UGANDA YAPIGA MARUFUKU MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA

UGANDA YAPIGA MARUFUKU MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA

Like
201
0
Thursday, 05 May 2016
Global News

SERIKALI ya Uganda imepiga marufuku urushwaji wa matangazo ya moja kwa moja yanayopinga uchaguzi wa rais Yoweri Museveni.

Usalama katika mji mkuu wa Uganda- Kampala umeimarishwa kabla ya maandamano yalioitishwa na chama cha Forum for Democratic Change (FDC).

Vyombo vya habari nchini Uganda vimetakiwa kutofanya matangazo ya moja kwa moja na wanachama wa upinzani ambao wanapinga kuchaguliwa kwa rais Museveni.

Comments are closed.