KIBOKO ALIYETISHIA MAISHA YA WATU AULIWA KIJIJI CHA MAGUNGA, IRINGA

KIBOKO ALIYETISHIA MAISHA YA WATU AULIWA KIJIJI CHA MAGUNGA, IRINGA

Like
441
0
Tuesday, 24 May 2016
Local News

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela aliongoza kikosi cha wananchi na maafisa wa wanyama pori kumsaka Kiboko aliyevamia mazao ya wananchi na kutishia maisha ya wananchi hao wa kijiji cha Magunga tarafa ya Kiponzelo. Kiboko huyo alijificha kwenye eneo ambapo wananchi wa kijiji hicho waliogopa kutembea kufanya shughuli za kilimo. mnamo saa 10 na nusu jioni kiboko huyo alipatikana na kuuawa na baadae wananchi kugawiwa nyama yake.

IMG_9373

Ilikuwa kazi ngumu kumtoa kwenye dimbwi alilo angukia baada ya kuuawa kwa risasi. Kumekuwa na matukio ya wanyama wa porini kuvuka mbuga na kuingia vijijini. wiki mbili zilizo pita simba alionekana kijiji cha Idodi

Comments are closed.