Tag: featured

  • Msanii LADY JAY DEE (@jidejaydee) ameula katika michuano ya Kombe la Dunia 2014

    Msanii LADY JAY DEE (@jidejaydee) ameula katika michuano ya Kombe la Dunia 2014

    Msanii Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ ameula katika michuano ya Kombe la Dunia 2014 baada ya kupata nafasi ya kuandaa wimbo kwa a jili ya michuano hiyo mikubwa zaidi ya soka duniani.

    Jaydee anayefahamika pia kama Komandoo au Anaconda, amepata fursa ya kuandaa wimbo maalum wa michuano hiyo ‘FIFA World Cup Anthem’ akishirikiana na wakali wawili David Correy wa Brazil na rapa Octopizzo wa Kenya.

    Katika wimbo huo, Lady Jaydee na Correy wameimba kwa lugha ya Kiingereza huku Octopizzo ‘akichana’ kwa Kiswahili.

    Wimbo huo ulipigwa kwa mara ya kwanza jana jijini Dar es Salaam wakati kampuni ya Coca-Cola ilipozindua promosheni yake mpya ya miezi miwili ya Kombe la FIFA la Dunia 2014 ambayo itawawezesha wateja wake kujishindia zawadi mbalimbali zikiwamo tiketi za kwenda kushuhudia mechi za robo fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil.

    Meneja Mkazi wa Coca-Cola Tanzania, Yebeltal Getachew alisema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi ya kampeni hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam huku akizitaja zawadi nyingine kuwa luninga, mipira na fulana. Wakati huo huo, Jmosi tarehe 12 April Lady Jaydee anataraji kuachia wimbo wake na video mpya ‘Nasimama’.
    CHANZO: Nipashe

  • VODACOM YATEMBELEA VYOMBO VYA HABARI KUIMARISHA UHUSIANO

    VODACOM YATEMBELEA VYOMBO VYA HABARI KUIMARISHA UHUSIANO

    Waendeshaji wa kipindi cha Morning Choice kinachorushwa na kituo cha Radio cha Choice FM Baby Kabai (kulia) na Evans Bukuku wakionesha manjonjo kwa Mkuu wa Masoko wa Vodacom Kelvin Twissa na Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Rosalynn Mworia (hawapo pichani) walipotembelea vyombo vya habari vilivyo chini ya Clouds Media Group.

  • Matumaini Katiba Mpya arijojo

    Matumaini Katiba Mpya arijojo

    Ikulu imeeleza kuwa imeshindwa kutimiza ahadi yake kwa taifa ya kulipatia Katiba Mpya ifikapo Aprili 26, 2014.

    Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue alilieleza gazeti hili kuwa kwa hali ya mchakato huo ilivyo sasa, wameshindwa kufikia lengo hilo, lakini hawajakata tamaa kuhusu kupatikana Katiba Mpya ndani ya mwaka huu.

    “Kweli matarajio ya awali yalikuwa hayo, lakini kama unavyoona hali ilivyo, ni vigumu kusema matarajio mengine, ingawa majadiliano yaliyofanywa mwaka huu ni lazima Katiba inayopendekezwa iwasilishwe kwa wananchi na mwakani tutakuwa na Katiba Mpya,” alieleza Balozi Sefue.

    Katika hali isiyoeleweka Balozi Sefue alisisitiza msimamo wa awali wa Serikali kwamba Katiba itakayopatikana itatumika kwenye Uchaguzi Mkuu, unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao.

    Dk Slaa

    Katibu Mkuu wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema), Dk. Willbroad Slaa, alisema hilo ni fundisho kwa Serikali kwamba kiburi na jeuri havitakiwi katika masuala yanayohusu umma.

    Alisema muda huo wa kupatikana Katiba Mpya ulipotangazwa, walioanzisha kilio cha kudai Katiba Mpya nchini ambao aliwataja kuwa ni vyama vya upinzani vya siasa, taasisi mbalimbali za kijamii walipinga na kutoa ushauri kwa Serikali, lakini walipuuzwa.

    Dk. Slaa alisema walipendekeza kwamba badala ya kupeleka mchakato wa Katiba mchakamchaka, warekebishe kwa mara ya 15 Katiba inayotumika, ili iende na wakati wa sasa ikiwamo Uchaguzi Mkuu ujao kwa lengo la kutoa muda wa kutosha kwa mchakato wa taifa kupata Katiba Mpya.

    “Lakini walitukebehi na kututukana sana, sasa kiko wapi Aprili 26 hiyo hapo na Katiba haijapatikana na kusema itapatikana mwaka huu na kutumika kwenye Uchaguzi Mkuu mwakani ni ndoto za mchana,” alieleza Dk. Slaa.

    Dk. Slaa alisema tukio hilo liwe fundisho kwa Serikali, wawe wakweli, wanyoofu na wafahamu kuwa nje ya Serikali kuna watu makini na wanaojua vilivyo mchakato wa Katiba.

    Alisema ana taarifa za Bunge Maalumu kuahirishwa Mei 9, 2014 ili kupisha Bunge la Bajeti. Hivyo mategemeo ya Katiba Mpya kwenye Uchaguzi Mkuu ujao, yanatia shaka.

    “Kwa akili ya kawaida tu isiyohitaji elimu ya chuo chochote, kutumia Katiba Mpya kwenye Uchaguzi Mkuu ujao ni jambo lisilowezekana kwa hiyo waache kutuletea matumaini yasiyokuwapo, sisi siyo watoto wadogo,” alieleza Dk. Slaa.

  • Mh. Edward Lowassa amuaga mkuu mkoa wa Mara

    Mh. Edward Lowassa amuaga mkuu mkoa wa Mara

    Waziri Mkuu mstaafu an mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akiwasili katika viwanja vya Mwalimu Nyerere kumuaga mwili wa Mkuu wa Mkoa wa Mara marehemu John G Tuppa.Pembeni ni mbunge wa Mwibara Kangi Lugola

  • Dar es Salaam ikinyesha mvua kidogo tu basi NI SHIDAAAA

    Dar es Salaam ikinyesha mvua kidogo tu basi NI SHIDAAAA

    20140327_065455

    Haya ni maeneo ya Mikocheni Tanesco ambapo huwaga hivi kama siku itanyesha mvua kubwa…husababisha foleni kubwa ya magari kwa wafanyakazi waendao makazini nyakati za asubuhi.

    20140327_06562720140327_06570520140327_065722