ICC YAANZISHA UCHUNGUZI WA AWALI KUHUSU MAUAJI YA BURUNDI

ICC YAANZISHA UCHUNGUZI WA AWALI KUHUSU MAUAJI YA BURUNDI

Like
208
0
Monday, 25 April 2016
Global News

MWENDESHA mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) amesema mahakama hiyo imeanzisha uchunguzi wa awali kuhusu mauaji ambayo yamekuwa yakitokea nchini Burundi.

 

Bi Fatou Bensouda amesema amekuwa akifuatilia kwa karibu matukio ya Burundi tangu Aprili 2015 na kwamba mara kwa mara amezitaka pande zote husika kutojihusisha na ghasia na mauaji.

 

Watu 430 wameuawa na wengine 3,400 kukamatwa tangu kuanza kwa machafuko Aprili mwaka jana.

Comments are closed.