RAIS MAGULI: KENYA NI MSHIRIKA WETU MKUBWA AFRIKA

RAIS MAGULI: KENYA NI MSHIRIKA WETU MKUBWA AFRIKA

Like
268
0
Monday, 31 October 2016
Slider

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema kuwa Kenya ndio mshirika nambari moja wa Tanzania katika uwekezaji na biashara barani Afrika.

Akizungumza katika ikulu ya rais jijini Nairobi mda mfupi baada ya kuwasili nchini Kenya,Rais Magufuli amesisitiza kuwa hakuna taifa jingine ambalo limewekeza nchini mwake kama Kenya.

Amesema kuwa kulingana na rekodi za uwekezaji nchini Tanzania kuna takriban kampuni 529 nchini humo kutoka Kenya ambazo zinaingiza takriban dola bilioni 1.7 kila mwaka huku takriban Watanzania 57,260 wakiwa wameajiriwa.

Rais huyo vilevile ametoa wito kwa Wakenya wanaotaka kuwekeza nchini Tanzania kuharakisha hatua hiyo.

Aidha ameongezea kuwa amekuwa akiwasiliana na rais Uhuru Kenyatta mara kwa mara na kiwakosoa wale wanaodhani kwamba uhusiano wake na rais wa Kenya una utata.

Comments are closed.