MSN NI MVUA YA MAGOLI, YAISAMBARATISHA CELTIC 7-0

MSN NI MVUA YA MAGOLI, YAISAMBARATISHA CELTIC 7-0

Like
292
0
Wednesday, 14 September 2016
Slider

Celtic walipokezwa kichapo kibaya zaidi katika mashindano ya Ulaya Jumanne usiku baada ya kuchapwa mabao 7-0 na Barcelona uwanjani Camp Nou.

Mshambuliaji Lionel Messi, raia wa Argentina, alifunga ‘hat-trick’ yake ya sita katika mechi hiyo ya kundi C.

Alianza kwa kufunga bao la mapema.

Mchezaji wa Celtic Moussa Dembele alishindwa kufunga penalti kabla ya Messi kufunga la pili.

Kipindi cha pili, Neymar alifunga kupitia frikiki, Andres Iniesta akafunga la nne, Messi akaongeza la tano naye Suarez akakamilisha ushindi kwa mabao ya sita na saba.

Katika misimu miwili ambayo wamekuwa pamoja Nou Camp, Messi, Neymar na Luis Suarez wamefunga mabao 253 na kusaidia ufungaji wa mabao 120.

Comments are closed.