VIONGOZI 72 DUNIANI WAHUSIKA NA KAMPUNI YA SIRI

VIONGOZI 72 DUNIANI WAHUSIKA NA KAMPUNI YA SIRI

Like
234
0
Monday, 04 April 2016
Global News

STAKABADHI za siri za shirika moja la kisheria la Panama zilizopatikana na gazeti moja la Ujerumani zimeonyesha viongozi zaidi ya 72 wakuu wa nchi wa zamani na wale waliopo madarakani wanahusika na kampuni hiyo ya kisiri iliyowasaidia wateja wao kukwepa kulipa kodi, utakatishaji fedha, kukiuka mikataba na vikwazo vya kiuchumi vya kimataifa.

Kwa mujibu wa nyaraka za siri zilizopatikana na gazeti moja la Kijerumani, kampuni hiyo ya Mossack Fonseca imewasaidia watu duniani kote kufungua kampuni kwenye visiwa ambavyo havitozi kodi.

Hati hizo zinaonyesha kuwa dola bilioni kadhaa zilitakatishwa na benki moja ya Urusi kwa kumuhusisha mtu mwenye uhusiano na rais wa nchi hiyo Vladimir Putin.

Comments are closed.