SERIKALI YATANGAZA KUTOA MAFUNZO KWA WASIMAMIZI NA MADEREVA WA KEMIKALI

SERIKALI YATANGAZA KUTOA MAFUNZO KWA WASIMAMIZI NA MADEREVA WA KEMIKALI

Like
328
0
Thursday, 05 May 2016
Local News

SERIKALI imesema kuwa inatarajia kutoa mafunzo kwa wasimamizi 61 wa shughuli za Kemikali na madereva 123wanaosafirisha Kemikali mbalimbali ili kuzuia athari zinazotokana na matumizi yasiyozingatia sheria na kanuni za kemikali.

 

Akizungumza jana Jijini Dar es salaam  wakati wa mkutano na waandishi wa Habari, Mkuu wa Kitengo Cha Utafiti na ubora wa Mifumo Benny Mallya kutoka Ofisi ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali amesema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa sheria ya usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani na majumbani sura namba 182.

 

Akifafanua juu ya madhara yanayosababishwa na Kemikali Mallya amebainisha kuwa katika kipindi cha mwaka 2015matukio ya kemikali yamesababisha vifo vya watu 14.

Comments are closed.