MHADHIRI na Mtafiti wa Masuala ya Kiislamu kutoka Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar -SUZA Dokta ISSA HAJI ZIDI amesema, Dini ya Kiislamu haipingani na Uzazi wa Mpango kwani ulikuwepo tokea wakati wa Mtume MUAHAMAD, hivyo amewashauri Waislamu kuzitumia kwa ajili ya kulinda afya zao.
Akizungumza kwenye mjadala kuhusu Uzazi wa mpango katika Uislamu ulioandaliwa na Kitengo Shirikishi cha Afya ya Uzazi na Mtoto, Dokta ZIDI amesema, lengo la Uzazi wa Mpango ni kulinda Afya ya Mama na Mtoto aliyezaliwa kabla ya Mtoto mwingine.
Amesema zipo njia za Asili za Uzazi wa mpango zilizokuwa zikitumiwa na Masahaba wakati wa Mtume MUHAMMAD lakini hivi sasa njia hizo zinaonekana kuwa ngumu kwa watumiaji na zipo njia za Kisasa ambazo ni salama na za uhakika zaidi.