Your message has been sent, you will be contacted soon

Call Me Now!

Close
Home » Slider » SABABU YA SAMAKI KUPUNGUA ZIWA TANGANYIKA

SABABU YA SAMAKI KUPUNGUA ZIWA TANGANYIKA

Utafiti mpya umebaini kupungua kwa idadi ya samaki katika Ziwa Tanganyika, mojawapo ya maziwa muhimu zaidi kwa uvuvi duniani, kumetokana na ongezeko la joto duniani katika karne moja iliyopita.

Ziwa Tanganyika ndilo la kale zaidi Afrika na samaki wake huwa muhimu sana kwa lishe katika mataifa yanayopakana na ziwa hilo.Lakini idadi ya samaki imepungua sana, huku wavuvi wakiendelea kuongezeka.

Ongezeko hili la wavuvi lilidhaniwa kuwa chanzo kikubwa cha kupungua kwa idadi ya samaki.Lakini utafiti mpya unaonesha chanzo hasa ni ongezeko la joto duniani kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Ziwa Tanyanyika ndilo la pili kwa ukubwa duniani miongoni mwa maziwa yenye maji yasiyo na chumvi na maji yake huwa katika mataifa manne: Burundi, Jamhuri ya KIdemokrasia ya Congo, Tanzania na Zambia.

Samaki kutoka kwa ziwa hilo hutoa asilimia 60 ya protini zitokanazo na wanyama ambazo huliwa na watu eneo hilo.Aidha, ni eneo lenye aina nyingi ya wanyama na mimea.

Comments

comments