MAPYA KUHUSU KUVUNJIKA KWA NDOA YA BRAD PITT NA ANGELINA JOLIE

MAPYA KUHUSU KUVUNJIKA KWA NDOA YA BRAD PITT NA ANGELINA JOLIE

Like
304
0
Thursday, 22 September 2016
Slider

Mwigizaji maarufu kutoka Marekani Brad Pitt amesikitishwa na mkewe Angelina Jolie kudai talaka na kusema watoto wasihusishwe na suala hilo.

Pitt amesema amegadhabishwa na suala hilo lakini amesema kitu muhimu kwa hivi sasa ni maslahi ya watoto wake, kwa mujibu wa gazeti la Marekani la People.

Jolie mwenye umri wa miaka 41 aliwasilisha ombi la kutaka talaka kutoka kwa Pitt mwenye umri wa miaka 52, kutokana na “sababu zisizoepukika” siku ya Jumatatu

Wakili wa Jolie, Robert Offer, alisema Jolie alichukua hatua hiyo ‘kwa manufaa ya familia hiyo’

Inaaminika Jolie anataka kusalia na watoto wao wote sita na amemuomba jaji kumruhusu Pitt haki za kuwatembelea.

Wawili hao walifunga ndoa Agosti 2014, miaka kumi baada yao kuanza kuchumbiana.

Comments are closed.