TANZANIA KUTENGENEZA HELIKOPTA

TANZANIA KUTENGENEZA HELIKOPTA

Like
547
0
Wednesday, 22 June 2016
Local News

Gazeti la Daily News limeripoti kwamba ndege hiyo aina ya helikopta inakaribia kukamilika na kwamba habari hiyo imekuwa ikisambaa barani Afrika kwa kasi.

Gazeti la Zambia, Observer linasema kuwa lengo la ndege hiyo itayokuwa ikibeba watu kwa bei rahisi itakabiliana na matatizo ya uchukuzi nchini humo.

Huku gazeti la Cameron, Concord likisema kuwa mradi huo ni wa kihistoria linaongezea kuwa lengo lake ni kutengeza ndege 20 kwa mwaka.

Ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba watu wawili inakaribia kukamilika katika chuo cha ufundi cha Teknolojia cha Arusha na itaanza kufanyiwa majaribio ya kuruka angani baada ya kuruhusiwa na mamlaka ya uchukuzi wa angani nchini Tanzania kulingana na Daily News.

Comments are closed.