WATU KUFANYA KAZI SIKU MBILI KWA WIKI VENEZUELA

WATU KUFANYA KAZI SIKU MBILI KWA WIKI VENEZUELA

Like
228
0
Wednesday, 27 April 2016
Global News

SERIKALI ya Venezuela imebuni mikakati ambayo itapelekea wafanyakazi wapatao milioni mbili wa serikali, kufanya kazi kwa siku mbili pekee kwa wiki katika kipindi cha majuma mawili.

Hatua hii inalenga kusaidia kukabiliana na uhaba wa umeme ambao unayumbayumba nchini humo.

Wafanyakazi hao wa umma na wale wanaofanya kazi katika sekta zinazomilikiwa na serikali watafika kazini siku za Jumatatu na Jumanne pekee hadi matatizo hayo ya nguvu za umeme yatakapodhibitiwa.

Comments are closed.