EFM RADIO, YAKABIDHIWA ENEO LA UJENZI WA MADARASA YA SEKONDARI-KATA YA KIMARA- KINONDONI.

EFM RADIO, YAKABIDHIWA ENEO LA UJENZI WA MADARASA YA SEKONDARI-KATA YA KIMARA- KINONDONI.

Like
495
0
Thursday, 21 January 2016
Local News

WILAYA ya Kinondoni kupitia Mkuu wa Wilaya hiyo inatarajia kuongeza shule za Sekondari ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi katika Wilaya hiyo. Efm Radio 93.7 katika kuunga mkono juhudi hizo za Serikali imeahidi kujenga madarasa mawili .

1

Mkuu wa Vipindi vya 93.7 efm Dickison Ponela akipokea mchoro wa madarasa, kutoka kwa Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni Bwana, Rogers J. Shemwelekwa Katikati ni Mhariri Mkuu wa Radio hiyo, Scholastica Mazula na Pembeni kushoto ni Injinia wa Wilaya hiyo Bwana Brighton.

2

Mhariri Mkuu wa Efm Scholastica Mazula, akifafanua jambo mbele ya Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni Bwana, Rogers J. Shemwelekwa (Kulia) Na Mkuu wa Vipindi wa Efm Bwana Dickison Ponela (kushoto) wakiwa katika eneo La shule ambako inatarajiwa kujengwa shule ya Sekondari lililopo Kimara mwisho jijini Dar es salaam.

3

Ni nyuso za furaha baada ya Makabidhiano ya Mchoro na eneo la Ujenzi wa Madarasa hayo, Efm inawaomba wadau wote kuunga Mkono Juhudi hizo za Wilaya ya Kiondoni ili dhana ya Elimu bure kwa wote iweze kufanikiwa.

Comments are closed.