Tag: DONALD TRUMP

  • Trump arudi nyuma katika sera yake ya kuzitenganisha familia

    Trump arudi nyuma katika sera yake ya kuzitenganisha familia

    Rais Donald Trump wa Marekani amesitisha sera yake uhamiaji iliyokuwa inalazimu kuzitenganisha familia za wahamiaji wanaobainika kuvuka mipaka kinyume cha sheria na watoto wao.

    Pamoja na kulegeza msimamo huo kutokana na kulalamikiwa kwa sera hiyo ndani na nje ya taifa hilo, Trump amesisitiza kwamba bado ataendelea kuilinda mipaka yake.

    Rais Trump ambaye tangu kuingia kwake madarakani alionekana kuhitaji sheria kali zaidi ya kukomesha suala la uhamiaji haramu, amejikuta matatani, safari na hasa baada ya picha zenye mguso za watoto waliotenganishwa na wazazi wao katika mpaka wa Marekani na Mexico kuanza kusambaa na kuleta mshituko mkubwa kwa raia wa Marekani.

    Bunge, makundi ya haki za binadamu na hata Bi.Melania Trump yaani mkewe rais Trump mwenyewe na wake wa marais wastaafu.

    Haki miliki ya picha Reuters

    Hata hivyo bado kuna mashaka kama amri hiyo mpya ya Rais Trump dhidi ya sera yake hiyo kama itawawezesha wanafamilia kuwa pamoja kwa zaidi ya siku 20, na bunge leo siku ya alhamisi linatarajiwa kuipigia kura miswada miwili ambayo inalenga kuondoa utata huo wa kuziumiza familia na mapendekezo mengine ya masuala ya kiuhamiaji.

    Akiwahutubia wanachama wake huko Minnesota, rais Trump amesema atatekeleza ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni zake ya kujenga ukuta kati yake na Mexico kwa kile alichodai ni jitihada za kulinda mipaka yake.

    “Tunapaswa kuwa na mipaka imara, hatuwezi kukatishwa tamaa na masuala ya kipuuzi. Lakini wakati huo huo tunayafanya hayo kwa uangalifu mkubwa.

    Nimesaini amri ya kuhakikisha familia zinakuwa pamoja, kwa sababu naona ni jambo muhimu kuamua hivyo. Lakini hatutaacha, tupo imara katika suala la mipaka ,tunahitaji kuwa na ukuta na ni lazima ujengwe” amesema Trump.

    Hata hivyo amri hiyo ya rais Trump bado haitoi muda maalumu wa utekelezwaji wake na haionyeshi ni kwa namna gani Zaidi ya watoto 2,00 waliotenganishwa na familia zao watakutanishwa.

    Waziri wa afya na huduma za kibinadam Alex Azar amesema idara yake itaanza kuwarejesha watoto kutoka katika maeneo waliyowekwa na kuwaunganisha na wazazi wao lakini hajabainisha ni lini suala ambalo linaleta mashaka kwamba huenda ikawa ni kauli ya kisiasa tu.

  • RAIS TRUMP AWATUMIA SALAAM ZA MWEZI MTUKUFU WAISLAM WASHIO MAREKANI

    RAIS TRUMP AWATUMIA SALAAM ZA MWEZI MTUKUFU WAISLAM WASHIO MAREKANI

    Rais wa Marekani, Donald Trump ametuma ujumbe kwa Waislamu wote nchini Marekani na kwingineko duniani kwa kuadhimisha kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na White House, wakati ambapo watu wengi wanaungana pamoja kusherehekea mwezi mtukufu wa Ramadhan, Rais Trump na mkewe Melania wana matumaini kuwa mwezi huu utakuwa wa baraka.

    Taarifa imesema kuwa Marekani imebarikiwa kuishi kwa mujibu wa katiba ambayo inaheshimu uhuru wa dini na inaheshimu uhuru wa kuabudu wa kila mwananchi. Katiba yetu inahakikisha kuwa waislamu wanaweza kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa mujibu wa imani yao ya dini na bila ya kuingiliwa na serikali.

    Wakati wa mwezi huu wa Ramadhan, Waislamu wanasherehekea kuteremeshwa Quran tukufu kwa Mtume Mohammed. Wengi wanaadhimisha mwezi huu kwa kufunga, kufanya vitendo vyema, kusali na kusoma Quran.

    Ramadhan ni wakati wa kujitathmini kwa azma ya mtu kujifahamu kwa undani nafsi yake na kuwa na dhana ya kushukuru kwa Baraka nyingi ambazo wanazipata kutoka kwa Mwenyenzi Mungu.

    Katika azma hii ya kushukuru na kujitathmini, wale wanaoadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhan wanasema kuziimarisha jamii zetu, kuwasaidia wale wenye shida, ni mfano mzuri wa jinsi ya kuishi maisha safi kwa waumini wa dini.

    Taarifa hiyo imeongeza kuwa Ramadhan inatukumbusha utajiri wa Waislamu ukiongezea na dini katika maisha ya Marekani. Nchini Marekani, tumebarikiwa kuishi kwa mujibu wa katiba ambayo inahamasisha uhuru wa dini na kuheshimu dini.

    Katiba ya Marekani inahakikisha kuwa Waislamu wanafunga Ramadhan kwa mujibu wa misingi ya dini na bila ya kuingiliwa na serikali, taarifa imesema.

    Kwa kufanya hivyo katiba pia inatoa fursa mbali mbali kwa Wamarekani wote kuelewa nafasi ya binadamu.

     

  • UNAJUA USAFIRI ANAOTUMIA RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP AKIWA MATEMBEZINI?

    UNAJUA USAFIRI ANAOTUMIA RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP AKIWA MATEMBEZINI?

     

    Rais wa Marekani Donald Trump akiwa katika mazingira ya kawaida ya kikazi hutembelea gari aina ya limousine.

    Gari hiyo ni moja kati ya magari ghali zaidi na yenye ulinzi mkali zaidi duniani kote ulinzi wake ni pamoja na vioo vyenye nguvu ya kuzuwia risasi, milango yake ina uzito sawa na milango ya ndege aina ya boeng 747, ikiwa itatokea janga la  moto tank la mafuta ya gari hiyo limefunikwa na vyuma kiasi hata mlipuko wa bomu hauwezi lipua tenki hilo.

    Matairi ya gari hiyo yametengenezwa maradufu kuweza kuzuwia pancha na ikitokea yamepasuka gari hilo liko na rims chuma ambazo zinawezesha gari kuendelea na safari yake.

    Gari hiyo ina silaha zenye risasi za kutosha, vilipuzi vya gesi za machozi, miwani ya kuonea usiku ikiwa wataamua kutembea bila ya taa, na vifaa vya moto vinavyotokana na moto kwa kukabiliana na hali yoyote. kuna bunduki nyuma ya grille mbele, na pembeni mwa gari hilo.

    Gari hiyo aina ya limo iliyopewa jina la the beast ina uzito wa tani 8 ambayo ni sawa na malori ya kusafirishia mizigo

     

    https://youtu.be/J9Vi3NrguJM

  • DONALD TRUMP AMFUKUZA KAZI WAZIRI WAKE WA MAMBO YA NJE

    DONALD TRUMP AMFUKUZA KAZI WAZIRI WAKE WA MAMBO YA NJE

    Rais Donald Trump amemfukuza kazi waziri wake wa mambo ya nchi za nje Rex Tillerson na kumchagua mkurugenzi wa idara ya ujasusi ya CIA, Mike Pompeo kuchua nafasi yake.
    Nafasi ya Pompeo katika CIA itachukuliwa na aliyekua naibu wake Gina Haspel.

    Katika ujumbe wa twitter, Rais Trump alimshukuru Tillerson akisema, “Mike Pompeo, Mkurugenzi wa CIA atakua waziri mpya wa mambo ya kigeni. Atafanya kazi nzuri kabisa. Ahsante Rex Tillerson kwa huduma yako! Gina Haspel atakua mkurugeni mpya wa CIA na anakua mwanamke wa kwanza kuteuliwa kwa kazi hiyo. Hongera kwa wotre.”

    Wachambuzi wanasema ingawa ni habari kubwa lakini ilikua inatarajiwa kutokana na hali ya kutoelewaqna kati ya Trump na Tillerson ambao hawakua na msimamo moja katika sera na Tillerson kutoa mara kadhaa matamshi yaliyokua tofauti na msimamo wa Trump.