Your message has been sent, you will be contacted soon

Call Me Now!

Close
Home » Global News » MAREKANI KUPELEKA MAJESHI SYRIA

MAREKANI KUPELEKA MAJESHI SYRIA

MAAFISA wakuu nchini Marekani wanasema kuwa Rais Barack Obama atatuma wanajeshi wa ziada wapatao 250 nchini Syria, ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na vikosi vya ndani vya nchi hiyo, katika kupambana na wapiganaji wa Islamic State.

Kwa mujibu wa maafisa hao, lengo hasa ni kuwasajili waarabu wa dhehebu la Sunni kuungana na wapiganaji wa kikurdi waliopo kaskazini mashariki mwa Syria.

Hata hivyo vikosi hivyo vya Marekani havitawajibika moja kwa moja katika mapambano hayo.

Comments

comments