MASWALI KABLA YA KUMUONA DAKTARI YAWAKERA WAGONJWA

MASWALI KABLA YA KUMUONA DAKTARI YAWAKERA WAGONJWA

Like
297
0
Tuesday, 11 October 2016
Slider

Wapokezi wa wagonjwa hospitalini wanao wahoji wagonjwa kuhusu ni kwanini wanahitaji kumuona daktari huenda yanawasababisha baadhi kutowatembelea madaktari wao , utaifiti umedhihirisha.

Karibu watu wazima 2000 waliohojiwa na taasisi ya utafiti wa Saratani Uingereza, 4 kati ya 10 wamesema hawapendi kujadili magonjwa yao na maafisa wa ofisi ili kupata nafasi ya kumuona daktari.

Wengi walikuwa na wasiwasi ya kupanda hamaki.

Wataalamu wanasema ni lazima wagonjwa wasisitize kumuona daktari na wasikubali kuambiwa haiwezekani, iwapo wanakabiliwa na hali inayohitaji kufanyiwa uchunguzi.

Wapokezi hao ni watu wa kwanza katika mawasiliano kuhusu huduma ya kwanza kwa wagonjwa na ni kazi yao kuamua ni mgonjwa yupi anapaswa kumuona daktari na kwa dharura ya kiasi gani.

Katika utafiti huo vikwazo vitatu vikuu vya kumuona daktari ni:

  • Ugumu wa kupata muda wa kumuona daktari maalum (41.8%)
  • Ugumu wa kupata kumuona daktari kwa wakati unaowardihisha(41.5%)
  • Kutopenda kumueleza mpokezi wa wagonjwa tatizo mtu analougua(39.5%)

Karibu thuluthi ya wagonjwa waliohojiwa pia walikuwa na wasiwasi kwamba watachukuliwa vibaya kama watu wanaopenda kulalamika kwa hasira jarida la Public Health – lililochapisha matokeo ya utafiti – limesema.

Mtafiti mkuu Dr Jodie Moffat amewaomba watu wanaoaugua kuwa wakakamuvu na wasisitize kupata usaidizi badala ya kuteseka kimya.

“usikubali kuvunjwa moyo. Omba muda wa kumuona daktari,” amesema.

“Sisitiza. Najua ni rahisi kusema kuliko kufanya. Lakini ni wazi kuwa mtu anapokuwa mgonjwa, au akizidiwa na ugonjwa ni lazima akaguliwe na daktari.”

Magonjwa yanayohitaji ukaguzi wa dkatari ni kama mtu anapovuja damu, kikohozi kisicho kwisha, mabadiliko wakati wa kwenda haja na kuvimba au kufura pasipo kawaida mwilini.

Comments are closed.