KENYA YAITAKA ICC KUIKABIDHI FAILI ZA WASHUKIWA 3

KENYA YAITAKA ICC KUIKABIDHI FAILI ZA WASHUKIWA 3

Like
177
0
Thursday, 21 April 2016
Global News

KENYA sasa inataka faili za kesi zinazowakabili wakenya watatu wanaotuhumiwa kuingilia ushahidi wa mashahidi wa ICC kushtakiwa nchini humo.

Mwanasheria mkuu Profesa Githu Muigai amesema kuwa Kenya ina mahakama zilizo na uwezo za kushtaki kesi ndogo kufuatia kuanguka kwa kesi kuu iliowahusisha wakenya sita maarufu kama Ocampo 6.

Mwanasheria huyo pia ameshtumu idara ya mashtaka katika mahakama ya ICC kwa kushindwa kushirikiana na Kenya kuhusu ombi la awali lililowasilishwa kwa aliyekuwa kiongozi wa mashtaka Moreno Ocampo kuikabidhi Kenya faili zote za washukiwa.

Comments are closed.