CHINA YAONYA MATAIFA YA KIGENI KUTOINGILIA HONG KONG

CHINA YAONYA MATAIFA YA KIGENI KUTOINGILIA HONG KONG

Like
518
0
Monday, 29 September 2014
Global News
china

picha ni maelfu ya waandamanaji huko Hong kong nchini china

Uchina imeonya kuwa  kuwa haitawavumilia wahaini kutoka nje ya nchi wanaounga mkono maandamano yasiyo halali nchini humo.

Kundi lijulikanalo kama Occupy Central ndilo linalolengwa kwa sababu limekuwa likiunga mkono juhudi za maandamano ya maelfu ya watu wanaounga mkono kuimraishwa kwa Demokrasia nchini Uchina.

Katika kile kinachoaminika kulenga maandamano yanayoendelea katika jimbo la Hong Kon, Uchina inaonya mataifa mengine yasijiingize kwa kila inachoamini na maswala ya ndani ya Uchina.Uchina mara kwa mara hutoa onyo kwa mataifa mengine yasijiingize katika jimbo hilo lake linalotaka kuendesha mambo yake kivyake.

china

polisi wakipambana na waandamanaji

kauli hiyo ya serikali imekuja siku chache baada ya matamshi ya Chris Patten, aliyekuwa wakati mmoja Gavana wa Hong Kong, aliposema kwamba Uingereza ina wajibu wa kutoa taarifa kwa niaba ya wakazi wa Hong Kong, eneo lililokuwa koloni yake wakati mmoja.

Baraza Kuu la Kitaifa la Uchina, ambalo ni kiungo muhimu katika Serikali, limesema kuwa lina imani kwamba Serikali ya Jimbo la Hong Kong, ina uwezo wa kukabiliana na maandamano hayo kibinafsi bila kuingiliwa na yeyote.

Kuna hofu kuu Hong Kong kuwa huenda Serikali Kuu ikatumia polisi wenye silaha kuzima maandamano hayo.

kumekuwa na mijadala mbalimbali duniani juu ya kauli hiyo ya serikali ya China na maoni tofauti yamekuwa yakitolewa na wasomi pamoja viongozi lakini pia watu mashuhuri duniani

 

 

Comments are closed.