SERIKALI YATOA UFAFANUZI WA URUSHAJI WA MATANGAZO YA BUNGE

SERIKALI YATOA UFAFANUZI WA URUSHAJI WA MATANGAZO YA BUNGE

Like
296
0
Thursday, 28 January 2016
Local News

SERIKALI imesema kuwa kusitishwa kwa baadhi ya matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge haina maana kuwa matangazo hayo hayataoneshwa bali matangazo yataendelea kwa muda husika uliopendekezwa ili kuruhusu Kituo cha matangazo cha Taifa TBC kuendelea na majukumu mengine hata kabla ya kikao cha Bunge kukamilika.

Akijibu swali la mheshimiwa Freeman Mbowe leo Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha maswali ya moja kwa moja kwa waziri mkuu, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Kassim Majaliwa amewataka watanzania kutokuwa na wasi wasi na ratiba hiyo ya urushaji matangazo ya Bunge kwani watapata nafasi ya kufuatilia Bunge kwa wakati husika.

Mbali na hayo Waziri Mkuu amewataka watanzania bila kujali itikadi za vyama vyao vya kisiasa kufanya kazi kwa ushirikiano ili kujiletea maendeleo na kuliinua Taifa kiuchumi.

Comments are closed.