DUTERTE ASEMA OBAMA ANAWEZA ‘KWEND JEHANAMU’

DUTERTE ASEMA OBAMA ANAWEZA ‘KWEND JEHANAMU’

Like
220
0
Wednesday, 05 October 2016
Slider

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amerejelea tena shutuma zake dhidi ya Rais Obama na viongozi wengine wa nchi za Magharibi wanaopinga mpango wake wa kupambana na walanguzi wa dawa za kulevya.

Kiongozi huyo amesema Bw Obama anaweza “kwenda jehanamu”.

Umoja wa Ulaya, ambao pia umemkosoa Bw Duterte, unaweza “kuchagua kwenda eneo la kutakasia dhambi ndogo, kwa sababu jehanamu kumejaa”, amesema.

Watu karibu 3,000 wameuawa tangu kiongozi huyo alipoingia madarakani mwezi Juni.

Watu wanaoshukiwa kulangua mihadarati au kuwa waraibu wa dawa hizo wamekuwa wakiuawa na maafisa wa polisi na magenge yanayoungwa mkono na serikali.

Bw Duterte amesema Urusi na China wako tayari kuwa washirika wake.

Wanajeshi wa Ufilipino na Marekani kwa sasa wanafanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi lakini Bw Duterte amesema mazoezi hayo hayana manufaa kwa raia wa Ufilipino.

Msemaji wa ikulu ya White House Josh Earnest amesema Washington kufikia sasa haijapokea ombi lolote rasmi kutoka kwa Ufilipino kufanyia marekebisho mikataba ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Akiwahutubia maafisa wa serikali na wafanyabiashara, Bw Duterte amesema amesikitishwa sana na Marekani kwa kukosoa mbinu za Ufilipino za kukabiliana na mihadarati.

Ameeleza Marekani kama mshirika asiye wa kutegemewa.

“Badala ya kutusaidia, wizara ya mambo ya nje (ya Marekani) ndio wa kwanza kutukosoa, kwa hivyo wanaweza kwenda jehanamu, Bw Obama, unaweza kwenda jehanamu.”

Baadaye Jumanne, alitahadharisha kwamba: “Mwishowe huenda, nikiwa bado uongozini, nikajitenga na Marekani. Heri kwenda kwa Urusi au Uchina.”

Comments are closed.