ZITTO AHOJIWA NA POLISI

ZITTO AHOJIWA NA POLISI

Like
225
0
Wednesday, 08 June 2016
Local News

JESHI la polisi kanda maalumu ya dar es salaamu limemuita na kumuhoji mbunge wa kigoma mjini ZITTO KABWE kwa ajili ya kupata ufafanuzi juu ya maudhui ya hotuba aliyo itoa jumapili iliopita katika viwanja vya Zakhiemu Mbagala .

Mheshimiwa KABWE alifika katika ofisi ya polisi kanda maalumu ya Dar es salaamu majira ya saa tatu na dakika thelathini na mbili asubuhi ambapo alihojiwa kwa masaa mawili na baada ya hapo mheshimiwa KABWE alizungumza na waandishi wa habari ambapo alionesha kusikitishwa na uamuzi huo huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatiwa kwa haki ya mkusanyiko kwa wananchi .

Comments are closed.