wa Chelsea Diego Costa ni utovu mkubwa wa nidhamu.

Hiyo ina maana ”akikutwa na hatia” kufungiwa michezo mitatu pekee haitoshi.Dembele, 28,amepewa mpaka siku ya Alhamisi kujibu mashataka hayo huku kwa pamoja Chelsea na Tottenham wakipewa mpaka siku ya jumatatu.

Katika mchezo huo zilitolewa kadi za njano 12 kutokana na vurugu zilizosababishwa na pande zote mbili. Spurs walihitaji kuifunga Chelsea ili kuweza kurudisha matumaini ya kutwaa taji la ligi kuu England lakini wakaishia suluhu hivyo Leicester kuwa mabingwa.

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino aliingia uwanjani kwa hatua kadhaa kwa lengo la kuwaachanisha mlinzi wa Spurs Danny Rose na kiungo wa Chelsea Willian,huku pia Rose akihusishwa katika tukio lililosababisha mejena wa Chelsea kuangushwa chini.

Mwamuzi wa mchezo huo Mark Clattenburg hakuweza kutoa adhabu kwa Dembele kwa vitendo vyake lakini kamera za uwanjani zilimnasa Mbelgiji huyo akiingiza vidole vyake kwenye macho ya Costa.

Comments are closed.