UTAFITI: BETRI ZINAZOTUMIWA KATIKA SIMU ZINA SUMU

UTAFITI: BETRI ZINAZOTUMIWA KATIKA SIMU ZINA SUMU

Like
276
0
Tuesday, 25 October 2016
Slider

Zaidi ya gesi 100 zinazoweza kusababisha kifo hutolewa na betri zinazopatikana miongoni mwa mabilioni ya vifaa vinavyotumiwa na raia wengi duniani kama vile simu aina ya smartphone na vipatakilishi kulingana na utafiti mpya.

Utafiti huo ulibaini gesi 100 zenye sumu zinazotolewa na betri za Lithium, ikiwemo ile ya kaboni monoksaidi, ambayo inaweza kusababisha kujikuna katika ngozi, macho na pua mbali na kuathiri mazingira.

Watafiti kutoka taasisi ya ulinzi ya NBC nchini Marekani pamoja na chuo kikuu cha Tsinghua nchini China wamesema kuwa watu wengi huenda hawajui hatari ya betri kupata moto, kuharibika ama kutumia chaji isiofaa katika vifaa hivyo, jarida la Science Explorer limeripoti.

Katika utafiti huo mpya,walichunguza betri moja ya kuchaji inayojulikana kama Lithium-ion,ambayo huwekwa katika vifaa vinavyotumika kila mwaka.

”Siku hizi,Betri za Lithium-ion hukuzwa na serikali nyingi duniani kama kawi inayopatikana kwa haraka ili kuviwasha vifaa vyote ikiwemo magari ya kielektroniki hadi simu,” alisema Jie Sun, profesa mkuu katika taasisi ya ulinzi ya NBC.

Sun na wenzake waligundua sababu kadhaa ambazo zinaweza kuongeza gesi zenye sumu zinazotolewa.

Betri zilizopata chaji zaidi hutoa gesi zaidi za sumu ikilinganishwa na betri ilio na asilimia 50 ya chaji.

Comments are closed.