Your message has been sent, you will be contacted soon

Call Me Now!

Close
Home » Slider » WATUMISHI 10 WATIMULIWA MVOMERO

WATUMISHI 10 WATIMULIWA MVOMERO

Watumishi 10 wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, wamefukuzwa kazi kutokana na makosa mbalimbali yakiwamo ya ubadhirifu wa fedha na utoro kazini.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Florent Kyombo alisema jana kwamba watumishi hao wamefukuzwa kutokana na kushindwa kusimamia ukusanyaji wa mapato, utoro na uzembe.

Kyombo alisema watumishi hao wamefukuzwa kwa kuzingatia kanuni na utaratibu wa utumishi wa umma kwenye vyombo husika na kuidhinishwa na vikao vya uamuzi.

Comments

comments