MUZIKI MNENE KIGAMBONI 2015

MUZIKI MNENE KIGAMBONI 2015

Like
479
0
Monday, 12 October 2015
Local News

MUZIKI mnene bar kwa bar wiki iliyopita ulivuka kivuko na kuhamia

kigamboni.Wakazi wa eneo hilo ambao ni wasikilizaji wa 93.7 EFM walipata

burudani ya aina yake kutoka kwa timu nzima ya EFM redio.

Burudani ilianza na kabumbu katika uwanja wa shule ya msingi Ufukoni kati ya

EFM na magogoni veteran.Timu ya magogoni veterani ilitetea ushindi nyumbani

kwa kuifunga EFM magoli manne huku EFM ikiambulia mawili 2.

Kwa kuwa kigamboni kumezungukwa na fukwe kibao, muziki mnene uliendelea

katika fukwe ya Navy beach. Rdj’s walishusha ngoma kali na kuwapagawisha

wakazi wa kigamboni kwa burudani ya kihistoria.

Baada ya pwani ni zamu ya Dar-es-salaam hivo wakazi wa jiji hili wajiandae kwa

kuwa tutawafikia na kuwapa burudani ya kihistoria alisema Denniss Ssebo mkuu wa idara ya mahusiano EFM.

unnamed

 

timu za EFM na magogoni veteran wakiendelea na mechi katika uwanja wa shule ya msingi Ufukoni.

 

2

mamia ya watu waliojitokeza kushabikia kabumbu kati ya 93.7 EFM na magogoni veteran kigamboni.

3

wakazi wa kigamboni wakishuhudia mechi kati ya EFM na magogoni veteran kigamboni.

4

pichani ni timu ya EFM na timu ya Magogoni veteran katika uwanja wa shule ya msingi Ufukoni.

5

pichani ni timu ya EFM na timu ya Magogoni veteran katika uwanja wa shule ya msingi Ufukoni.

 

Comments are closed.