JUMBA LA GHOROFA LAPOROMOKA MOMBASA

JUMBA LA GHOROFA LAPOROMOKA MOMBASA

Like
288
0
Monday, 09 May 2016
Global News

Sehemu ya jumba kubwa la kibiashara mjini Mombasa imeporomoka siku chache baada ya jumba la makazi kuporomoka jijini Nairobi na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40.
Sehemu ya jumba hilo la Nyali Centre iliporomoka usiku wa kuamkia Jumatatu.

Hakuna aliyeripotiwa kujeruhiwa wakati wa mkasa huo.

Polisi, maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu na maafisa wa Mamlaka ya Taifa ya Ujenzi (NCA) wamefika eneo hilo kufanya uchunguzi zaidi.

Comments are closed.