Mshambuliaji mpya wa klabu ya Costal Union ya Tanga, Ali Kiba, ameanza kujinoa na wachezaji wa kikosi hicho huko Tanga tayari kwa msimu mpya wa ligi utakaoanza Agosti 22 2018.
Tag: kiba
-

ALIKIBA AANZA KAZI COASTAL UNION
Kiba ambaye pia ni Msanii wa Kimataifa kupitia Muziki wa kizazi kipya, ameanza kambi hiyo baada ya kujiunga na Coastal akisaini mkataba wa mwaka mmoja.Nyota huyo amekuwa gumzo kubwa ndani ya jiji la Tanga na kwa mashabiki na wanachama wa Costal kutokana na usajili wa Kiba ambao haukutarajiwa na wengi.Ikumbukwe Kiba amekuwa na umaarufu mkubwa zaidi katika tasnia ya muziki tofauti na mpira, japo ana kipaji kikubwa cha kusakata kambumbu.Caostal wameanza kujifua tayari kwa maandalizi ya msimu mpya ambao utakuwa na idadi ya timu 20 kutoka 16 ilivyokuwa kwa 2017/18. -

Wachambuzi wa Soka Wasema Alikiba Anaweza Kucheza Ulaya
Baadhi ya Wachambuzi wa Soka nchini akiwemo kocha wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo amesema msanii wa Bongo Fleva nchini, Ally Salehe Kiba ‘Alikiba’ ni mchezaji mwenye uwezo wa kucheza Ligi Kuu Bara, na kama akiandaliwa vizuri anaweza kucheza hata Ulaya.
Julio ameyasema hayo akiwa kocha wa Team Samatta mara baada ya kumalizika kwa mchezo maalum wa kuchangia elimu ulioandaliwa na msanii huyo akishirikiana na Mbwana Samatta anayecheza soka la kulipwa katika Klabu ya Genk nchini Ubelgiji. Katika mchezo huo uliopigwa juzi Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar, Team Samatta iliibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Team Kiba.
Julio alisema msanii huyo ni mchezaji mzuri na amekuwa akimwambia kuwa yupo tayari kumsajili achezee katika timu yake kutokana na uwezo mkubwa alionao na kama akiwekwa vizuri ana uwezo wa kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.
“Alikiba ni mchezaji mzuri sana, mimi binafsi huwa namwambia ‘nataka nikusajili’, kama hawezi kuja kule mkoani lakini tukija hapa Dar aje acheze, ana uwezo mkubwa sana kuliko wachezaji wengi wa Simba na Yanga ambao wanalipwa mishahara ya bure.
“Isipokuwa tu nchi yetu haitaki kujua watu wenye uwezo, tunafuata majina na labda wana sababu zao, ndiyo hivyo lakini Kiba kama anatengenezwa hakuna ambaye anaweza kusema kuwa Kiba siyo mchezaji na kwa uwezo wake kama anacheza basi hapa atacheza ligi hii, mwaka wake mmoja tu anakwenda kucheza soka la kulipwa,” alisema Julio.

