VIRUSI VYA ZIKA NI HATARI ZAIDI

VIRUSI VYA ZIKA NI HATARI ZAIDI

Like
169
0
Monday, 02 May 2016
Global News

WANASAYANSI nchini Brazil wamesema kuwa virusi vya ZIKA ambavyo vimehusishwa na kuzaliwa kwa watoto wakiwa na vichwa vidogo huenda ni hatari zaidi kuliko ilivyofikiriwa awali.

Madaktari bingwa wamesema kuwa virusi vya Zika vinaweza kuwa sababu ya kutokea kwa matatizo ya neva za fahamu kwa mwanamke mmoja mjamzito kati ya watano wanaoathiriwa na Virusi hivyo.

Madaktari wengi na watafiti kwa sasa wanakubali kuwa kuna uhusiano kati ya mbu anayeeneza virusi na tatizo la watoto kuzaliwa na dosari kwenye ubongo.

Comments are closed.