DARFUR KUPIGA KURA YA MAONI LEO

DARFUR KUPIGA KURA YA MAONI LEO

Like
201
0
Monday, 11 April 2016
Global News

JIMBO la magharibi mwa Sudan Darfur, leo linapiga kura ya maoni, miaka 13 baada ya kuanza kwa mzozo wa wenyewe kwa wenyewe uliosababisha watu laki 3, kupoteza maisha.

 

Kura ya maoni itaamua kama Darfur itakuwa na majimbo matano au jimbo moja, ambapo raia watakuwa na siku mpaka ya jumatano kuamua.

 

Marekani imeeleza hofu yake kuwa kura hiyo haitakuwa ya haki, lakini Rais Omar al-Bashir amesisitiza kuwa itakuwa huru na haki. Ikiwa ni hatua ya mwisho ya mchakato wa kuleta amani ambayo makubaliano yake yalitiwa saini mjini Doha .

Comments are closed.