Category: World

Ut wisi luctus ullamcorper. Et ullamcorper sollicitudin elit odio consequat mauris, wisi velit tortor semper vel feugiat dui, ultricies lacus. Congue mattis luctus, quam orci mi semper

  • Ronaldo kumuwakilisha Messi Ligi ya mabingwa

    Ronaldo kumuwakilisha Messi Ligi ya mabingwa

     

    Cristiano Ronaldo

    Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya inaendelea tena usiku wa leo ambapo mabingwa wa Bundesliga, Bayern Munich watakuwa wanaikaribisha Real Madrid.

    Real Madrid tayari wameshatua mjini Bayern ambapo nguvu zao kubwa wameziweka kwenye mashindano hayo hivi sasa.

    Madrid haina nafasi tena katika taji la La Liga kutokana na ubora wa mpinzani wake, FC. Barcelona ambaye ameshajiwekea mazingira mazuri ya kutwaa Kombe hilo huku akitupwa nje ya UEFA Champions League na AS Roma.

    Nyota Cristiano Ronaldo anapewa nafasi ya kuendelea kucheka na nyavu kwenye mashindano haya ambapo mpaka sasa anaongoza kwa kuwa na mabao mengi.

    Ronaldo atakuwa anamuwakilisha Messi kutokana na ushiriki wa Madrid ambayo inacheza La Liga pia nchini Spain leo.

  • Trump aapa ”kutumia nguvu” kujibu shambulio ”la kemikali” Syria

    Trump aapa ”kutumia nguvu” kujibu shambulio ”la kemikali” Syria

     

    Rais wa Marekani Donald Trump ameahidi ” kutumia nguvu ” kujibu madai ya shambulio la kemikali nchini Syria, huku mataifa ya magharibi yakitafakari hatua watakayoichukua.

    “Tuna njia nyingi za kijeshi,”aliwambia waandishi wa habari.

    Aliongeza kuwa hatua ya kujibu shambulio hilo itaamuliwa katika kipindi cha “muda mfupi”.

    Bwana Trump alisema kuwa Marekani inapata ”msaada mzuri” juu ya nani aliyehusika na shambulio la Douma Jumamosi.

    Duru za kitabibu zinasema makumi kadhaa ya watu waliawa katika shambulio hilo, lakini idadi kamili haijathibitishwa.

    Bw Trump pia alijadili tukio hilo la rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Jumatatu jioni, na viongozi wote walielezea utashi wao wa “kujibu kikamilifu”.

    Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amesema kuwa “analaani vikali” kitendo cha “ukatili” kinachodaiwa kuwa ni shambulio la kemikali na akatoa wito kwa wanaomuunga mkono rais Bashar al-Assad kuwajibishwa.

    Kauli za viongozi wa kimagharibi za kulaani shambulio hilo zimefuatia kikao cha malumbano katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambapo Marekani na Urusi walitupia na maneno makali kuhusiana na tukio la Douma.

    Muwakilishi wa Urusi kwenye baraza hilo Vassily Nebenzia alisema shambulio linalodaiwa lilipangwa na akaonya kwamba hatua za kijeshi za Marekani zinazolenga kujibu tukio hilo “litakuwa na athari mbaya”.

    Mjumbe wa Marekani Nikki Haley alisema kuwa-wanaounga mkono jeshi la Syrian – wana “damu ya watoto wa Syria ” mikononi mwao na akambandika jina rais Assad kama “zimwi “.

    Bi Haley alitoa wito wa kupigwa kura juu ya muswada wa maazimio ya kubuniwa kwa tume ya uchunguzi juu ya matumizi ya silaha za kemiikali nchini Syria siku ya Jumanne.

    Lakini Urusi inasema haiwezi kuunga mkono pendekezo hilo kwasababu lina “vipengele visivyokubalika”.

    Shirika la matibabu la Marekani na Syria linasema kuwa watu zaidi ya 500 waliletwa kwenye kituo cha matibabu katika mji wa Douma, uliopo katika jimbo la mashariki la Ghouta , karibu na mji mkuu Damascus, wakiwa na dalili “zinazoonesha kuwa walishambuliwa na kemikali”.

    Shirika hilo linasema dalili walizaokuwa nazo ni pamoja na ugumu wa kupumua, ngozi ya samawati , kutokwa na povu mdomoni , kuungua kwa mboni na “walikuwa na harufu kama ya kemikali ya chlorine”.

    Idadi kamili ya vifo ya na ni nini hasa kilichotokea haviwezi kuthibitishwa kwasababu eneo hilo halina mawasiliano.

    Makadirio ya idadi ya watu waliouawa katika shambulio linaloshukiwa kuwa la kemikali ni kuanzia watu 42 hadi zaidi 60, lakini makundi ya kitabibu yanasema idadi hiyo inaweza kuongezeka baada ya wahudumu wa uokoaji kuweza kufika kwenye sehemu za chini za majengo ambako mamia ya familia walikuwa wamekimbilia kuepuka mashambulio ya mabomu.

    Muwakilishi wa Ufaransa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa amesema gesi ya sumu ilitumiwa kwa makusudi kwasababu inaweza kusambaa hadi sehemu za chini za majengo hadi.

    Marekani ,ufaransa na Uingereza wameongoza kampeni ya kimataifa ya kulaani shambulio hilo linalodaiwa kuwa la kemikali, huku serikali ya Syria na waungaji mkono wao Urusi wakikana kuwajibika kwao kokote na tukio hilo.

  • Brazil: Lula da Silva kufungwa miaka 12 jela

    Brazil: Lula da Silva kufungwa miaka 12 jela

    Luiz Inacio Lula da Silva

     

    Mahakama ya rufaa nchini Brazil imeagiza kuwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Luiz Inacio Lula da Silva, ni sharti aanze kutumikia kifungo chake cha miaka kumi na miwili gerezani, baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika na ufisadi.
    Majaji sita kati ya kumi na mmoja wa mahakama ya rufaa walipinga rufaa hiyo huku watano kati yao wakimuunga mkono. Kesi hiyo imezua hali ya wasi wasi wa kisiasa nchini humo.

    Hatia hiyo imetokana na uchunguzi wa muda mrefu wa sakata la rushwa linalojulikana kama ”Operation Car Wash”
    Lula aligundulika kukubali rushwa yenye thamani Euro laki saba na tisini.

    Lula da silva amekua akitarajiwa na watu wengi kusimama kama mgombea asie na ushindani katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi octoba,
    Lakini ndoto hizo zimeisha baada ya mahakama kuu kuamuru mwanasiasa huyo mkongwe aanze kifungo cha miaka 12 gerezani baada ya kukutwa na hatia ya ufisaidi.
    Maandamano yamefanyika katika miji mbalimbali, waandamanaji katika mji wa Sao Bernardo wanataka Da silva aachiwe huru.
    ” mkusanyiko wetu wa leo ni kuhakikisha kuwa rais wetu wa zamani Lula, ana haki ya kurudi kuwa mgombea wa Urais na kama kweli hawataki kumuona basi njia pekee ni kumshinda katika uchaguzo”
    Baadhi ya watu wanapinga kuachiwa huru kwa Lula Da Silva na badala yake jeshi ndio liongoze nchi hiyo.
    ”Kama mahakama kuu haitamuweka Lula jela, basi tunataka jeshi ndio lishike madaraka kwasababu taasisi zimejaa rushwa , zote hadi mahakama”
    Mbali na kukutwa na hatia Lula amekua akipinga vikali kuhusika na kashfa yoyote ya rushwa anasema kuwa amekua akipinga vikali uonevu wa aina yoyote hivyo hatakubali uonevu wa mahakama.

    Kiongozi huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 72 atabaki uraiani kwa muda hadi pale nyaraka za kifungo chake zitakapo kamilika.
    Lula Da silva amekua madaraki kati yam waka 2003 hadi 2011. Kama angeingia kama mgombea katika uchaguzi wa mwezi oktoba huenda angeshinda kwa kishindo kutokana na umaarufu wake.

     

  • RONALDO REKODI MPYA UGENINI

    RONALDO REKODI MPYA UGENINI

    Ni Cristiano Ronaldo tena anaendelea kuwanyamazisha wapinzani wa Real Madrid, dakika ya 3 tu alipiga shuti lake la 9 kwa Gianluigi Buffon na kufunga bao lake la 8 dhidi ya golikipa huyo, hili likiwa bao la kwanza katika mchezo huu.

    Dakika ya 64 Cristiano Ronaldo tena aliifungia Real Madrid bao la pili na kumfanya kuwa mchezaji katika historia aliyewafunga Juve mabao mengi (9) kabla ya Marcelo kufungia bao la 3 Real Madrid.

    Hii ni mara ya kwanza Juventus wanaruhusu kufungwa mabao 3 nyumbani tangu mwaka 2009 walipofungwa bao 4-1 na Bayern Munich, Juventus walimaliza wakiwa pungufu baada ya Paulo Dyabala kuoneshwa kadi nyekundu.

    Kama hujui tu ni kwamba bao la kwanza la Madrid ndio bao la mapema zaidi kwa Cristiano Ronaldo kuwahi kufunga katika Champions League, huku sasa Mreno huyo akiwa na mabao 38 katika msimu huu(michuano yote) ikiwa ni idadi kubwa kuliko mchezaji yeyote barani Ulaya.

    Tangu klabu ya Juventus wahamie katika uwanja wao mpya mwaka 2011 hawajawahi kupokea kipigo kama hiki katika uwanja huo katika mashindano yoyote yale.

     

  • TETESI: Man United kumuongezea mkataba mrefu zaidi De Gea, kumpatia mshahara wa kufa mtu

    TETESI: Man United kumuongezea mkataba mrefu zaidi De Gea, kumpatia mshahara wa kufa mtu

    Klabu ya soka ya Manchester United hawana mpango kabisa ya kumuachia David de Gea kwenda Real Madrid.

    Man United inampango wa kumuongeze mkataba wa miaka mitano mchezaji huyo na kumlipa mshahara wa paundi 350,000 kwa wiki kabla ya kuanza kwa kombe la dunia, hiyo ni kwa mujibu wa gazeti la The Sun.

    De Gea ambaye alitua United mwaka 2011 akitokea Atletico Madrid, anatarajia kumaliza mkataba wake mwaka 2019.

    Golikipa huyo amekuwa tegemezi katika kikosi cha Man United huku katika msimu huu akiwa anaongoza katika ligi kuu ya Uingereza kwa kuwa na clean Sheet 16 akifuatiwa na golikipa wa Manchester City, Ederson mwenye clean sheet 14.