WABUNGE WAWILI WA CHADEMA WASIMAMISHWA KUHUDHURIA VIKAO VYA BUNGE KUANZIA LEO

WABUNGE WAWILI WA CHADEMA WASIMAMISHWA KUHUDHURIA VIKAO VYA BUNGE KUANZIA LEO

Like
389
0
Thursday, 30 June 2016
Local News

MHESUGU

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi amesimamishwa kuhudhuria vikao kumi vya bunge kuanzia leo June 30 mwaka huu baada ya kubainika kunyosha kidole cha kati kwa wabunge baada ya kukiri mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka kwamba alifanya kitendo hicho. Hata baada ya kuhojiwa Mbunge Mbilinyi alishindwa kumtaja Mbunge wa CCM aliyedaiwa kumtukana ili nae achukuliwe hatua na kamati hiyo. Bunge limeridhia adhabu hiyo iliyotolewa na kamati.

kubn

Nae Mbunge wa Ubungo Chadema Saed Kubenea amesimamishwa kuhudhuria vikao vitano vya bunge na Naibu Spika Dk Tulia Akson baada ya kubainika kusema uongo kwamba Waziri wa Ulinzi na JKT Dk Hussein Mwinyi ameingia Mkataba na kampuni ya China Henan International Cooperation Group Company wa ujenzi wa nyumba za JWTZ na nyumba ya Waziri huyo jambo ambalo sio kweli.

Comments are closed.