VAN GAAL APANGA KUMREJESHA CRISTIANO RONALDO OLD TRAFFORD

VAN GAAL APANGA KUMREJESHA CRISTIANO RONALDO OLD TRAFFORD

Like
221
0
Sunday, 22 November 2015
Slider

Kocha wa Manchester United imethibitishwa anajaribu kumrejesha mshambuliaji matata wa Real Madrid Cristiano Ronaldo Old Trafford .

Louis van Gaal amethibitisha kuwa wanawafuatilia wachezaji kadhaa akiwemo Ronaldo kwa nia ya kuwarejesha Old Trafford ilikuiimarisha ushindani wake msimu huu.

”Kwa hakika tunawafuatilia wachezaji kadhaa sio tu Ronaldo.”

”Kwa kiwango kikubwa wengi wa wachezaji tunaowataka hawaachiki”

van

 

”Kumhusu Ronaldo, kwa hakika tunasubiri thibitisho kwa udi na uvumba” alisema Van Gaal.

Mshambulizi huyo machachari aliihama man United katika msimu wa 2009 akielekea Real Madrid kwa kitita cha pauni milioni 80.

Mreno huyo ameibuka kuwa mfungaji hodari wa mabao wa klabu hiyo bingwa mara kumi barani ulaya.

Ronaldo ambaye ametawazwa kuwa mchezaji bingwa wa dunia mara tatu aliweka rekodi ya kuifunga Real Madrid mabao 323.

Rekodi ya awali ilikuwa inashikiliwa na Raul.

Comments are closed.